Rais Kikwete, wanaovuruga nchi yetu ni wanasiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete, wanaovuruga nchi yetu ni wanasiasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Oct 18, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  Na Julius Samwel Magodi
  Wiki iliyopita katika safu hii niliangalia haki ya wananchi kujua afya ya Rais Jakaya Kikwete na nikajadili kama rais ana wasaidizi kwa nini kila mahali aende yeye.

  Pia nilijadili taarifa ya madaktari wake ambao wametuhakikishia kuwa rais hataanguka tena kwa sababu watampangia ratiba isiyomchosha.

  Nilitahadharisha kuwa kama taarifa yao hiyo wameipaka mafuta ya kisiasa, basi huenda ahadi yao kuwa hataanguka tena ikawaweka katika kitanzi, kwani Watanzania hawatakubali kuona wanapewa taarifa ambazo sio sahihi.

  Leo ningependa kujadili hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati akihutubia taifa katika kilele cha sherehe za kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo cha Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere.

  Moja ya jambo muhimu ambalo aliligusia katika hotuba hiyo, ni kukemea watu wanaohatarisha kubomoa misingi ya utaifa na umoja wetu nchini ambao ndio lulu yetu tuliyoachiwa na mwasisi wetu huyu wa taifa.

  Rais Kikwete alikwenda mbali zaidi katika kuwasihi Watanzania waichezee lulu hiyo karibu na tundu la choo kwani ikitumbikia hatuwezi tena kuipata aslani.

  Aliwataka wananchi wasidanganywe na viongozi wa kisiasa, au dini wanaotaka kutuingiza katika vitendo vinavyoweza kuvuruga umoja wetu kwa misingi ya dini, ukabila ama rangi.

  Pia alivitaka vyombo kuacha kuripoti habari za viongozi wachochezi na kwamba, nchini Rwanda mauaji yale makubwa yalichochewa na kuongozwa na redio moja ya Millie Collines (RTLM).

  Kwa hakika kauli hii ya Rais Kikwete ni nzuri kutolewa sasa ili kulinda umoja na utaifa wetu.

  Hakuna mtu ambaye anataka umoja wetu tuliozoea kuwa nao leo upotee, haiwezi kuingia akilini katika zama hizi turudi nyuma eti ili uweze kupata kazi lazima uangaliwe rangi yako, kabila lako au dini yako. Huko tulishapita zamani mno.

  Lakini nani anataka kuturudisha huko, ni wananchi wa walalahoi au wanasiasa? Ni wazi kuwa ni viongozi wetu wa kisiasa. Kuporomoka kwa maadili ya viongozi wa kisiasa ndiko ambako kunataka kuhatarisha umoja wetu, Rais Kikwete asitafute mchawi.

  Mchawi ni viongozi wetu wametufikisha hapa tulipo, wala lawama hizo hawawezi kuzikwepa hata kidogo, wao ndio wanaotaka kutufikisha huko.

  Kwa mfano hivi karibuni suala la serikali kujiunga na OIC liligeuzwa na wabunge kuwa la udini badala ya kujadiliwa kwa maslahi ya taifa zaidi.

  Ingawa suala hili lilikuwapo miaka mingi, safari hili lilikuja likiwa limebeba udini zaidi kila mbunge alichangia kulingana na dini yake. Wapo wabunge walidiriki hata kufikia kutoa nyongo zilizomo mwilini mwao kuhusu jambo hilo kwa kusema wazi wazi kwamba, wafuasi wa dini yao wamekuwa wakibaguliwa na kutengwa na serikali.

  Watanzania siku zote tulizoea ukisema ukabila ilikuwa ni utani, mtu akimuuliza mwenzake kabila anataka kuona kama ni mtani wake amtanie, lakini siku hizi viongozi wetu wamekuwa wakishabikia udini, ukanda na hata tumeshuhudia wakidiriki hata kujipendelea kupeleka miradi ya barabara katika maeneo wanayotoka.

