Rais Kikwete: Sina mgombea Urais

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,678
22,685
Licha ya idadi kubwa ya makada wa CCM waliojitokeza na wanaoendelea kujitokeza kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwania urais kupitia chama hicho tawala, Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake amesema hana mgombea, hivyo asihusishwe nao.

Amesema baadhi wamekuwa wakiomba ridhaa yake, lakini hakunaaliyemkatisha tamaa huku akimtakia kila la heri anayejiona ana ubavu wa kutaka kumrithi baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Aidha, amesisitiza ana imani na chama anachokiongoza, kitafanya chaguo sahihi na mgombea wa urais atakayepeperusha vyema bendera ya CCM katika mchakato wa kumpata Rais wa Awamu ya Tano waTanzania baadaye mwaka huu.

Rais Kikwete alisema hayo juzi usiku katika mkutano wake na Jumuiya ya Watanzania waishio Uholanzi, uliofanyika katika hoteli ya Crownie Plaza mjini hapa.

Alisema hayo alipokuwa anaelezea hali ya kisiasa nchini na pia maandalizi yanayoendelea ya uchaguzi mkuu ujao na pia mchakatowa Kura za Maoni ya Katiba Inayopendekezwa.

Hana mgombea Akizungumzia mbio za urais zinazoendelea kushika kasi, alisema hali ya kisiasa ya Tanzania ni shwari, licha ya kuwa kumekuwa na kishindokatika kuwania kumrithi.

"Nyumbani hali ni shwari, lakini kwa kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi kuna mengi yanayoendelea, hasa mchakato wa kuwania Urais… huko CCM mpaka leo (juzi) watu 15 walishachukua fomu, na wengine zaidi ya 15 ama wametangaza nia au wanakusudia kufanya hivyo.

"Ndiyo demokrasia ndani ya CCM, lakini niwahakikishie acheni waumane, lakini mimi binafsi sina chaguo langu.

Chama ndicho kitakachoamuana ninaamini kitatupatia kiongozi sahihi kwa saizi na hadhi ya CCM na huyu atatuvusha mpaka Ikulu," alisema.Aidha, alisema wapo wanaojipitisha kwake wakiomba kuungwa mkono, lakini pamoja na hayo, akasisitiza hana mgombea.

"Jana (Jumapili), kuna mtu alinitumia ujumbe akisema anakusudia kutia nia hivyo nimpe baraka zangu…nikamwambia `Goodluck' (Kila la heri), sasa kama alitafsiri ndiyo tayari mambo safi, aah…sijui bwana, ila mimi sina mgombea.

"Nasisitiza chama chetu ni makini na kitatupatia mgombea makini.

Mwenyezi Mungu atuepushiembali ili tusipate kiongozi atakayeipeleka nchi pabaya," alisema na kuwataka Watanzania hao kutokuwa na hofu juu ya mchakato huo ndani ya CCM.


Chanzo:
Habari Leo
 
Kutokuwa na mtu sidhani kama ni jambo jema kwa nafasi yake kama baba anapokaribia kustaafu alitakiwa awe na mtoto aliyempima vizuri kwa vigezo vya manufaa ya Taifa . . . . . kama tumemuamini katika miaka kumi basi tusingeshangaa kama angekuwa na majina mawili ambayo yangefanyiwa kazi na mwisho tuchague. . . . . . . Ok mzee hana jina la anayefaa lakini pia hajui hata wasiofaa??!!!

Haya tuombe kuepushwa. . . .
 
Kutokuwa na mtu sidhani kama ni jambo jema kwa nafasi yake kama baba anapokaribia kustaafu alitakiwa awe na mtoto aliyempima vizuri kwa vigezo vya manufaa ya Taifa . . . . . kama tumemuamini katika miaka kumi basi tusingeshangaa kama angekuwa na majina mawili ambayo yangefanyiwa kazi na mwisho tuchague. . . . . . . Ok mzee hana jina la anayefaa lakini pia hajui hata wasiofaa??!!!

Haya tuombe kuepushwa. . . .

Ccm upo utaratibu wa kuchuja na kuchagua mtu atakayepeperusha bendera.
 
Huyu ndio rais hana makundi na tumeshuhudia uongozi wake uwajibikaji upo sijui wapinzani wanataka uongozi gani.
 
Hapo ndiyo utampenda jk hana kundi wala hana kisasi na mtu anataka chama kiamue.
 
Mbona anashindwa kumkataa Lowasa? Lowasa kamuamrisha kuwa Amsaidie kwakua Yeye Lowasa alimsaidia sana kupata Urais... Pengine alimsaidia na.mengine
 
sina imani na kauli hii ya jk. yaani kwa nini mtu kugombea urais mpaka apate kibali kwke? hapo kuna wallakini.
 
Huyu ndio rais hana makundi na tumeshuhudia uongozi wake uwajibikaji upo sijui wapinzani wanataka uongozi gani.

mkuu unazungumzia makundi gani? ni jk huyuhuyu aliongoza kugawa vyeo kwa kwa ndugu na marafiki waliokuwemo kwenyemtandao wake kama njugu. mkuu ww unaishi hapa tanzania ama..... haa haa.
 
mkuu unazungumzia makundi gani? ni jk huyuhuyu aliongoza kugawa vyeo kwa kwa ndugu na marafiki waliokuwemo kwenyemtandao wake kama njugu. mkuu ww unaishi hapa tanzania ama..... haa haa.

Vyeo vilitolewa kwa undugu au kwa sifa? Demokrasia iliyoonekana kipindi cha kikwete kuna hawamu yoyote uliwahi kuiona? Je miaka ya nyuma uliona wapinzani wanasauti kama leo ya kumtukana rais hadharani? Kama ni undugu na urafiki Rostam na El wasingewajibika kwenye utawala wa JK au tatizo kubalance vyeo bila kujali dini,kabila na jinsia ndio undugu?
 
umesoma vizuri lakini gazeti husika?

nimerudia mara 3 kitendo cha huyo mgombea kumweleza kwanza jk kabla ya kutangaza azma kina maanisha huyo mgombea aliwahi jadiliana na jk juu ya jambo hilo. isingewezekana kamwe. jk anawazuga tu watu hapo.
 
Back
Top Bottom