Rais Kikwete ziarani Marekani na Canada - Oktoba 01, 2012 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete ziarani Marekani na Canada - Oktoba 01, 2012

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by n00b, Oct 1, 2012.

 1. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

  Telephone: 255-22-2114512, 2116898
  E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
  press@ikulu.go.tz
  Fax: 255-22-2113425  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anaanza Ziara ya Kikazi ya Marekani na Ziara Rasmi ya Kiserikali ya Canada akianzia mjini New York, Marekani leo, Jumatatu, Oktoba Mosi, 2012.

  Rais Kikwete na ujumbe wake uliondoka nchini usiku wa jana, Jumapili, Septemba 30, 2012, na utawasili mjini New York, Marekani mchana wa leo tayari kwa ziara hiyo ya Marekani.

  Rais Kikwete atakuwa Marekani kwa siku mbili kabla ya kwenda Canada kwa ziara Rasmi ya Kiserikali ya siku mbili.
  Katika ziara yake mjini New York, Marekani, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Ban Ki Moon ofisini kwa Katibu Mkuu huyo kesho asubuhi Oktoba 2, 2012.

  Baada ya mazungumzo hayo, Rais Kikwete ataungana na Mheshimiwa Ban Ki Moon, Meya wa Jiji la New York na Mfadhili Mkubwa wa Misaada ya Kibinadamu Duniani, Mheshimiwa Michael Bloomberg; Mama Helen Agerup ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Misaada ya Kibinadamu ya H&B Agerup na Dkt. Kelly J. Henning, Mkurugenzi wa Mipango ya Sekta ya Afya ya Taasisi ya Bloomberg Philanthropies kwenye Uzinduzi wa Matokeo ya Mpango ya Ubunifu wa Afya ya Akinamama katika Tanzania.

  Kwenye sherehe hiyo iliyopangwa kufanyika kwenye ukumbi uitwao Green Room kwenye makao makuu wa Umoja wa Mataifa, Rais Kikwete, Mheshimiwa Ban Ki Moon, Meya Bloomberg na mama Helen Agerup kwa pamoja watazindua Matokeo ya Mpango huu uitwao Innovative Maternal Health Program.

  Kwenye shughuli hiyo pia Meya Bloomberg atatangaza matokeo ya miaka mitatu ya misaada ya kiafya chini ya mpango huo kwa akinamama iliyotolewa na taasisi ya inayomilikiwa na Meya Bloomberg ya Bloomberg Philanthropies.
  Aidha, kwenye shughuli hiyo, Meya Bloomberg atatangaza misaada mpya wa mabilioni ya fedha kuboresha afya ya akinamama katika Tanzania chini ya mpango huo na atatangaza mshirika mpya ambaye atasaidiana na taasisi ya Bloomberg Philanthropies katika kuunga mkono huduma bora za afya kwa akinamama wa Tanzania.

  Katika Tanzania, misaada ya taasisi ya Bloomberg Philanthropies huelekezwa katika maeneo ya vijijini yasiyokuwa na huduma bora zaidi kwa kiafya na huduma ambazo hutolewa ni zile za kuokoa maisha ya akina mama hasa wakati wa uzazi.

  Tokea mwaka 2006, taasisi hiyo imetoa kiasi cha dola za Marekani milioni 11.5 Fedha hizo ni sehemu ya kiasi cha dola za Marekani milioni 330 ambazo zilitolewa na taasisi hiyo kwa nchi mbali mbali duniani kwa mwaka jana peke yake.

  Taasisi hiyo hufanya kazi ya kuendeleza maeneo matano duniani ambayo ni Usanii, Elimu, Mazingira, Ubunifu katika Serikali na Afya ya Umma.
  Rais Kikwete ataondoka Marekani kwenda Canada keshokutwa Jumatano Oktoba 3, 2012 kwa ajili ya Ziara Rasmi ya Kiserikali ya siku mbili katika nchi hiyo kwa mwaliko wa Gavana Jenerali wa nchi hiyo, Mheshimiwa David Johnston.

