Rais Kikwete ziarani Marekani na Canada - Oktoba 01, 2012

kiswahili kipo ila wanafanya makusudi. fax=nukushi, email= baruapepe, website=tovuti. diroctorate=kurugenzi
 
kiswahili kipo ila wanafanya makusudi. fax=nukushi, email= baruapepe, website=tovuti. diroctorate=kurugenzi

Hawafanyi makusudi mzee hawajui kigezo cha kupewa hiyo kazi ni uswahiba so hata ukiwa kilaza utapewa tu ili mradi wewe ni swahiba wa J mzururaji
 
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anaanza Ziara ya Kikazi ya Marekani na Ziara Rasmi ya Kiserikali ya Canada akianzia mjini New York, Marekani leo, Jumatatu, Oktoba Mosi, 2012.

Rais Kikwete na ujumbe wake uliondoka nchini usiku wa jana, Jumapili, Septemba 30, 2012, na utawasili mjini New York, Marekani mchana wa leo tayari kwa ziara hiyo ya Marekani.

Rais Kikwete atakuwa Marekani kwa siku mbili kabla ya kwenda Canada kwa ziara Rasmi ya Kiserikali ya siku mbili.
Katika ziara yake mjini New York, Marekani, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Ban Ki Moon ofisini kwa Katibu Mkuu huyo kesho asubuhi Oktoba 2, 2012.

Baada ya mazungumzo hayo, Rais Kikwete ataungana na Mheshimiwa Ban Ki Moon, Meya wa Jiji la New York na Mfadhili Mkubwa wa Misaada ya Kibinadamu Duniani, Mheshimiwa Michael Bloomberg; Mama Helen Agerup ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Misaada ya Kibinadamu ya H&B Agerup na Dkt. Kelly J. Henning, Mkurugenzi wa Mipango ya Sekta ya Afya ya Taasisi ya Bloomberg Philanthropies kwenye Uzinduzi wa Matokeo ya Mpango ya Ubunifu wa Afya ya Akinamama katika Tanzania.

Kwenye sherehe hiyo iliyopangwa kufanyika kwenye ukumbi uitwao Green Room kwenye makao makuu wa Umoja wa Mataifa, Rais Kikwete, Mheshimiwa Ban Ki Moon, Meya Bloomberg na mama Helen Agerup kwa pamoja watazindua Matokeo ya Mpango huu uitwao Innovative Maternal Health Program.

Kwenye shughuli hiyo pia Meya Bloomberg atatangaza matokeo ya miaka mitatu ya misaada ya kiafya chini ya mpango huo kwa akinamama iliyotolewa na taasisi ya inayomilikiwa na Meya Bloomberg ya Bloomberg Philanthropies.
Aidha, kwenye shughuli hiyo, Meya Bloomberg atatangaza misaada mpya wa mabilioni ya fedha kuboresha afya ya akinamama katika Tanzania chini ya mpango huo na atatangaza mshirika mpya ambaye atasaidiana na taasisi ya Bloomberg Philanthropies katika kuunga mkono huduma bora za afya kwa akinamama wa Tanzania.

Katika Tanzania, misaada ya taasisi ya Bloomberg Philanthropies huelekezwa katika maeneo ya vijijini yasiyokuwa na huduma bora zaidi kwa kiafya na huduma ambazo hutolewa ni zile za kuokoa maisha ya akina mama hasa wakati wa uzazi.

Tokea mwaka 2006, taasisi hiyo imetoa kiasi cha dola za Marekani milioni 11.5 Fedha hizo ni sehemu ya kiasi cha dola za Marekani milioni 330 ambazo zilitolewa na taasisi hiyo kwa nchi mbali mbali duniani kwa mwaka jana peke yake.

Taasisi hiyo hufanya kazi ya kuendeleza maeneo matano duniani ambayo ni Usanii, Elimu, Mazingira, Ubunifu katika Serikali na Afya ya Umma.
Rais Kikwete ataondoka Marekani kwenda Canada keshokutwa Jumatano Oktoba 3, 2012 kwa ajili ya Ziara Rasmi ya Kiserikali ya siku mbili katika nchi hiyo kwa mwaliko wa Gavana Jenerali wa nchi hiyo, Mheshimiwa David Johnston.

