Rais Kikwete sasa kuunda kamati mpya ya madini

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Rais Kikwete sasa kuunda kamati mpya ya madini
*Itajumuisha wapinzani, wasomi na wataalam wa madini

Na Waandishi Wetu, Dodoma

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa serikali itaunda kamati ya kutazama upya mikataba na sheria ya madini ambayo itajumuisha pia wanasiasa wa chama tawala na upinzani.

Kamati hiyo itatakiwa kushauri marekebisho ya yanayostahili kufanywa katika mikataba hiyo, ili iweze kuinufaisha zaidi nchi kuliko ilivyo sasa ambapo mikataba mingi inawanufaisha zaidi wawekezaji katika sekta hiyo.

Wengine watakaohusishwa katika kamati hiyo ni wanasheria, wasomi, wachumi, wataalam wa madini.Kamati hiyo itakayoundwa inatarajiwa kutatua matatizo ya kisheria katika mikataba ya madini, jambo ambalo limezua mjadala mkubwa kwa wananchi na wadau mbalimbali wa sekta hiyo.

�Kwa vile jambo limezua mjadala sana na kupelekea watu kudhani kuna kitu serikali inaficha, ni makusudio yangu kuunda kamati pana zaidi ya kutazama upya sheria ya madini na kushauri marekebisho yanayostahili,� alisema.

Rais Kikwete alifafanua pia kuwa, sekta ya madini nchini inakabiliwa na upungufu katika baadhi ya vipengele vya mikataba ya utafutaji na uchimbaji wa madini na ana lengo la kuifanyia marekebisho makubwa ili kuwanufaisha Watanzania badala ya hali ilivyo sasa, ambapo wawekezaji ndiyo wanaonufaika zaidi.

Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, alisema sekta ya madini nchini inakuwa kwa kasi na inayovutia wawekezaji barani Afrika na ina fursa kubwa ya kuchangia zaidi kwenye pato la taifa kwa fedha za kigeni, ingawa hadi sasa mchango wake bado ni mdogo sana ambayo ni sawa na aslimia 1.9.

Alisema kuwa, katika mikataba ya madini kumekuwapo na kipengele cha kumlinda mwekezaji iwapo anapata hasara kwa mtaji kwa kile alichodai kuwa, iwapo atashindwa kufidia gharama zake za uwekezaji hasara hiyo huhamishiwa mwaka unaofuata.

�Mwekezaji hupewa nafuu ya asilimia 15. Maana ya kipengele hicho ni kuwa, mwekezaji atachelewa kuilipa serikali kodi ya mapato na inawezekana

asilipe kabisa katika uhai wa mgodi wake,� alisema Kikwete.

Alisema kuwa pamoja na nia njema ya kuvutia wawekezaji, sheria hiyo ilijali kumlinda mwekezaji asipate hasara na ikasahau kumlinda Mtanzania anayepata hasara ya dhahabu yake inayochukuliwa kwa ajili ya kufidia hasara anayopata.

Alisema kuwa, hoja yake na Watanzania wote ni kuwa lazima mkataba ulinde pande zote mbili zinufaike sawa. Aliongeza kuwa baada ya kulizungumza na baadhi ya makampuni yamekubali kifungu hicho kiondolewe na kubaki na mfumo wa msingi uliopo kwenye sheria.

�Mfumo huo umeainisha wazi haki na wajibu wa mwekezaji. Upande wa wajibu wa mwekezaji anatakiwa kulipa kodi zifuatazo: Kwanza mrabaha wa asilimia

3, pili kodi ya mapato ya asilimia 30,� alisema na kuongeza kuwa kodi hiyo huanza kulipwa baada ya mwekezaji kufidia mtaji aliowekeza.

Alisema kuwa kutokana na hali hiyo alilazimika kupigia kelele kipengele cha nafuu ya ziada ya asilimia 15 ya mtaji kwa mwekezaji, iwapo hakufidia

mtaji aliowekeza katika mwaka husika.

Alisema kuwa kipengele hicho kinazuia na kuchelewesha Tanzania kupata kodi ama kinaweza kusababisha tukose kodi hiyo kabisa na kwamba sasa Tanzania

inapata kodi hiyo.

Alisema kuwa mgodi unapoanza kutoa gawio kwa wenye hisa, gawio hutozwa kodi ya aslimia 10 na makampuni ya madini hutakiwa kulipa kodi ya huduma za kiufundi ya asilimia 5 na kodi ya asilimia 15 ya gharama za menejimenti.

Rais Kikwete alisema kuwa kimsingi makampuni pia yanapewa nafuu ya kutokulipa ushuru wa mitambo inayoingia nchini sanjari na mahitaji ya uwekezaji kutoka nje.

�Huo ndiyo mfumo wa kodi katika mikataba ya madini. Mfumo huo ndiyo unatumika kwa kila mwekezaji wa madini. Hakuna mazungumzo wala maelewano maalum baina ya mwekezaji na Afisa wa Serikali awe Waziri, Katibu Mkuu, Kamishina au Mwanasheria Mkuu wa Serikali au Kamati ya majadiliano ya serikali.

Katika mazingira haya, kama tunapata hasara, siyo kwa hila ya mtu, bali itakuwa kwa sababu ya mfumo uliopo kwa mujibu wa sheria,� alisema Kikwete.

Alisema kuwa baada ya kubaini mapungufu kupitia kamati iliyoundwa, tayari maeneo yenye mapungufu yameainishwa na kufanyiwa marekebisho hususani katika kifungu kinachomlinda mwekezaji, bila kujali mwenye rasilimali.