  Imetolewa na
  :
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu.
  Dar es Salaam.
  1 Oktoba, 2012
   
 2. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Ahsante kwa taarifa mkuu,

  Mkuu anakwenda mara kwa mara, ingawa kuna wawakilishi .. leo hii amekwenda wiki ijayo amerudi, wiki itayofuata ataondoka and the week after anarudi, na ile wiki(mwezi sasa) atarudi KULE KULE...sasa hivii ni kwa nini Rais wetu asikae huko huko hadi amalize "mikutano/ziara n.k" YOTE ndio arudi?
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Safari moja huanzisha nyingine.
   
 4. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,170
  Likes Received: 1,173
  Trophy Points: 280
  Ya mia sita na ngapi hiyo?
   
 5. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mhhh haya asanteni kwa taarifa
   
 6. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,321
  Likes Received: 10,400
  Trophy Points: 280
  Ahsante kwa taarifa
   
 7. m

  mamanalia JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 671
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
 8. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,087
  Likes Received: 1,731
  Trophy Points: 280
  Inasikitisha!
   
 9. R

  Ruppy karenston JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Owkay.
   
 10. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,728
  Likes Received: 12,797
  Trophy Points: 280
  Hahahaha
  safari ni safari
   
 11. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #11
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  My god, Hivi Tanzania tutakuja kweli kupata Raisi mwingine wa aina hii, Ina sikitisha sana, na kuna kitu gani huko Marekani? Kwa nini sio Nchi kama

  1. INDIA, INDONESIA, MALAYASIA, NA KAZALIKA? Make hizi nchi ndo kidogo zinaweza kutufaa,
   
 12. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #12
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

  Telephone: 255-22-2114512, 2116898
  E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
  press@ikulu.go.tz
  Fax: 255-22-2113425


  Hii kitu hii kwani hakuna kiswahili chake
  hakuna kiswahili cha email au fax au website au hiyo Directorate
   
 13. M

  Moony JF-Expert Member

  #13
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  safari njema
   
 14. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #14
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  wanajitahidi kweli kuipamba ionekane ni shughuli muhimu kwa rais kusafiri, lakini kwa mtizamo wangu baloz majar paleNew york au Kalaghe angweza kufanya shughuli hii jamani, naona mkubwa alikuwa hajasafiri muda kidogo kaamua kutoka ukizingatia muda unayoyoma. Rweyemamu nae kaandika sana kwa kuwa kishakamata Perdiem ya siku kumi ulaya sio mchezo bana, njaaa hizi. Tanzania njaa haina mdogo wala mkubwa, Kiongozi au asiye kiongozi, haina jinsia na wala haina chama, its a rotten system.
   
 15. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #15
  Oct 1, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Ujumbe wake yumo pia mkewe?
   
 16. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #16
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Hiyo KURUGENZI imekosa kazi hii si taarifa ni utaratibu uliozoeleka kwa huyo bwana kuongoza nchi kwa safari za nje kutoa taarifa ni sawa MUME kuutangazia UMA anataka kuzaa ma MKEWE.
   
 17. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Marekeni anaenda kufanya nini wakati Waziri wake wa Mambo ya Nje yupo huko!!?

  [​IMG]
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Mhe. Waziri Benard Membe, katika picha ya pamoja na Rais Obama na Mama Michele Obama wakati wa hafla ya Viongozi wa Nchi Wanachama za Umoja wa Mataifa iliyoandaliwa na Mhe. Rais Barack Obama jijini New York. Mhe. Waziri Membe yuko New York akiongoza ujumbe wa Tanzania akimuwakilisha Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
   
 18. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #18
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  Ziara hii ni ya KUOMBAOMBA zaidi kuliko KIUWEKEZAJI
   
 19. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #19
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hawana MCC hao!
   
 20. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #20
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mbona hakuna bendera ya Tanzania hapo! Picha imechakachuliwa!
   
Loading...