Rais Kikwete ziarani Marekani na Canada - Oktoba 01, 2012

KLKUNA WATU AMABAO WATAULIZWA PESA ZA MAFISADI LAKINI MH WANGU LAZIMA MUNGU AMUULIZE HIZI SAFARI AMETOA PESA WAPI JAMANI KABISA KABISA .....KAMA NDIO CHAGUO LA MUNGU MUNGU AHIMIDIWE KWA SAFARI HIZI
Kikwete-file-picture1.jpg
 
Kama alihutubia aliongelea Daudi Mwangosi, kama hakumuongelea basi hakuhutubia maana nachijua mie hutuba ya mwisho wa mwezi lazima ibebe matukio mhimu ya mwezi huo na solution zake na sio blabla
 
nadhani sio yeye peke yake ambae yuko newyork kwa sasa,ukitazama utaona kwamba hata AHMEDNEJAD nae yuko huku licha ya kuwa nchi yake na marekani ziko katika hali ya sintofahamu,lakini pia mbowe na sugu walikua huko hivi majuzi na safari yao tuliigharamia sisi tax payer,ndi gharama za demokrasia,hatuna jinsi wazungu wametuletea demokrasia lakini lazima tuigharamie
 
Mkuu huko nchi gani? Mbona alitoa jana hotuba?

Jamani huyu jamaa ni utaratibu wake kulihutubia taifa kila mwezi ao anafanya anvyopenda yeye
tulitaka kusikia kasi mpya,ari mpya na nguvu mpya inaendeleaje.
 
Hapana mkuu ni matumizi ya safari ndio nayaonea wivu kulinganisha na wale wenzetu loliondo wanaokufa na njaa shukuru mungu baba yako aliwahi umande mkuu ukazaliwa dar es salaam ..wenzio wanataabikandio tunajaribu kuwaondolea umande kwa wahusika kuwapa msaada hata wa chakula tu
 
mnamuonea wivu!

Acha siasa za Wasira wewe jibu issue hiyo sasa anaonewa kwa lipi wakati anatumia kodi za wanyonge kwa saafari ambazo hazina tija.Ama kweli ukitaka kushabikia CCm na Kikwete wao lazima uwe na akili ya maiti.Si mmeona waliimba wee lazima mapacha 3 Edward Lowasa,Andrew Chenge na Rostam Azizi wajivue gamba lakini cha kushangaza leo hii mapacha wale wamekuwa watu wasafi sijui huyu aliyeanzisha Vua gamba yu wapi au ndio kalala ajabu hii
 
nadhani sio yeye peke yake ambae yuko newyork kwa sasa,ukitazama utaona kwamba hata AHMEDNEJAD nae yuko huku licha ya kuwa nchi yake na marekani ziko katika hali ya sintofahamu,lakini pia mbowe na sugu walikua huko hivi majuzi na safari yao tuliigharamia sisi tax payer,ndi gharama za demokrasia,hatuna jinsi wazungu wametuletea demokrasia lakini lazima tuigharamie

Muwe mnaona aibu ingawa wanasema nyie waswahili hamna aibu; unapomfananisha Rais wa Iran na Vasco Dagama, je unajua mara ngapi kwa mwaka huyu bwana anakwenda marekani? Rais wa Iran huenda mara moija kwa mwaka kwenye mkutano wa U.N. wakati Vasco Dagama yeye hata mikutano ambayo angeweza kuwakilishwa mradi ni mareakani ataacha kila shuhuli na kukwea pipa!!! Jamaa haoni aibu asilani kazi kutembeza bakuli halafu fedha wanaficha Uswisi!!
 
