Rais Kikwete umechakachua NISHANI .... Bi kidude ni Mzanzibar

huu mkanganyiko lazima uondoke, atuwezi kuisha mazingira machafu kiasi hiki,
Tuna sherehe ya Muungano na tahere zinajulikana, kisha tuna Tanganyika, kama kuna watu
wanaona kusema 9/12/1961 wa TANGANYIKA basi sherehe yenyewe iondolewe,
Nini maana ya kufanya sherehe ya kitu tunachokiogopa, tunafikia hatua tunachanganya hata majina ya nishani

Alieanzisha sherehe hizi za Uhuru wa Tanzania ni baba enu wa Taifa! sasa akienziwa kuna shida gani?
 
Alieanzisha sherehe hizi za Uhuru wa Tanzania ni baba enu wa Taifa! sasa akienziwa kuna shida gani?
Lini mwalimu alifuta jina la Tanganyika?! ( sio lazima kwamba alikuwa sahihi katika kila kitu anyway) lakini Kama hii itokea tunataka kuona historia ilisema hivyo
 
Kikwete ni kama yupo gizani, hajui anamtumikia nani!

Wapo hapa jamvini vilaza wake Nape Moses Nnauye na William J. Malecela wanajifanya watetezi wa serikali ya kikwete na wapo tayari kukifia chama ilimradi tu wahakikishiwe matumbo yao kujaa,

Hapa mimi nitaelekeza lawama kwa TISS hasa wakuu wa kitengo cha itifaki kwa rais.

Naamini leo rais akibanwa swali hilo atasema "ni upepo tu utapita"

Tukiendelea kukaa kimya mambo yatakuwa magumu huko mbeleni, tushindwa kuelewa kipi ni kipi, TANGANYIKA lazima iwepo ili kuwe na TANZANIA, huu usanii kwa kiita TANGANYIKA eti TANZANIA ndio matokeo yake NISHANI za watanganyika zinakwenda kwa wazanzibar, tuwaenzi wazanzibar kwa mambo yao, hisitoshe wanataka twende na passport huko Zanzibar, tuna mifumo ya kodi tofauti, wana sherehe yao ya mapinduzi ya Zanzibar kwa nini tuna zika kila kitu Mpaka jina la TANGANYIKA sana ni halamu
 
hapo kwenye blue,pamenichekesha sana
Mkuu, umesahau kwamba kimsingi hakuna tena taifa linaloitwa Tanganyika hapa duniani, labda kama tutaifufua tena. Na ndio maana hata katika michuano ya Challenge kule Uganda hakukuwa na taifa liitwalo kwa jina hilo. Muungano tulionao uliiua Tanganyika kabisa na pia Uliiacha Zanzibar hai lakini kwa kuhakikisha umeing'oa meno yote. Sasa Muungano tulio nao ni wa nchi mbili: moja imeuawa na ni marehemu na nyingine imeng'olewa meno yote kwa hiyo haina nguvu yake inayojitegemea. Sasa katika hali kama hii usitegemee kwamba kuna Utanganyika.
 
Yes, Kama tunaogopa utanganyika tufute hiyo sherehe, tuwe na ile ya MUUNGANO na ya ZANZIBAR, maana naona hata NISHANI zimechakachuliwa na kuwa NISHANI za TANZANIA siku ya UHURU wa TANGANYIKA, hii ni potosha HISTORIA, atuwezi kujifanya TANGANYIKA imefufa wakati kuna shehere za UHURU wake kila mwaka.

Tanganyika ni lazima irudi na katiba mpya la sivyo patachimbika. Tume ya maoni ya katiba waelewe kitu hiki na kitu kisiwaelewe wao.
 
Mimi ninawaomba Halima Mdee, John Mnyika, Joshua Nassari, Zitto Kabwe, Msigwa etc I believe in you because you're the VOICE of the VOICELESS. Kwenye Bunge lijalo kipindi cha MASWALI na MAJIBU mmuulize PM Pinda inakuwaje Rais wa JMT anatoa NISHANI ya UHURU wa Tanganyika/Tanzania bara kwa Wazanzibari?

Je Rais wa SMZ anaweza kutoa NISHANI ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa raia wa Tanganyika/Tanzania Bara?.

Kusdema kweli I'm SICK to a point of dying huyu ni RAIS gani anaendelea kUVUNJA KATIBA ya JMT aliyoahidi kuilinda with IMPUNITY.

Sitaki kusikia UPUUZI kwamba eti watu wa ITIFAKI ndiyo wamemshauri vibaya.
 
Tanganyika ni lazima irudi na katiba mpya la sivyo patachimbika. Tume ya maoni ya katiba waelewe kitu hiki na kitu kisiwaelewe wao.

serikali Tatu ni lazima, hatuwezi kuendelea kuishi kwa hisani, Kama walivyo na raisi na TANGANYIKA tuwe na serikali yetu, kama kuna watu wataona ni tatizo basi kusiwe na muungano, tunabembelezana sana, habari za usalama kulinda muungano ni uhuni, Kama issue ni usalama basi tuungane na Malawi, msumbiji, kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia na Congo ... Kwa nini Zanzibar tu ndio Mpaka wa kuhofia?!
Tutalinda mpaka huo Kama tunavyolinda mingine
 
Tanganyika ni lazima irudi na katiba mpya la sivyo patachimbika. Tume ya maoni ya katiba waelewe kitu hiki na kitu kisiwaelewe wao.

Msipokwenda kuyasema haya tena aggressively kwenye tume ya katiba Tanganyika haitarudi. FYI, Judge Warioba ni mpenzi na mshabiki mkubwa wa Serikali mbili i.e Ya Muungano na Zanzibar.
 
Siku ya uhuru iko moja tu Dec 9 ile ya Zanzibar sio ya uhuru ni ya Mapinduzi Zanzibar haijwahi kuwa huru kama Taifa, JK yuko sahihi kabisa Duniani hakuna Taifa lijulikanalo kama Zanzibari. Passport ya Bibi Kidude ya Tanzania
 
Mkuu, umesahau kwamba kimsingi hakuna tena taifa linaloitwa Tanganyika hapa duniani, labda kama tutaifufua tena. Na ndio maana hata katika michuano ya Challenge kule Uganda hakukuwa na taifa liitwalo kwa jina hilo. Muungano tulionao uliiua Tanganyika kabisa na pia Uliiacha Zanzibar hai lakini kwa kuhakikisha umeing'oa meno yote. Sasa Muungano tulio nao ni wa nchi mbili: moja imeuawa na ni marehemu na nyingine imeng'olewa meno yote kwa hiyo haina nguvu yake inayojitegemea. Sasa katika hali kama hii usitegemee kwamba kuna Utanganyika.
Aagh, mie hutaabika kidogo kwa watu wanaofikiri muungano wetu SI wa nchi MBILI!!!!!!
Huu ni muungano wa nchi MBILI bado na si zaidi yake, ni muungano wa nchi za TANGANYIKA na nchi ya ZANZIBAR. Tatizo nilionalo ni UFUNIKWAJI wa historia halisi. Pana makala walizokuwa wakizitoa ndugu Jenerali Ulimwengu na ndugu Joseph Mihangwa kupitia gazeti la Raia Mwema, hizo ni ELIMU tosha kwetu. Pia tume za majaji Nyalali na Kisanda zinatosha kabisa kututoa katika dimbwi hili la UJINGA kuhusu muungano huu.
 
Msipokwenda kuyasema haya tena aggressively kwenye tume ya katiba Tanganyika haitarudi. FYI, Judge Warioba ni mpenzi na mshabiki mkubwa wa Serikali mbili i.e Ya Muungano na Zanzibar.
Ndio maana yuko kwenye hiyo tume wenye maono tulishaliona zamani sana, kwanza walijaribu kusema hakuna kujadili ili suhala na madaraka ya raisi, walipoona ukinzani waka lunch plan B (silence whisper ) kwa kumtia mwenyekiti aliye na mapenzi furani,
TANGANYIKA lazima irudi ili twende sawa Hasa kwenye mgawanyo wa rasilimali, kwa sasa tunahudumia raisi wa Muungano kwa kiasi kikubwa ( Kama sio kila kitu) tuna hudumia polisi, mawaziri wa muungano, tuzo za NISHANI kwa wazanzibar, wapemba wanauza kariakoo wafaida inakwenda zanzibar ( Hawa ni wawekezaji wa kigeni kutoka zanzibar )
tutabeba huu mzigo na matusi yote haya.
Leo wamekaa huko wanataka Muungano wa Mkataba bila kutushirikisha wanasukuma/lazimisha watakavyo wao sisi tunafuata tu maana hatuna serikali ya TANGANYIKA
 
Mkuu, umesahau kwamba kimsingi hakuna tena taifa linaloitwa Tanganyika hapa duniani
Tanganyika ipo mioyoni mwa watanganika,na itaendelea kuwa mioyoni mwa watanganyika mbaka mwisho wa Dunia.Kumbuka
*maji huwa hayasahau njia zake hata ipite miaka mingapi!!
*Ni umbumbumbu kusherekea uhuru wa Tanzania Bara,wakati Tanzania bara haikuwahi kutawaliwa!!
 
Msipokwenda kuyasema haya tena aggressively kwenye tume ya katiba Tanganyika haitarudi. FYI, Judge Warioba ni mpenzi na mshabiki mkubwa wa Serikali mbili i.e Ya Muungano na Zanzibar.
Kweli kabisa huyu bwana kafaidika na muundo huu wa MASLAHI binafsi wa muungano hata mie nina SHAKA mno matokeo yake kwani yatapingana na ya tume mbili zilizopita. Mwenye macho haambiwi TAZAMA.
 
Salamu wandugu

Kwanza naomba nianze kwa kuweka kumbukumbu sahihi, Mimi ni Mtanganyika mwenye HESHIMA na Utanzania.
Lakini pia nimechoka na huu uzekezaji unaofanywa zidi wa wazanzibar

Siku ya UHURU wa TANGANYIKA Raisi Kikwete alitoa NISHANI mbalimbali hapa kuna matatizo (uchakachuaji wa aina mbili)

1. Uhuru ni Tanganyika lakini nishani zilitoka za Tanzania, sasa nashindwa ilikuwa ni siku ya UHURU wa Tanzania? na kama ndivyo na siku ya MUUNGANO tutatoa nishani zipi? nishani za Tanzania siku ya Tanganyika ni kuwatisha wazanzibar kwamba Tanganyika ndio Tanzania, hii sio sahihi ni uchakachuaji.

2. Bi Kidude kwenye nishani za TANGANYIKA anahusika vipi? ni nani asiyejua kwamba Bi Kidude ni Zanzibar?!!! tunawaogopa nini hawa wazanzibar mpaka siku ya UHURU wetu wa TANGANYIKA tujikombe na kuwanishani? vitu kama hivi ni uchakachuaji, lakini pia vinawapa kiburi wazanzibar, matokeo yake wanajisahahu kama walivyo sasa.

Mwisho ni kwa Watanganyika, tuwe macho, mambo kama haya yakitokeo VISIWANI wangepiga kelele na kusema wamedharauliwa, kwa upande wangu hii sio dharau lakini kama tunajikomba sana kwa wazanzibar mpaka kuwapa NISHANI za watanganyika

Mkuu tambua kitu kimoja:
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitokana na Muungano wa nchi ya Tanganyika na Zimbabwe mwaka 11964.
 
Tanganyika ipo mioyoni mwa watanganika,na itaendelea kuwa mioyoni mwa watanganyika mbaka mwisho wa Dunia.Kumbuka
*maji huwa hayasahau njia zake hata ipite miaka mingapi!!
*Ni umbumbumbu kusherekea uhuru wa Tanzania Bara,wakati Tanzania bara haikuwahi kutawaliwa!!
Haikuwepo 9 decemba 1961 na hata sasa tafuta kwenye ramani zote za dunia HAIPO.
 
Siku ya uhuru iko moja tu Dec 9 ile ya Zanzibar sio ya uhuru ni ya Mapinduzi Zanzibar haijwahi kuwa huru kama Taifa, JK yuko sahihi kabisa Duniani hakuna Taifa lijulikanalo kama Zanzibari. Passport ya Bibi Kidude ya Tanzania
Zanzibar ilipewa UHURU 1963, jaribu kuwa na ujasiri wa KUJISOMEA japo historia tu.
 
Salamu wandugu

Kwanza naomba nianze kwa kuweka kumbukumbu sahihi, Mimi ni Mtanganyika mwenye HESHIMA na Utanzania.
Lakini pia nimechoka na huu uzekezaji unaofanywa zidi wa wazanzibar

Siku ya UHURU wa TANGANYIKA Raisi Kikwete alitoa NISHANI mbalimbali hapa kuna matatizo (uchakachuaji wa aina mbili)

1. Uhuru ni Tanganyika lakini nishani zilitoka za Tanzania, sasa nashindwa ilikuwa ni siku ya UHURU wa Tanzania? na kama ndivyo na siku ya MUUNGANO tutatoa nishani zipi? nishani za Tanzania siku ya Tanganyika ni kuwatisha wazanzibar kwamba Tanganyika ndio Tanzania, hii sio sahihi ni uchakachuaji.

2. Bi Kidude kwenye nishani za TANGANYIKA anahusika vipi? ni nani asiyejua kwamba Bi Kidude ni Zanzibar?!!! tunawaogopa nini hawa wazanzibar mpaka siku ya UHURU wetu wa TANGANYIKA tujikombe na kuwanishani? vitu kama hivi ni uchakachuaji, lakini pia vinawapa kiburi wazanzibar, matokeo yake wanajisahahu kama walivyo sasa.

Mwisho ni kwa Watanganyika, tuwe macho, mambo kama haya yakitokeo VISIWANI wangepiga kelele na kusema wamedharauliwa, kwa upande wangu hii sio dharau lakini kama tunajikomba sana kwa wazanzibar mpaka kuwapa NISHANI za watanganyika

VIKWAZO
,
1. kwanza nikupongeze kwa kuliona hili na kulisemea huku ukikemea uzuzu unaopaliliwa na CCM
2. Pili nalazimiSHA KUMTETEA Mh Kikwete, nathubutu kusema kuwa Mh raisi AMEDANGANYWA, na huu sio mwanzo wala mwisho wa kudanganywa kwa Mh raisi...naye akadanganyika kisha akachakachua.
3. CCM sio oyee!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom