Rais Kikwete umechakachua NISHANI .... Bi kidude ni Mzanzibar

VIKWAZO

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
1,899
580
Salamu wandugu

Kwanza naomba nianze kwa kuweka kumbukumbu sahihi, Mimi ni Mtanganyika mwenye HESHIMA na Utanzania.
Lakini pia nimechoka na huu uzekezaji unaofanywa zidi wa wazanzibar

Siku ya UHURU wa TANGANYIKA Raisi Kikwete alitoa NISHANI mbalimbali hapa kuna matatizo (uchakachuaji wa aina mbili)

1. Uhuru ni Tanganyika lakini nishani zilitoka za Tanzania, sasa nashindwa ilikuwa ni siku ya UHURU wa Tanzania? na kama ndivyo na siku ya MUUNGANO tutatoa nishani zipi? nishani za Tanzania siku ya Tanganyika ni kuwatisha wazanzibar kwamba Tanganyika ndio Tanzania, hii sio sahihi ni uchakachuaji.

2. Bi Kidude kwenye nishani za TANGANYIKA anahusika vipi? ni nani asiyejua kwamba Bi Kidude ni Zanzibar?!!! tunawaogopa nini hawa wazanzibar mpaka siku ya UHURU wetu wa TANGANYIKA tujikombe na kuwanishani? vitu kama hivi ni uchakachuaji, lakini pia vinawapa kiburi wazanzibar, matokeo yake wanajisahahu kama walivyo sasa.

Mwisho ni kwa Watanganyika, tuwe macho, mambo kama haya yakitokeo VISIWANI wangepiga kelele na kusema wamedharauliwa, kwa upande wangu hii sio dharau lakini kama tunajikomba sana kwa wazanzibar mpaka kuwapa NISHANI za watanganyika

UPADATE
Nimebadilisha kichwa cha habari kidogo ili kuongeza maana
 
Hapo ndo mkanganyiko mkubwa ulipo.

huu mkanganyiko lazima uondoke, atuwezi kuisha mazingira machafu kiasi hiki,
Tuna sherehe ya Muungano na tahere zinajulikana, kisha tuna Tanganyika, kama kuna watu
wanaona kusema 9/12/1961 wa TANGANYIKA basi sherehe yenyewe iondolewe,
Nini maana ya kufanya sherehe ya kitu tunachokiogopa, tunafikia hatua tunachanganya hata majina ya nishani
 
CCM wana vichaa, wamewalea wazenj hadi hawajui tena nini si haki yao na nin ni haki yao.

Tunako elekea ni kubwa, KOSA la sisi kuitwa TANGANYIKA ni lipi? kwa nini tunapenda kushirikisha wazanzibar kwenye mambo ya TANGANYIKA na kila siku tunatukana MUUNGANO?
tuna haja jani ya kuwa na sherehe hiy TANGANYIKA?
 
...sherehe nzima ni maigizo mtupu...haya maigizo yamekuwa yakichoma fedha zetu kila mwaka bila sababu ya msingi...

Yes, Kama tunaogopa utanganyika tufute hiyo sherehe, tuwe na ile ya MUUNGANO na ya ZANZIBAR, maana naona hata NISHANI zimechakachuliwa na kuwa NISHANI za TANZANIA siku ya UHURU wa TANGANYIKA, hii ni potosha HISTORIA, atuwezi kujifanya TANGANYIKA imefufa wakati kuna shehere za UHURU wake kila mwaka.
 
Niliposikia nikaona kujipendekeza kwa kitu kisichofaa hata,hakuna watu kwenye fani ya sanaa waliosaidia kujenga Tanganyika?hadi urukie Zanzibar?itakuja siku mtu wa Bara atapewa nishani na rais wa zbar?itatokea kweli?kama kutokea alitakiwa Marehemu Adam Mwakanjuki,sidhani mwingine!Kwa nini yule Bi Kidude?au inaruhusiwa kupewa mtu yeyote?kutoka popote?
 
Salamu wandugu

Kwanza naomba nianze kwa kuweka kumbukumbu sahihi, Mimi ni Mtanganyika mwenye HESHIMA na Utanzania.
Lakini pia nimechoka na huu uzekezaji unaofanywa zidi wa wazanzibar

Siku ya UHURU wa TANGANYIKA Raisi Kikwete alitoa NISHANI mbalimbali hapa kuna matatizo (uchakachuaji wa aina mbili)

1. Uhuru ni Tanganyika lakini nishani zilitoka za Tanzania, sasa nashindwa ilikuwa ni siku ya UHURU wa Tanzania? na kama ndivyo na siku ya MUUNGANO tutatoa nishani zipi? nishani za Tanzania siku ya Tanganyika ni kuwatisha wazanzibar kwamba Tanganyika ndio Tanzania, hii sio sahihi ni uchakachuaji.