Kama wapiga kura mmeridhika na trip zake ataendelea kuzurula tu
 
Muwe mnaona aibu ingawa wanasema nyie waswahili hamna aibu; unapomfananisha Rais wa Iran na Vasco Dagama, je unajua mara ngapi kwa mwaka huyu bwana anakwenda marekani? Rais wa Iran huenda mara moija kwa mwaka kwenye mkutano wa U.N. wakati Vasco Dagama yeye hata mikutano ambayo angeweza kuwakilishwa mradi ni mareakani ataacha kila shuhuli na kukwea pipa!!! Jamaa haoni aibu asilani kazi kutembeza bakuli halafu fedha wanaficha Uswisi!!
Ala, huyo atakayemwakilisha atakwenda kwa miguu, hatalipwa per diem na hatatumia fedha za walipa kodi? Hivi issue ilikuwa matumizi ya fedha au mkuu kusafiri kila mara? . Mwacheni rais atumie nafasi yake kama rais. Nawe siku ukiwa rais usisahau kutumia nafasi yako kama rais.
 
Kama kawaida, kutembeza bakuli kumeanza. Infact ni aghalabu kusikiliza speech yake bila neno msaada ndani yake. Mpaka sasa hajajua madhara ya misaada ya wazungu anayoona fahari kuitaja. For a perfect man kuzungumzia kuomba misaada ni aibu kubwa... Hasa kama huna sababu za msingi za kuomba hiyo misaada!
 
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anaanza Ziara ya Kikazi ya Marekani na Ziara Rasmi ya Kiserikali ya Canada akianzia mjini New York, Marekani leo, Jumatatu, Oktoba Mosi, 2012.

Rais Kikwete na ujumbe wake uliondoka nchini usiku wa jana, Jumapili, Septemba 30, 2012, na utawasili mjini New York, Marekani mchana wa leo tayari kwa ziara hiyo ya Marekani.

Rais Kikwete atakuwa Marekani kwa siku mbili kabla ya kwenda Canada kwa ziara Rasmi ya Kiserikali ya siku mbili.
Katika ziara yake mjini New York, Marekani, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Ban Ki Moon ofisini kwa Katibu Mkuu huyo kesho asubuhi Oktoba 2, 2012.

Baada ya mazungumzo hayo, Rais Kikwete ataungana na Mheshimiwa Ban Ki Moon, Meya wa Jiji la New York na Mfadhili Mkubwa wa Misaada ya Kibinadamu Duniani, Mheshimiwa Michael Bloomberg; Mama Helen Agerup ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Misaada ya Kibinadamu ya H&B Agerup na Dkt. Kelly J. Henning, Mkurugenzi wa Mipango ya Sekta ya Afya ya Taasisi ya Bloomberg Philanthropies kwenye Uzinduzi wa Matokeo ya Mpango ya Ubunifu wa Afya ya Akinamama katika Tanzania.

Kwenye sherehe hiyo iliyopangwa kufanyika kwenye ukumbi uitwao Green Room kwenye makao makuu wa Umoja wa Mataifa, Rais Kikwete, Mheshimiwa Ban Ki Moon, Meya Bloomberg na mama Helen Agerup kwa pamoja watazindua Matokeo ya Mpango huu uitwao Innovative Maternal Health Program.

Kwenye shughuli hiyo pia Meya Bloomberg atatangaza matokeo ya miaka mitatu ya misaada ya kiafya chini ya mpango huo kwa akinamama iliyotolewa na taasisi ya inayomilikiwa na Meya Bloomberg ya Bloomberg Philanthropies.
Aidha, kwenye shughuli hiyo, Meya Bloomberg atatangaza misaada mpya wa mabilioni ya fedha kuboresha afya ya akinamama katika Tanzania chini ya mpango huo na atatangaza mshirika mpya ambaye atasaidiana na taasisi ya Bloomberg Philanthropies katika kuunga mkono huduma bora za afya kwa akinamama wa Tanzania.

Katika Tanzania, misaada ya taasisi ya Bloomberg Philanthropies huelekezwa katika maeneo ya vijijini yasiyokuwa na huduma bora zaidi kwa kiafya na huduma ambazo hutolewa ni zile za kuokoa maisha ya akina mama hasa wakati wa uzazi.

