Rais Kikwete, toa tamko na msimamo wako

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
6,381
6,707
Ingawa wengi ambao tumekuwa tukikosoa staili ya utawala wa rais Jakaya Kikwete, tumeonekana wabaya. Ingawa lengo letu ni kumsaidia kufanya anachopaswa kufanya badala ya kugeuka kiguu na njia kila siku angani akizurura ughaibuni, tunaonekana wabaya. Hakuna ubishi kuwa nchi yetu sasa iko msambweni ikitishiwa kusambaratishwa na udini utokanao na ujinga, ukosefu wa ajira, usongo na husda kwa baadhi ya watu wetu tulioshindwa kuwaendeleza. Hapa ndipo unatakiwa uongozi wenye visheni na mipango madhubuti ili kupangua janga hili la kujitakia. Kumekuwa na malalamiko kuwa serikali inatumia nguvu nyingi kupambana na upinzani badala ya kutimiza wajibu wake.

Jeshi la polisi limekuwa jepesi kuwahi kusitisha mikutano ya upinzani. Bila kujua kuwa kuna upande mwingine ambao umekuwa ukiutumia udhaifu huu, sasa serikali inajikuta uso kwa uso na wahafidhina wenye hoja zao fichi. Je ni wakati wa utawala wa Kikwete kuwekwa kwenye mizani au kuumizwa na wale uliowadharau na kuwafumbia macho. Ingawa tunaona machafuko yanayoendelea kama matokeo ya udini, ukweli ni kwamba ni matokeo ya ufisadi, umaskini, ujinga, ufisi, uroho na kasumba.

Watu wetu wengi hawana ajira na hawajui kesho yao itakuwaje. Wamekata tamaa na wanaweza kutumiwa na yeyote awezaye hata kuwaahidi jibu achilia mbali kutoa hilo jibu. Hii ndiyo maana hot spots za vurugu ni kwenye makazi ya watu maskini kama vile Mbagala na siyo Oyester Bay wala Masaki. Walioko kule wana uhakika wa maisha wagombee au kuandamana kwa kitu gani? Sasa Kikwete amerejea. Tumshinikize atoe mwelekeo wa taifa. Kwa mazoea yake ya kutojali unaweza kuambiwa kuwa kesho ana safari ya kikazi kwenda nje. Amekuwa akituchezea akili hivyo. Kila kukitokea matatizo Kikwete na genge lake wako nje wakitanua huku umma wetu ukiendelea kuteseka. Amekuwa akitumia jeshi la polisi kuzuia rabsha. Sasa ameishiwa hadi anaanza kutumia jeshi ambalo kikatiba kazi yake ni kupambana na maadui wa nje na si wa ndani.

Tumalizie kwa kumuasa Kikwete kuwa kama hatabadili staili yake ya kutawala ataiweka nchi pabaya. Ameacha mambo yajiendee ambapo kila tapeli anaweza kuanzisha dhehebu au kundi la dini kama walivyofanya Uamsho na Ponda Issa Ponda. Tunao wachumia tumbo wengi waliojificha nyuma ya majoho ya dini kutokana na kuujua udhaifu wa Kikwete. Rais Kikwete toa tamko na msimamo kuhusiana na mwelekeo wa taifa letu.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Kwani Kikwete ndo nani? Ametoa matamko mangapi pale anapohitajika kufanya hivyo? Na hayo ambayo ameyatoa yameleta matunda gani?
 
Hivi atoe tamko gani? Sawa unamsaidia hebu sema sasa wewe ulipenda aseme nini?

Je ulitaka aseme waislam wote wauawe?
Ama atangaze hali ya hatari kwa taifa? Guys kila kitu kina hatua zake na mkihamalika ndipo mtakapokuza tatizo.

Achen mambo yaende kama yalivyokusudiwa huku kila mmoja akichukua tahadhari juu ya usalama wake ikiwa ni pamoja na kutulia nyumbani kuepuka misongamano na magenge ya fujo. Ama wataka hata hili raisi aseme?

Wala raisi wetu hana shida ambayo wengine wanaikuza na kama anamapungufu yake basi ni kama binadamu wengine tu ila si kama watu wanavyompakazia.
Tena napata hisia kwamba wapo wanaotamani hali hii iendelee hivi ili aonekane kikwete kama sio raisi shupavu ila kamwe halitawezekana manake tz si ya kikwete pekee ni ya watu wote.

