Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,797
- 71,216
Rais wetu amekubali kuwa ameiacha nchi ikiwa masikini pamoja na kuwepo ofisi kuu kwa miaka 10 pamoja na maandalizi yake ya miaka 10 mingine ili aingie ofisi hiyo. Cha kusikitisha ni kuwa kaamua kuyasemea hayo huko Uholanzi badala ya kuyasemea hapa nyumbani ambapo tungemuuliza kwa nini hali hiyo imetokea?
Angeyasemea hapa nyumbani kwa sasa yangetusaidia sana hasa wakati huu tukielekea kwenye uchaguzi mkuu maana tungejua sababu iliyomsababisha akaiacha nchi ikiwa masikini huku fedha nyingi sana zikiwa zimepotelea kwa mafisadi wachache? Jee ni yeye mwenyewe aliyeshindwa kazi au usimamizi mbovu wa serikali uliokuwa chini ya chama chake?
Ili aondoke na heshima ni vema atuweke wazi wananchi ili tuwe na maamuzi safi Octoba na yeye abaki salama huku tukimtunza kama mstaafu wa Urais. Hawezi kupoteza chochote kwa kuwa wazi na kuisaidia nchi yake isiendelee kupotea.