Rais Kikwetwe;Tengua uwaziri wa Kagasheki mara moja

TRANQUILITIST

Member
Oct 28, 2012
84
35
Rais wangu wa jamuhuri ya muungano ya Tanzania, tunakuomba tengua uwaziri wa Kagasheki mara moja kutokana na sababu zifuatazo:

1; Waziri Kagasheki amekiri mbele ya wananchi wa Bukoba kuwa alipindisha sheria kwa kuwapatia passport ya kusafiria watoto wa Meya wa manispaa ya Bukoba ambao hawakuwa raia halali wa tz kwa wakati huo. Akiwa naibu waziri wa mambo ya ndani kwa wakati huo aliamuru watoto hao wapewe vibali vya kusafiria kinyume na katiba ya nchi.

2;Amekiri kusababisha migogoro ndani ya chama kwa kutengeneza makundi wakati wa kumchagua meya, ambapo amekiri kufarakana na mwanachama mashuhuri bw. LUANGISA
.

KWA HALI HIYO HAFAI KUWA WAZIRI MWENYE DHAMANA, PIGA CHINI.
 
muombe rais pia awawajibishe na walio mpigia huyo meya kura kuwa meya.lakini kumbuka ukitaka kula lazima na ww uliwe ndio maana kaga alitoa hizo passport
 
Una stress wewe sio bure

NO NDUGU NAMUUNGA MKONO MLETA HOJA NAAMINI ATA MAJIRANI ZETU WANATUCHEKA SANA KUWA NA RAISI DHAIEU AJABU, ANGALIA WALA RUSHWA WAKUBWA NDO MARAFIK ZAKE, KAMTEUA JANGILI KWA MBWEMBWE KUWA KATIBU MKUU WAKE NA LICHAMA LAKE, IKULU YAKE IMESHIRIK KUMPA KICHAPO DR ULI.., IKULU YAKE IMESHIRIK KT DILI YA KIFISAD YA RICHMOND, NA MENGINE MENGI, JAMANI IMETOSHA TNAAIBIKA KWA MAJIRANi
 
Atatengua wangapi wakati wote wameoza! JK ndio aanze kwanza kujitengua mwenyewe kutokana na kuwa DHAIFU.
 
for sure hana intergrity ya kuendelea kushikilia wadhifa wa uwaziri,ni kosa la jinai kabisa tena kupitia mikono yake
 
Mi nilidhani kitu gani kikubwa,chama cha mapinduzi ni kawaida kuvunja sheria na kuachwa huru ila wangekuwa CHADEMA basi tungekuwa tunahangaika kushughulikia dhamana.Vipi kuhusu katibu mkuu Mhe.Kinana kampuni yake ilisafirisha meno ya tembo ampige chini? Lowassa alijiuzulu kwa kashfa ya ufisadi ampige chini uanachama wa ccm? Andrew Chenge alihusika na ununuzi wa radar mbovu na kuhatarisha usalama wa nchi,ampige chini? Nape Nnauye alituhumiwa kufoji cheti cha kuzaliwa ili agombee uvccm 2007 kitu ambacho ni kinyume cha sheria,je ampige chini? Prof.Sospeter Muhongo alilidanganya bunge kuhusu tenda na ununuzi wa vifaa TANESCO,je ampige chini? Waziri wa elimu Mhe.Mulugo alidhalilisha taifa kwa kushindwa kusema Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar kisha alisingizia tongue slip,je ampige chini kwa kuwa siyo mfano wa kuigwa kwa wanafunzi? Rais JK ameunda cabinet mara 4 kwa miaka 7,na kudhihirisha ana udhaifu katika uteuzi,ajipige chini? ccm ni mahututi!
 
ushauri wako ni finyu na duni baada ya kumshauri avunje serikali yote wewe umemwona kagashek wivu tu. Ukimtoa mwakyembe magufuli na sita nani msafi?
 
Uteuzi wa viongozi wetu Tanzania hauji hivi hvi ni who knows who kuna mlolongo mrefu kwa ufupi mambo yako hivi.
mzee Mwinyi alipoteuliwa kuwa balozi wetu nchini Misri aliachiwa ubalozi na balozi Kagasheki mkubwa, stori haikushia hapo,baadae mtoto wa mzee Mwinyi ambae ni waziri wa Afya akaoa kwa kina Kagasheki.
Mpaka hapo jiulize nani aliye mgroom Jakaya from the scratch its none other than mzee ruksa,kama mkulu alivyotupasha za kuambiwa na wewe ........................
Therefore it goes without saying that your request will definetly fall in a deaf ear.
 
Utakuwa umebwia ugolo...... unamfundisha JK.!! Asikiagi tangu dogo msoga.
 
tuna safari ndefu mbele kuhusu kuwajibishana au kuwajibika ila hakuna MAREFU YASIYOKUWA NA NCHA.
 
Mtu anayekuza rushwa nchini..jk, atengue u-waziri wa mshikaji,
ccm kuwa madarakani ni maajabu ya dunia.
Upole wa watanzania unakera.....,piga chini mzigo.
 
Slaa si ndio Rais wenu mbona una mwomba Kikwete mnashida sana nyie
 
Back
Top Bottom