Kwani ungekuwa wewe ungesema ama ungetoa tamko gani?
 
Napenda kutoa ushauri kwa Rais Kikwete kutumia busara na kulivunja BAKWATA mara moja.Naelewa hili si suala la serikali lakini ushahidi upo kwamba nyerere aliivunja jumuiya iliyokuwepo kabla ya Bakwata "kwa lengo la kuwapa waafrika uongozi wao wenyewe wa kiislam na kuleta maendeleo" bakwata waka rithishwa mali zote ya iliyokuwa jumuia ya waislam enzi hizo Bakwata tangia wakati huo hawakuweza kuleta maendeleo yoyote kwa waislam na mara zote serikali wanaikingia kifua hata kama kuna makosa ya wizi wa wazi kuna sheria za vyama visivo vya kiserikali inaweza kutumika kwa sababu hawa mali hizo ambazo ni pamoja na majumba na viwanja wamekua wakiviuza kwa ubadhirifu mkumbwa.

La kushangaza serikali na kamanda kova tumemuona anatetea wizi na ufisadi huu fujo zinazotokea zinasababishwa na waislam kuchoka kuona Bakwata inafanya inavotaka na kufisadi mali za waislam na serikali inaikinga kifua hata waislam wanapo jaribu kuzuia kwa njia za kimahakama kwa sasa bakwata baada ya kuona hawana waislam ambao wapo nyuma yao wanauza mali hizi kwa kasi ya ajab.

Mheshimiwa rais kama kiongozi wa nchi una wajibu kuona amani haitoweki kutokana na hili na kwa vile na wewe ni muislam unalo jukumu kubwa kuhakikisha suala la Bakwata unalimaliza kabla ya muda wako wa urais haujaisha Livunje hili baraza na badala yake haraka uunde kamati ya muda ambayo itatoka kutoka madhebu yote ya waislam tanzania.Kumbuka Bakwata ndio baraza linalotambuliwa na serikali kuhusu mambo yote ya waislamu.

hivyo ni vyema kamati hio ikatoka kutoka madhehebu yote ya waisalm mfano sunni, shia,ibaadhi,bohora,ansari na wengineo.
kazi ya kamati hii ya muda itakuwa ni kuhakiki mali zote za waislam zilizopo na zilizouzwa kwa njia ya udanganyifu na kutengeneza katiba ya muda amabyo itapitishwa na misikiti yote uwekwe utaratibu wa kuchagua viongozi wapya ambao uwe wa wazi na wanaokubalika.

nakuhakukishia mheshimiwa rais utakuwa umewafanyia hisani kubwa wasilam wa nchii na kwa taifa lako. hili inawezekana na pia naamini kama ulivokuwa na ujasiri wa kuwapatia watanzania katiba mpya basi na hili utaweza. Allah akupe nguvu ufanye wema kuepusha shari ya kukumbatia baraza lisilotakiwa
 
Na pia ahakikishe ameifunga mitandao kama jamiiforum inyochochea uvunjifu wa amani kwa watu ambao hata jana humu wameliambia kuwa jeshi likae tayari na leo tumeliona linafnya doria,hii sio kazi ya jeshi, kwaiyo mtu mmoja tu humu aneza kusababisha jehi letu likatekwa, tunaiyomba serikali inteljesi ifanye kazi yake na sio ifate mambo ya hum jamiiforum
 
akitoa tamko atasema natoa wito kwa pande note................ hata akitoa agizo sidhani kama litatekekezwa.
 
..."Tumshinikize atoe mwelekeo wa taifa...." Tumalizie kwa kumuasa Kikwete kuwa kama hatabadili staili yake ya kutawala ataiweka nchi pabaya. Ameacha mambo yajiendee ambapo kila tapeli anaweza kuanzisha dhehebu au kundi la dini kama walivyofanya Uamsho na Ponda Issa Ponda.."
Mungu ibariki Tanzania.