  Kama waziri anaweza kuamua kupendelea eneo au kanda anayotoka anapandikiza mbegu gani kwa wananchi sio ya ubaguzi hiyo? Ni wazi hapo anaotesha mgawanyiko katika taifa.

  Jambo jingine ambalo linaongeza chuki ya ubaguzi nchini, ni pengo kati ya matajiri na maskini ambalo sasa ni kubwa, kiasi sasa maskini hawezi kuota kufikia katika ufalme wanaoishi viongozi wetu waliojilimbikizia mali. Sasa hivi serikali inaongozwa na matajiri wachache huku masikini ambao ni wengi wakiachwa hawana sauti.

  Katika mazingira niambie utakuwepo umoja hapo? Upendo na umoja utatoka wapi wakati wananchi wanashuhudia viongozi wao wakigawana mali za umma kupitia wimbo wa uwekezaji, kumbe wanawawekeza wananchi ambao wamebaki watazamaji tu?

  Huko nyuma hawa wananchi wa kawaida walikuwa na sauti katika kuendesha nchi, serikali sasa imekumbatiwa na matajiri kuliko watu wa kawaida. Umoja hapa upo wapi na nani anasababisha hali hii?

  Matokeo yake sasa wananchi wamekosa uvumilivu wameamua kutumia nguvu ya umma katika kudai haki zao. Sasa Tunashuhudia wananchi katika maeneo mbalimbali nchini wakichukua sheria mkononi kwa kuandamana na pengine kuamua kuweka kizuizi, ili Rais Kikwete asipite barabara fulani. Hii ni hatari sana kwa ustawi wa taifa letu.

  Hata hilo la vyombo vya habari kwamba ndivyo vilivyosababisha mauaji Rwanda, ninachoweza kusema ni kwamba mauaji ya halaiki ya Rwanda yalichochewa zaidi na viongozi wa kisiasa.

  Kama haingekuwa tamaa ya wanasiasa wa nchi hiyo kutaka madaraka, leo hakuna chombo cha habari ambacho kingeshabikia mauaji hayo. Watakaoibomoa nchi hii ni wanasiasa sio mtu mwingine.

  Viongozi wa dini wanaingilia kati pale ambapo serikali inapoonyesha kwamba, imekwama kutekeleza majukumu yake. Viongozi wa dini ni walinzi wa amani na wanapoona inataka kutoweka wanakemea.
  http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=15387
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  wanasiasa anaowasema na yeye akiwemo au sio hivyo
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,403
  Likes Received: 81,428
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa anakimbia kivuli chake. Kwanini tu asitamke anayeivuruga Tanzania ni Kikwete na uongozi wake dhaifu na mbovu. Sasa hao wanasiasa wanaoivuruga Tanzania kwanini asiwataje na kuwachukulia hatua zinazostahili ili wasiendelee kuivuruga Tanzania. Tutaona vioja vingi vya huyu jamaa katika jitihada zake za kurudi Ikulu 2010. Anataka kuwalaumu wengine wote lakini yeye mwenyewe hana tatizo lolote lile katika uongozi wake. Ukistaajabu ya Mussa...
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Oct 18, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,563
  Likes Received: 3,858
  Trophy Points: 280
  Waandishi wengine na title zao, yaani title kama vile in m-exclude JK. Mwandishi hawezi kusema moja kwa moja JK wewe ndiye unavuruga nchi

  Hii tabia ndiyo ya wapinzani wetu 'wapiganaji CCM' , wachungaji, maprofesa vyuoni, eti kumsema jk wanamzunguka!
   
 5. M

  Manundu Member

  #5
  Oct 18, 2009
  Joined: Apr 7, 2008
  Messages: 89
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Hizo kauli tata tulishazizoea, tulishaambiwa suala la mgawo wa umeme litabaki kuwa historia,je historia au ...........
   
Loading...