2. Bi Kidude kwenye nishani za TANGANYIKA anahusika vipi? ni nani asiyejua kwamba Bi Kidude ni Zanzibar?!!! tunawaogopa nini hawa wazanzibar mpaka siku ya UHURU wetu wa TANGANYIKA tujikombe na kuwanishani? vitu kama hivi ni uchakachuaji, lakini pia vinawapa kiburi wazanzibar, matokeo yake wanajisahahu kama walivyo sasa.

Mwisho ni kwa Watanganyika, tuwe macho, mambo kama haya yakitokeo VISIWANI wangepiga kelele na kusema wamedharauliwa, kwa upande wangu hii sio dharau lakini kama tunajikomba sana kwa wazanzibar mpaka kuwapa NISHANI za watanganyika
Mkuu, umesahau kwamba kimsingi hakuna tena taifa linaloitwa Tanganyika hapa duniani, labda kama tutaifufua tena. Na ndio maana hata katika michuano ya Challenge kule Uganda hakukuwa na taifa liitwalo kwa jina hilo. Muungano tulionao uliiua Tanganyika kabisa na pia Uliiacha Zanzibar hai lakini kwa kuhakikisha umeing'oa meno yote. Sasa Muungano tulio nao ni wa nchi mbili: moja imeuawa na ni marehemu na nyingine imeng'olewa meno yote kwa hiyo haina nguvu yake inayojitegemea. Sasa katika hali kama hii usitegemee kwamba kuna Utanganyika.
 
Kikwete ni kama yupo gizani, hajui anamtumikia nani!

Wapo hapa jamvini vilaza wake Nape Moses Nnauye na William J. Malecela wanajifanya watetezi wa serikali ya kikwete na wapo tayari kukifia chama ilimradi tu wahakikishiwe matumbo yao kujaa,

Hapa mimi nitaelekeza lawama kwa TISS hasa wakuu wa kitengo cha itifaki kwa rais.

Naamini leo rais akibanwa swali hilo atasema "ni upepo tu utapita"
 
Ina maana mkuu wa nchi kila siku tukiadhimisha kumbukumbu za uhuru lazima atoe nishani? Du kama ni za dhahabu naona itabidi tufungue mgodi mpya
 
Wachaa tu iko siku marehemu Tanganyika atafufuka na kuwahoji wanaomdhalilisha.

Pbr778AByzwwAQXbPDBCCes8MIMN+zwwxBHLPHEFOe75MUYZ6zxxhx37PHHIIcs8sgkl2zyySinrPLKLLfs8sswxyzzzDTXbDOOAuTHn1w67+zzz0AHLfTQRBdt9NFIJ6300kw37fTTUEct9dRUV2311VhnTV7PWnft9ddghy322GSXbfbZaKet9tpst+3223DHLffcdNftmd1456333nz3I+3334AHLvjghBdu+OGIJ6744ow37vjjkEcu+eSUV255RQE1ADs=
 
Yes, Ni uchakachuaji tu, kwenda mbele!!! link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...rehekea-uhuru-wa-nchi-ipi-14.html#post5195595

link 2 https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/364633-seif-tumekusikia%3B-sasa-jiuzulu-na-iondoe-cuf-kwenye-suk-10.html#post5190018

link 3. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...u-na-iondoe-cuf-kwenye-suk-6.html#post5180582

link 4. Huyu ndugu hapa ndio amekubali yaishe, ameshachakachuliwa kichwani (samahani ndugu DSN) wanatusomesha historia iliyochakachuliwa sio kosa lako. link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...u-na-iondoe-cuf-kwenye-suk-6.html#post5181372

Kuna mtu zinasema hata muungano ukivunjika basi tubakishe Tanzania kama mbadala wa jina Tanganyika.

Pia unakutana na kitu kama hii"miaka 51 ya uhuru wa Tanzania bara" link VIJIMAMBO: WATANZANIA WASHEREHEKEA MIAKA 50 YA UHURU UGIRIKI

link WATANZANIA WASHEREHEKEA MIAKA 50 YA UHURU UGIRIKI - Global Publishers
 
Au walikuwa wamekusudia kumpa Bi Kidude Nishani kwenye sherehe za Muungano maana sielewi uhusiano wa wake (Bi Kidude) na uhuru wa Tanganyika?
 