Ngd yangu Father of All, hivi wewe hujui kuwa sikio la kufa halisikii dawa?
Unanisikitisha sana kuona bado unategemea kitu kutoka kwa huyo vasco dagama. Nakwambia fikiria habari ya kumweka pembeni, siyo mambo ya kumshinikiza atoe msimamo!!
Nakwambia utoe kabisa fikra kama hizo kichwani, haya yanayotokea hayajaanza leo bali ni matunda ya miaka 6 iliyopita. Unafikiri atafanya nini leo???? Nawaasa wenye mawazo kama hayo, wageuke upande wa pili, huko ni chaka tu!!!
 
Atasema kitu gani zaidi uongo? Raisi anakuwa kama katibu kata matamko dhaifu yanakuja kukinzana na ukweli! Hii aibu sana.
 
Ingawa wengi ambao tumekuwa tukikosoa staili ya utawala wa rais Jakaya Kikwete, tumeonekana wabaya. Ingawa lengo letu ni kumsaidia kufanya anachopaswa kufanya badala ya kugeuka kiguu na njia kila siku angani akizurura ughaibuni, tunaonekana wabaya. Hakuna ubishi kuwa nchi yetu sasa iko msambweni ikitishiwa kusambaratishwa na udini utokanao na ujinga, ukosefu wa ajira, usongo na husda kwa baadhi ya watu wetu tulioshindwa kuwaendeleza. Hapa ndipo unatakiwa uongozi wenye visheni na mipango madhubuti ili kupangua janga hili la kujitakia. Kumekuwa na malalamiko kuwa serikali inatumia nguvu nyingi kupambana na upinzani badala ya kutimiza wajibu wake.

Jeshi la polisi limekuwa jepesi kuwahi kusitisha mikutano ya upinzani. Bila kujua kuwa kuna upande mwingine ambao umekuwa ukiutumia udhaifu huu, sasa serikali inajikuta uso kwa uso na wahafidhina wenye hoja zao fichi. Je ni wakati wa utawala wa Kikwete kuwekwa kwenye mizani au kuumizwa na wale uliowadharau na kuwafumbia macho. Ingawa tunaona machafuko yanayoendelea kama matokeo ya udini, ukweli ni kwamba ni matokeo ya ufisadi, umaskini, ujinga, ufisi, uroho na kasumba.

Watu wetu wengi hawana ajira na hawajui kesho yao itakuwaje. Wamekata tamaa na wanaweza kutumiwa na yeyote awezaye hata kuwaahidi jibu achilia mbali kutoa hilo jibu. Hii ndiyo maana hot spots za vurugu ni kwenye makazi ya watu maskini kama vile Mbagala na siyo Oyester Bay wala Masaki. Walioko kule wana uhakika wa maisha wagombee au kuandamana kwa kitu gani? Sasa Kikwete amerejea. Tumshinikize atoe mwelekeo wa taifa. Kwa mazoea yake ya kutojali unaweza kuambiwa kuwa kesho ana safari ya kikazi kwenda nje. Amekuwa akituchezea akili hivyo. Kila kukitokea matatizo Kikwete na genge lake wako nje wakitanua huku umma wetu ukiendelea kuteseka. Amekuwa akitumia jeshi la polisi kuzuia rabsha. Sasa ameishiwa hadi anaanza kutumia jeshi ambalo kikatiba kazi yake ni kupambana na maadui wa nje na si wa ndani.

Tumalizie kwa kumuasa Kikwete kuwa kama hatabadili staili yake ya kutawala ataiweka nchi pabaya. Ameacha mambo yajiendee ambapo kila tapeli anaweza kuanzisha dhehebu au kundi la dini kama walivyofanya Uamsho na Ponda Issa Ponda. Tunao wachumia tumbo wengi waliojificha nyuma ya majoho ya dini kutokana na kuujua udhaifu wa Kikwete. Rais Kikwete toa tamko na msimamo kuhusiana na mwelekeo wa taifa letu.

Mungu ibariki Tanzania.
kikwete atoe tamko gani?ambalo wametoa maaskofu ndilo hilo ambalo serikali inalifanyia kazi.
 
Tumechomewa makanisa makafiri,yeye inamhusu nini?asikae baharini akala upepo ahangaike na makafiri?Tutamsaidia nini tena sisi makafiri?Sidhani kama ana cha kusema kwa makafiri kama sisi,na wala sitaki atusemee sisi makafiri,lakini akae akijua 2015 ndio tutamuonyesha kuwa sisi ni wakina nani!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom