Rais Kikwete, toa tamko kuhusu mafuta: Tunaumia wananchi!

Jk mnamuonea tu mkwele wa watu!! Kwanza kwa sasa hawezi kufikiri sana, maana swaumu ndo mwezi mbichi. Acheni hizo bana!! Prezidaa kwa sasa amefunga bana!!

Kwanza hata haya mambo ya sijui wese, sijui nini, si ni uchonganishi tu wa magazeti.

Laleni Mungu yupo inshalaah, ataleta kheri!!
 
Kikwete ni chaguo la Mungu,ni kweli Mungu alimchagua Kikwete ili CCM imfie mkononi na cku ya mwisho tupate ukombozi wa kweli,RIP CCM!
 
Sio Waziri wa Wizara husika, wala Waziri Mkuu, wala Rais wa nchi ametoa tamko juu ya huu mgomo wa wauza mafuata? Nchi hii inaongozwa na nani? Hawa wauza mafuta wanapata leseni wapi?

Na yule mwenyekiti wa kamati ya bunge inayoshughulika na nishati na madini yuko wapi? au interest yake iko Dowans peke yake?
 
Napata uchungu sana napoona serikali yetu ilivyo dhaifu, kiasi hata inashindwa kusimamia maagizo yake.

Serikali ilitoa agizo la kushushwa kwa bei ya mafuta. Tena agizo likasisitiza kuwa wafanyabishara wa mafuta watakaofunga vituo kwa kisingizio chochote watakiona.

Lakini wiki moja imekwisha bila agizo hilo kutekelezwa. Vituo vimefungwa na serikali badala ya kuchukua hatua eti inawaomba wamiliki wa vituo wapunguze bei.

Nimemsikia afisa mmoja wa EWURA akisema "tunatoa wito vituo vyote viuze mafuta." alitoa kauli hii baada ya kutembelea vituo tisa na kukuta ni vitatu tu vyenye kutoa huduma.

Hivi Serikali huwa inatoa wito au huwa inaagiza? Serikali inayoshindwa kutekeleza maagizo yake ni serikali ya hovyo sana.

Jamani, Serikali hii haina sababu ya kuendelea kuwepo.

Amesha toa tamko kuwa viongozi wa dini waombe ili vua zinyeshe mabwawa yajae maji. Tamko ili alilitoa alipo futuru na viongozi wa dini
 
Atoe tamko wakati yeye na serikali yake walipewa masaa 24,
Nyerere alituambia huyu hafai kuwa rais mwaka jana tukaambiwa tukimchagua tutajuta hivi mnataka malaika aje atuambie acha tukome tukomae ili akili itukae sawia.

Chadema haina haja tena ya kuitisha maandamano kuna siku watu wataingia mitaani wenyewe.
 
Bei za mafuta haziwezi kushushwa kwa matamko, serikali lazima ishughulikie uchumi. Katika karne hii uchumi hauongozwi kwa matamko ya Nape NNauye na CCM! Ikiwa shilingi inadhoofika kila kukicha, waagizaji mafuta lazima wauze bei itakayowawezesha kuagiza stock nyingine.

Bei za mafuta hazifuati kodi tu, au bei iliyopo sokoni bali inatazama mwelekeo wa shilingi dhidi ya fedha za kigeni! Inachotakiwa serikali sio kutoa maagizo bali kushughulikia uchumi, kudhibiti mfumuko wa bei, na kuifanya shilingi stable ili waagizaji wa mafuta waweze kukadiria gharama na faida na hapo ndipo bei zita-stabilize.

Sasa matamko ya wakina Nape, kulazimisha serikali kushusha bei huku wakijua kuwa uchumi uko taabani matokeo yake ndiyo hayo! Total chaos! Watanzania tusikubali kudanganywa na matapeli wa CCM. Uchumi wa zamani wa Chama kushika hatamu na kutoa matamko hauwezekani tena kwa sasa!
 
Sio Waziri wa Wizara husika, wala Waziri Mkuu, wala Rais wa nchi ametoa tamko juu ya huu mgomo wa wauza mafuata? Nchi hii inaongozwa na nani? Hawa wauza mafuta wanapata leseni wapi?

Na yule mwenyekiti wa kamati ya bunge inayoshughulika na nishati na madini yuko wapi? au interest yake iko Dowans peke yake?
rais i mwenye akili ya ubwabwa ubwabwa unategemea nini! kwa usawa huu atakuwa anawazia daku tu saa zote!
 
Hivi hili suala la mafuta Ngeleja hahusiki nalo? Yuko wapi? Mbona hasemi lolote? Ile budget yake itapita kweli? Mimi nadhani Ngeleja ajiuzulu kwa niaba ya JK angalau tutaona uwajibikaji.
 
Tatizo letu sisi mitanzania ni mioga!!maybe na mimi nikiwemo!!!kwanini tusiwashinikize kwa kupaza sauti mabarabarani???au tunasubili mpaka asubuhi tushindwe kwenda makazini na shuleni?

Amani kwenye njaa haitadumu kila mwaka Wandugu!!!tutakaa na kusubili watu wawajibuke mpaka lini??au watoe tamko...kwani hatuna macho na akili za kuchambua!!!this is crazy wandugu!!!
 
Atoe tamko wakati yeye na serikali yake walipewa masaa 24,
Nyerere alituambia huyu hafai kuwa rais mwaka jana tukaambiwa tukimchagua tutajuta hivi mnataka malaika aje atuambie acha tukome tukomae ili akili itukae sawia. Chadema haina haja tena ya kuitisha maandamano kuna siku watu wataingia mitaani wenyewe.

Na bado!!!yan mpaka tunye!!!MITANZANIA BWANA!!KAMA KENGE AKIONA YAI!!HAJUI KUWA NI MTEGO COZ NI YAI LA KUCHEMSHA SO HALIPASUKI KWENYE KOO!!!
 
Msimbugudhi JK wa watu mwe...yuko mfungo swaumu kali mwacheni atulie khaaaa...
 
Napata uchungu sana napoona serikali yetu ilivyo dhaifu, kiasi hata inashindwa kusimamia maagizo yake.

Serikali ilitoa agizo la kushushwa kwa bei ya mafuta. Tena agizo likasisitiza kuwa wafanyabishara wa mafuta watakaofunga vituo kwa kisingizio chochote watakiona.

Lakini wiki moja imekwisha bila agizo hilo kutekelezwa. Vituo vimefungwa na serikali badala ya kuchukua hatua eti inawaomba wamiliki wa vituo wapunguze bei.

Nimemsikia afisa mmoja wa EWURA akisema "tunatoa wito vituo vyote viuze mafuta." alitoa kauli hii baada ya kutembelea vituo tisa na kukuta ni vitatu tu vyenye kutoa huduma.

Hivi Serikali huwa inatoa wito au huwa inaagiza? Serikali inayoshindwa kutekeleza maagizo yake ni serikali ya hovyo sana.

Jamani, Serikali hii haina sababu ya kuendelea kuwepo.

Kama alivyosema kuwa hana uwezo wa kuleta mvua uli kuondoa mgawo wa umeme, mkimlazimisha atete atasema kuwa hana uwezo wa kuingilia soko huriaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom