Rais kikwete ukimya wako ni angamizo kwa taifa letu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais kikwete ukimya wako ni angamizo kwa taifa letu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DOUGLAS SALLU, Apr 2, 2012.

 1. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,571
  Likes Received: 4,688
  Trophy Points: 280
  Mheshimiwa Rais Kikwete, imekuwa kawaida sasa kwa wanachama wa CCM kufanya vurugu kwenye chaguzi ndogo na hata kufanya mauaji. Hali hii haitokei kwa bahati mbaya kwani ni kawaida ya CCM kila kwenye chaguzi ndogo hizi kupeleka vijana kwenye makambi na kuwapa mafunzo ya kigaidi kwa baraka za uongozi wa juu wa chama ambacho wewe ni mwenyekiti wake.

  Yalitokea Tarime, Biharamulo,Busanda,Igunga ambapo makada wawili wa Chadema waliuawa kikatili na vijana hawa wanaopewa mafunzo ya kuua watu.

  Arumeru Mashariki wametekwa watu na kuteswa mpaka kuharibiwa sehemu za siri, Mwanza wabunge wawili wa Chadema wamecharangwa mapanga, katika matukio yote haya hatujasikia wahusika wakichuliwa hatua za kisheria kwa uhalifu huu, kibaya zaidi ni ukimya wako juu ya ugaidi unaofanywa na wanachama wako. Ukimya wako Mh. Rais ni kiashiria kuwa umebariki vitendo hivi vya kigaidi ili kulinda utawala wenu dhalimu.

  Ushauri wangu kwako Mh. Rais uvifute vyama vyote ibaki CCM peke yake ili kuokoa maisha ya watu wasiokuwa nahatia. Ukishindwa kuvifuta vyama hivi na kuendelea kukalia kimya ugaidi huu ujue nchi itaingia kwenye umwagaji mkubwa wa damu kwa ajili ya uroho wenu wa kubaki madarakani, na damu za watanzania hawa zitakuwa juu ya kichwa chako.
   
 2. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wala hajali, alishatishia hata wafanyakazi kuwa mkiandamana nitatumia dola kuwatuliza, kiongozi anayejivunia dola si wa kuaminika tena, hana uchungu na wananchi.
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Mimi naona mnamuonea
  Aseme nini wakati hana la kusema??
  Kama alishindwa kusema wakati wa mgomo wa madaktari unategemea atasema kwa ajili ya watu wachache waliojeruhuwa??

  Tafadhali, hebu soma mchezo.
   
 4. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hana uwezo wa kufuta vyama vya upinzani na kubakiza ccm. Kuhusu ukimya ni kwamba bado anasubiri mtoto wa mkulima aongee kisha nae afikirie nini tofauti na cha mtoto wa mkulima ili akakiongee kwa wazee wa darisalama.
   
 5. M

  Mponjori JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 2,210
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mwoneeni huruma rais wenu jamani,kuna watu wameshika remote controler yeye ni kama sensor,sensor haina maamuzi
   
 6. j

  jjjj Senior Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mi labda sijakuelewa,awezaje kufuta chama chake cha CCM ikiwa yeye ndiyo mwenyekiti?
  naye amechaguliwa Urais kupitia hicho chama akifuta atakuwa anamwakilisha nani?
  halafu akivifuta vyama vingine kibaki ccm peke yake hili sijaelewa wewe unakiri mwenyewe kuwa ccm wanafanya fujo ume
  diriki hata kueleza sehemu ambazo vifo vimetokea baada ya ccm kuleta fujo tena unataka vyama vingine vifutwe kibaki
  CCM.sijalielewa.hili
   
 7. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Umeongea ukweli kabisa. Lakini unafiki na udhaifu wa JK ndio utakaoikomboa Tanzania kutoka mikononi mwa wahuni, madhalimu, mafisadi na wanyanganyi.
   
 8. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Naamini kama hujakurupuka basi una upungufu wa akili, unasema ccm ndo chanzo cha vurugu katika chaguzi , then una suggest vyama vingine ndo vifutwe ili ibaki ccm watu wawe na amani. How comes? kwa nini usishauri hao wauaji ndo wafutwe ili watu wakae kwa amani. Tangu lini jambazi akivamia kijiji watu wanahama na kumwachia kijiji?

   
 9. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,571
  Likes Received: 4,688
  Trophy Points: 280
  Ni kweli hujanielewa mkuu, maana yangu ni kuwa kwa vile serikli dhalimu ya CCM ikiongozwa na JK haitaki kuendesha siasa za kistaarabu chini ya mfumo wa vyama vingi ambavyo viko kisheria basi airudishe nchi chini ya utawala wa chama kimoja, hapo hawatakuwa na mtu wa kugombana naye, kifupi ni kuwa ushauri niliompa ni kejeli kwa huyu kilaza JK (Janga la Kitaifa)
   
 10. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #10
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,571
  Likes Received: 4,688
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye bold,hii ni nchi huru unayo haki ya kuamini chochote,hata ungeamua kuamini kuwa mimi ndiye baba yako mzazi hakuna ambaye angekuzuia kuamini hivyo. Wewe ndiye umekurupuka, ungesoma kati kati ya mistari ungeelewa nilichomaanisha.
   
 11. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #11
  Apr 3, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,571
  Likes Received: 4,688
  Trophy Points: 280
  Kumtaka JK akemee mfumo alio uasisi yeye mwenyewe ni sawa na kumtaka ng'ombe dume atoe maziwa.
   
 12. MANI

  MANI Platinum Member

  #12
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  Sasa mkuu nini kifanyike maana watu wanateketea.
   
 13. MANI

  MANI Platinum Member

  #13
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  Mkuu kusoma na kuelewa ni vitu viwili tofauti msamehe bure tu !
   
 14. b

  bibi.com JF-Expert Member

  #14
  Apr 3, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 1,155
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  mi nilifikiri wanaume sio dhaifu jamani au?
   
 15. BINARY NO

  BINARY NO JF-Expert Member

  #15
  Apr 3, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,776
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  ICC the HAGUE ipo as long as evidence zipo acha waendelee ata hayo mataifa makubwa wanayojipendekeza nikua wanaona mchezo mzima mda ulifika watawatupa kwenye madust bin
   
 16. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #16
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,828
  Likes Received: 2,765
  Trophy Points: 280
  Wazee hapa naomba nipite kimya kimya nisijepelekwa cell na mh. Paw! Lakini nawashwa kumsema kidogo tu huyu Rais wa Pwani, Mods msinifunge tena ni kidogo tu msipige mayowe!! Hatuna Rais tuna GALASA!! Teh teh teh!
   
Loading...