Mtaka Haki
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 492
- 149
Nimewaza kuwa ni muhimu na kwa haraka tukaweka bayana kuwa endapo rais Mh. Dr. Jakaya Kikwete ataamua kutokutia saini muswada wa katiba. Basi ijulikane sio unyonge bali ni busara, hekima na heshima kwake. Kwa upande wa CDM ni muhimu nao wakatae kulitumia hilo au watu watakaolitumia hilo kama ushindi. Haya mambo yaonekana kama madogo lakini yasipowekwa sawa yanazuia ufanisi huko mbele.
Chadema wakatae kupokea sifa katika hili na wao waseme kwa nguvu kuwa ni busara ya Rais na utashi wake. Naye rais ni muhimu akasisitiza kuwa ameheshimu mawazo chanya yaliyopelekwa kwake na kama baba ameamua kuwasikiliza watoto wote.
Hongera Mh Dr. Jakaya Kikwete kwa busara zako na usikivu wako. Hongereni viongozi wa CHADEMA.
Hongereni wananchi wa Tanzania kwa umoja na mshikamano wenu.