Imetolewa na
:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
1 Oktoba, 2012


HUYOOO AKIKIMBILIA PIPA AONDOKE BONGO HARAKA HARAKA...


ALeqM5iITr-XOC5QuQQc0QwmhUMRHTwRHg.jpg
 
Marekani kutakua kuzuri sana!!!! Ila hata hivyo hajamuuzia BUSH Kigamboni! Alikanusha hili kwa mdomo!!!
 
Marekeni anaenda kufanya nini wakati Waziri wake wa Mambo ya Nje yupo huko!!?

photo.JPG

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Mhe. Waziri Benard Membe, katika picha ya pamoja na Rais Obama na Mama Michele Obama wakati wa hafla ya Viongozi wa Nchi Wanachama za Umoja wa Mataifa iliyoandaliwa na Mhe. Rais Barack Obama jijini New York. Mhe. Waziri Membe yuko New York akiongoza ujumbe wa Tanzania akimuwakilisha Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Mgombea uraisi ajaye kwa tkt ya Nyinyiemu
 
Namuombea kwa Mwenyezi Mungu apate terrible accident na afe hapo hapo. Ni janga la taifa huyu JKilaza!

Hapana!!hapana mkuu wangu!hiyo ni mbaya sana!!japo tumemchoka lakini tusimwombee hayo,Heshimu uhai mkuu,mengine tutapambana nayo tu.
 
Safari zingine hata mkuu wa wilaya anaweza kutumwa sio kila kitu prezidaa kupunguza gharama maana ujumbe wake pamoja na wanausalama kibao,safari mmoja tu mabilioni duu tatafika kweli ,2015 mbali.........
 
"Taasisi hiyo hufanya kazi ya kuendeleza maeneo matano duniani ambayo ni Usanii, Elimu, Mazingira, Ubunifu katika Serikali na Afya ya Umma.Rais Kikwete ataondoka Marekani kwenda Canada keshokutwa Jumatano Oktoba 3, 2012 kwa ajili ya Ziara Rasmi ya Kiserikali ya siku mbili katika nchi hiyo kwa mwaliko wa Gavana Jenerali wa nchi hiyo, Mheshimiwa David Johnston."

Nimependa eneo la USANII
 
Hii kali. jamaa anapangilia kweli per diem zake na hivi mshahara siri yake du mwache rizi awe bilionea tu. Haya sawa safari njema mkuu.
 
Kama kawa vasco dagama is in controll.
Jana lipumba kwenye kale kamkutano kao ka ukoo alisema "huyu bwana(JK) tangu amechaguliwa amekua mtu wakujiandaa na safari tuu!! anataka kuvumbua kama Vasco dagama".
Safari njema JK, nyie ndo wala nchi bana sisi wananchi hali si hali kila pasi ni chali kama biti ya makochali.
Ila msalimie EMINEM the slim shady my favourate hip hop musician,
 
JK si angeeda yeye kwenye mkutano wa UN ili aunganishe hizo safari nyingine kuokoa gharama?Ama si angemwacha Membe aendelee na hizo shughuli huku baadhi ya hao alioenda nao kwenye mkutano warudi nyumbani?Hawa watu wanaudhi sana!
 
Anaenda kuonana na Ban Kimoon ambaye ameshaonana na Membe,ni hiyo misaada ya billions ndo imemkurupusha akaona aende mwenyewe.Itakuwa ni dili ambayo alikuwa hana taarifa nayo,labda Membe ndo kaambiwa na yeye kamshtua(baada ya ile statement ya bakuli) JK akaamuwa kukwea pia ili asikose dili,maana panga pangua wana 10 pasenti zao,hizo pesa haziendi zote kwa waliokusudiwa.Huo mkutano umeandaliwa na Ban Kimoon baada ya kuiona statement ya bakuli ya Membe na kuwashtua kina Bloomberg,wenzetu wamejipanga si kama vichwa nazi wetu!

Halafu ukiangalia behind the scenes,ni rasilimali ndizo zinatolewa kwa mlango wa nyuma,ndiyo maana hata statement ya Membe juzi inazungumzia bakuli tu,lakini kwa ninavyomjuwa Bloomberg and the likes,wao wako kibishara zaidi,na tayari behind the scenes kuna deals wamesaini,nahisi zitakuwa zile za gesi
 
Back
Top Bottom