Tokea mwaka 2006, taasisi hiyo imetoa kiasi cha dola za Marekani milioni 11.5 Fedha hizo ni sehemu ya kiasi cha dola za Marekani milioni 330 ambazo zilitolewa na taasisi hiyo kwa nchi mbali mbali duniani kwa mwaka jana peke yake.

Taasisi hiyo hufanya kazi ya kuendeleza maeneo matano duniani ambayo ni Usanii, Elimu, Mazingira, Ubunifu katika Serikali na Afya ya Umma.
Rais Kikwete ataondoka Marekani kwenda Canada keshokutwa Jumatano Oktoba 3, 2012 kwa ajili ya Ziara Rasmi ya Kiserikali ya siku mbili katika nchi hiyo kwa mwaliko wa Gavana Jenerali wa nchi hiyo, Mheshimiwa David Johnston.

Imetolewa na
:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
1 Oktoba, 2012

Sema ana hamu na mkewe. Si alitangulia na akina Membe!!!!!!!!!!!!

Vile vile wakuu. Ingekuwa vyema katiba mpya ikaweka wazi ukomo wa siku za raisi kuwa nje ya ofisi ( mobile ofice). Maana huyu jamaa nadhani kala miguu ya kuku.
 
Na posho anapata sawa na wajumbe wengine hata kama watapewa 6,000 USD na yeye anachukua wakati pale wamekwenda kama mke na mume hivyo baadhi ya cost nilitegemea kwa upande wake kuwa chini kama ya malazi, inaelekea retirement zao hazifanyiki kwa receipt inasainiwa ela yote kama allowance.
 
Sema ana hamu na mkewe. Si alitangulia na akina Membe!!!!!!!!!!!!

Vile vile wakuu. Ingekuwa vyema katiba mpya ikaweka wazi ukomo wa siku za raisi kuwa nje ya ofisi ( mobile ofice). Maana huyu jamaa nadhani kala miguu ya kuku.

Mimi nilikuwa nimeshangaa Mhe Dkt Dkt Dkt JK 'kususia' kikao cha UN General Assembly amtume Membe kumwakilisha, yaani akose kwenda Marekani? Ilikuwa karibu nifungue uzi wa kumpongeza kwamba ameanza kufanya kama Baba wa Taifa Hayati JKN alivyokuwa akifanya. JKN alikuwa anawatuma akina Sam Malecela kuwakilisha Tanzania katika vikao vya UN. Kumbe inaelekea alilazimishwa na vikao vya CCM kubaki na hivyo akili yake yote wakati wa vikao ilikuwa nyyuyoko!! aahhhh, aahhh,:biggrin:
 
Wadau mnakumbuka ule wimbo wa msanii wa kenya unaimbwa..
Bwana nipe pesa,watoto wana njaa,
huyu kiongozi wangu amezoea kutangatanga,hata majirani wamechoka kumuoa huku wakisema fungeni milango anakujaaaa!
 
Wadau mnakumbuka ule wimbo wa msanii wa kenya unaimbwa..
Bwana nipe pesa,watoto wana njaa,
huyu kiongozi wangu amezoea kutangatanga,hata majirani wamechoka kumuoa huku wakisema fungeni milango anakujaaaa!

Ndo ivo ujue ulimchagua ili aweze kutimiza ndoto zake za kusafiri
 
Ahsante kwa taarifa mkuu,

Mkuu anakwenda mara kwa mara, ingawa kuna wawakilishi .. leo hii amekwenda wiki ijayo amerudi, wiki itayofuata ataondoka and the week after anarudi, na ile wiki(mwezi sasa) atarudi KULE KULE...sasa hivii ni kwa nini Rais wetu asikae huko huko hadi amalize "mikutano/ziara n.k" YOTE ndio arudi?

Kuna uwezekano tuakajenga IKULU NDOGO Marekani?
 
Back
Top Bottom