Tanganyika ni jina tulilopachikwa na Wakoloni wa Kiingereza, mimi huwa silipendi. Lina maana ya Tanga na Nyika. Yaani ukiacha Tanga (kwa Wasambaa) sehemu iliyobaki iliitwa nyika(ni) hadi huku kwetu. Kabla ya hapo wakoloni wa Kijerumani waliita nchi yetu Deusch Ostaafrica. Jina la Tanzania tulilibuni wenyewe na kulifuta kabisa (kulikana) hilo jina la kipuuzi alilotupa mkoloni, mwaka 1964. Ni jina tu tulilolipenda hivyo hata Muungano wetu na visiwa vya Pemba na Zanziba ukifa sisi tutabaki na jina letu la Tanzania wala hatutarudisha hilo jina la nyikani (kwa masokwe). Sana sana tunaweza kurudisha la Ostaafrica (e.g. Nyerere Ostaafrica).
Waulize wa CRDB Bank, hilo jina CRDB walilipataje, kirefu chake nini wakati original CRDB ilishakufa! Jamani jina ni jina tu, unajiita ambavyo roho yako inapenda. Tunalazimika tu kuheshimu mipaka tuliyoundiwa na wakoloni lakini si majina waliyotuita. Zambia ilikuwa North Rhodesia, Zimbabwe ilikuwa North Rhodesia, Malawi ilikuwa Nyasaland, Tanzania ilikuwa Tanga-Nyika n.k.
 
Niliposikia nikaona kujipendekeza kwa kitu kisichofaa hata,hakuna watu kwenye fani ya sanaa waliosaidia kujenga Tanganyika?hadi urukie Zanzibar?itakuja siku mtu wa Bara atapewa nishani na rais wa zbar?itatokea kweli?kama kutokea alitakiwa Marehemu Adam Mwakanjuki,sidhani mwingine!Kwa nini yule Bi Kidude?au inaruhusiwa kupewa mtu yeyote?kutoka popote?

Kimsingi hata tuzo/nishani zenyewe zilitakiwa kuitwa NISHANI ZA TANGANYIKA, hakuna kwenye kumbukumbu kwamba TANZANIA ilizaliwa 09/12, hiyo ni siku ya TANGANYIKA na iheshimike hivyo
 
Dr Akili
Tanganyika ni jina tulilopachikwa na Wakoloni wa Kiingereza, mimi huwa silipendi. Lina maana ya Tanga na Nyika. Yaani ukiacha Tanga (kwa Wasambaa) sehemu iliyobaki iliitwa nyika(ni) hadi huku kwetu.
ina maana ili ndilo tatizo la kupinga ili jina ? yaani TANGANYIKA really?

Kabla ya hapo wakoloni wa Kijerumani waliita nchi yetu Deusch Ostaafrica. Jina la Tanzania tulilibuni wenyewe na kulifuta kabisa (kulikana) hilo jina la kipuuzi alilotupa mkoloni, mwaka 1964.
Mbona Tanzania tunaikubali na imetokana na TANGANYIKA? kwa nini hatukuikana TANGANYIKA kwanza kabla ya MUUNGANO ili jina la TANZANIA litokane na jina la kibunifu?
Ni jina tu tulilolipenda hivyo hata Muungano wetu na visiwa vya Pemba na Zanziba ukifa sisi tutabaki na jina letu la Tanzania wala hatutarudisha hilo jina la nyikani (kwa masokwe). Sana sana tunaweza kurudisha la Ostaafrica (e.g. Nyerere Ostaafrica).
Huu uoga unatokana na nini? kama ni usokwe sio lazima upewe jina bana, sokwe sokwe tu

Waulize wa CRDB Bank, hilo jina CRDB walilipataje, kirefu chake nini wakati original CRDB ilishakufa! Jamani jina ni jina tu, unajiita ambavyo roho yako inapenda. Tunalazimika tu kuheshimu mipaka tuliyoundiwa na wakoloni lakini si majina waliyotuita. Zambia ilikuwa North Rhodesia, Zimbabwe ilikuwa North Rhodesia, Malawi ilikuwa Nyasaland, Tanzania ilikuwa Tanga-Nyika n.k.
Naomba jina la TANGANYIKA jipya na usiniambia ni TANZANIA hapo equation haito-balance maana lazima iwe
TANGANYIKA +ZANZIBAR = TANZANIA
But ZANZIBAR is not equal to 0, ukisema TANZANIA ni sawa na TANGANYIKA ni kuwatukana wazanzibar, watawaka tena tunawatukana
 
Au walikuwa wamekusudia kumpa Bi Kidude Nishani kwenye sherehe za Muungano maana sielewi uhusiano wa wake (Bi Kidude) na uhuru wa Tanganyika?

Yawezekana walipiga sana mvinyo wakachanganya TAREHE, na hayo ndio matatizo ya kuvunja kanuni au Taratibu, kwanza kwa nini waziite NISHANI za TANZANIA , wakati ilikuwa siku ya UHURU wa TANGANYIKA vipi matukio kuendana na SHEREHE husika, siku ya HARUSI kuna sababu za kuongelea jinsi ya kuhachana/divorce ?
 
  • Thanks
Reactions: FJM

Similar Discussions

Back
Top Bottom