Rais Kikwete: Tukatae madikteta Katiba Mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete: Tukatae madikteta Katiba Mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quinine, May 2, 2011.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,846
  Likes Received: 11,965
  Trophy Points: 280
  Rais Jakaya Kikwete amekemea watu wanaotaka kuhodhi mjadala wa mchakato wa kupata katiba mpya na amewafananisha na madikteta. Amesema watu hao wanajiona kuwa wao ndio wenye mawazo mazuri kuliko wengine.

  Alisema inashangaza kuona kuna watu wanaodhani kuwa wana mawazo mazuri kuliko wengine ilihali Katiba ni ya kila mmoja.

  "Kuhusu Katiba lazima tuchanganye mawazo ya wote hatuwezi kuwa na kikundi cha watu wanaotaka kusikilizwa wao tu wengine wakisema wanazomewa … katika hili lazima kila mtu atoe mawazo yake na yasikilizwe," alisema.

  "Tuwakemee wale wote wanaotaka kuhodhi mjadala wa Katiba, wanaojifanya kwamba wao ndio wenye mawazo mazuri kuliko wengine," alisisitiza.

  Alisema wanaotaka mawazo yao tu hao ni madikteta, na ni lazima Watanzania wawakatae madikteta.

  My take:
  Hivi huyu jamaa huwa anageuka nyuma na kuangalia kivuli chake kuwa kinafanana naye nina wasiwasi na IQ yake, ni nani anayehodhi uandishi wa katiba au hajui kukataliwa kwa mswada bungeni ni kutokana na yeye kuyahodhi madaraka kutoka uteuzi wa wajumbe hadi uchapishwaji. Ina maana amejijua kuwa yeye ni dikteta, kweli ukistaajabu ya musa utasikia ya filauni.

  GO Home
   
 2. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,634
  Likes Received: 1,401
  Trophy Points: 280
  kweli tuna kilaza pale magogoni, kwani ni lazima aongee?

  kama unajijua we zumbukuku kwa nini usitume hata wenye uwezo kidogo wakusaidie?
   
 3. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hii mbona iko wazi alikuwa anawasema CDM. Kumbe CDM ni chama cha kidikteta tuepukane nacho. Thanx Presidaaaaaaaaaaa
   
 4. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,846
  Likes Received: 11,965
  Trophy Points: 280
  Kwani CDM ndio waliopeleka mswada bungeni kwa hati ya dharula kama si maelekezo ya rais
  Kwani CDM ndio wanaoteua wajumbe 30 kama si rais
  kwani CDM ndio wanopelekewa taarifa za mchakato kila baada ya muda kama si rais
  Kwani CDM ndio watakaoidhinisha usahihi wa katiba kama si rais

  So kwa akili yako nani dikteta
   
 5. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kuwa na raisi mshabiki anayepelekewa kila kitu bila hata kufanya uchambuzi yakinifu anaruka nao.
  Jana amepata sehemu ya kuonyeshea uoga wake., Shame on him nausanii wake.
   
 6. T

  The GreatMwai Member

  #6
  May 2, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu hivi dikteta ni yupi kati ya anayetaka kila kitu kiamuliwe na yeye, watu wasijadili muswada kwa kupeleka kwa hati ya dharura na yule anayezomea watu wengine kama hawaendani naye kama ulivyowozomea CDM? Au ndo ule usemi wa mkuki kwa nguruwe .....
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  May 2, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kuna wakati huwa nashindwa kushangaa mpaka nashangaa, JK alichaguliwaje 2nd term.
   
 8. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #8
  May 2, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Muulize mnyika, ameisha tengeneza kabisa rasimu ya katiba mpya ! na anasema wameisha jadiliana chamani. Katiba, ndio kwanza mchakato umeanza , nyie mmeisha tengeneza ya kwenu, huu ni udikteta wazi wazi
   
 9. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #9
  May 2, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ww ndio ujiulize kwa nini hukumchagua wakati watu wote walimchaguana kushinda kwa kishindo na kwenye uchaguzi ulio huru na wa haki
   
 10. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #10
  May 2, 2011
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mhe.Rais sasa hapa unaonyesha wazi kuwa Tuikatae serikali yako kwa sababu ni madikteta kwenye suala la klatiba?
  Unataka sasa tukatae Mwanasheria mkuu wa serikali kwa kutaka mawazo yake yawekwe kwenye katiba na wananchi wasisikilizwe?
  Unataka tumkatae spika ambaye alisema kuwa mikoa mitatu tuu ndio itoe maoni yao kuhuisiana na katiba mpya?
  Unataka tukukatae wewe kwa kutotaka urais wako ujadiliwe kwenye mswada na hata katiba?

  Sasa hapa dikteta ni nani kati ya waliotaka mawazo ya wananchi yasikilizwe na aliyetaka mawazo yake na kakikundi kake ndiop yasikilizwe?
   
 11. M

  Mdau NO 1 Member

  #11
  May 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kayasema wapi haya?
   
Loading...