Rais Kikwete alisema kuwa serikali pia inajenga uwezo wa uhakiki wa mitaji inayowekezwa na shughuli zinazofanywa na makampuni ya madini, nia ni kuwa

na uwezo wa kuhakiki taarifa za kampuni kuhusu uwekezaji na shughuli zao.

Juu ya mapambano dhidi ya rushwa Mwenyekiti huyo wa CCM, alisema kuwa katika kuhakikisha kunakuwa na mafanikio katika vita hiyo, Bunge limetunga sheria mpya mwezi Februari mwaka huu na hivyo kupanua wigo wa vitendo vya rushwa tofauti na ilivyokuwa siku za nyuma.

Alisema kuwa sheria hiyo imeongeza adhabu kwa wahalifu ikiwa ni pamoja na kufilisiwa mali ya mtu aliyekutwa na makosa ya rushwa, sanjari na hilo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa imeimarishwa.

Alidai kuwa taasisi inayo uhuru kamili wa kufanya kazi zake bila kuingiliwa na mtu yeyote na pia ina mamlaka ya kufikisha mashauri mahakamani tofauti na ilivyokuwa zamani.

Alisema kuwa taasisi hiyo inayopambana na rushwa ina mtandao mpana zaidi ikiwa na ofisi katika wilaya 113, pia imaejiri watumishi wapya 396 na utaratibu wa mafunzo umeimarishwa kwa ajili ya watumishi wake ndani na nje ya nchi.

�Nimewaahidi kuwa mimi sitawatisha wala kuwaingilia ili wasimwogope mtu yeyote�.sasa wanaendesha kesi 246 mahakamani. Hata makada wa chama tawala ni miongoni mwa watuhumiwa, pia wanaendelea na tuhuma 38 za watumishi wa umma wenye mali nyingi zisizolingana na kipato chao.�

Mimi napenda kuuliza kama uamuzi huu wa leo unakuja baada ya kupitia mikataba ama kauli ya mwanzo haikuwahi kufanya kazi ?
 
Karamagi alisema mazungumzo ya Mikataba yamemalizika na ya kuwa mkataba wa Buzwagi ndio umeboreshwa zaidi.. sasa haya mengine ya nini? Si tayari Sheria ya Madini imeshaanza kufanyiwa mabadiliko..
 
the man is serious, sasa sijui kama upinzani will still EXIST in the same manner as it is ! tafuteni kazi nyingine jamani, the man needs props !

hongera rais JK !

kamua babu endelea hivyo hivyo ! usiogope, endeleza cheche !
 
Kada, hivi si walisema mikataba tayari imeshapitiwa na imeboreshwa, na kuwa serikali haifanyi kazi kwa shinikizo.. sasa haya mazingaombwe ya nini?
 
serikali will do anything to benefit wananchi wake and at any time ( no time frame ), so hata kama hawakuwa CONSISTENT na walichosema before, then wakaja na better idea than the one they had before, why not go with the better idea ? au kwa sababu walishasema kitu prior the better idea ndio imaanishe wasifanye mambo bora zaidi au ?

mie naona hapa wanastahili pongezi na naipongeza serikali kwa hili, tena tushukuru wapinzani, wataalamu wa madini, na wengine wameshirikishwa !

hata hapo babu hutoi props ??
 
hawakuja na better idea, the didn't have one in the first place.. haya mawazo ya wengine wao wanayakumbatia.. kwanza ni aibu kwa Rais kukiri kuwa tumeshindwa kutengeneza mikataba yenye kunufaisha Taifa! yaani tumeshindwa kuingia makubaliano yenye kunufaisha Taifa, na Rais anakiri hilo... halafu wale wale walioshindwa kufanya hivi wanatarajiwa waje na mawazo mapya? c'mmon Kada najua ni mkereketwa lakini not on this buddy!
 
hapa naweza nikasema umeonyesha LOW THINKING SKILLS !
Unadhani maendeleo huletwa na mawazo ya mtu mmoja ? hata kama wazo ni lako binfasi, una maana wasitumie hilo wazo kuleta maendeleo ili wananchi tuendelee ? kwani tupo hapa JF kufanya nini ? kubomoa tu serikali bila ya kuishauri (serikali kutumia mawazo ya baadhi ya wananchi?)

Hakuna aibu yoyote kwa rais kuonyesha kwamba tumeshindwa, that shows how REAL AND STRONG he is, kumbuka hata mwalimu alikiri pale alipokosea, sasa kama only upo after Muungwana and not his policies hapo nitakuelewa !

Wale wale walioshindwa kufanya hivi wanatarajiwa waje na mawazo mapya ? yes, kwa kuwashirikisha wapinzani, na wataalam ! YES I BELIEVE WE CAN DO IT, AND YES I BELIEVE WE CAN ACHIEVE IT !

Lets not criticise something we havent tried yet !
 
hawakuja na better idea, the didn't have one in the first place.. haya mawazo ya wengine wao wanayakumbatia.. kwanza ni aibu kwa Rais kukiri kuwa tumeshindwa kutengeneza mikataba yenye kunufaisha Taifa! yaani tumeshindwa kuingia makubaliano yenye kunufaisha Taifa, na Rais anakiri hilo... halafu wale wale walioshindwa kufanya hivi wanatarajiwa waje na mawazo mapya? c'mmon Kada najua ni mkereketwa lakini not on this buddy!

Ni kweli ni aibu kubwa kwamba maslahi ya wananchi na rasilimali zao hazikupewa kipa umbele wakati wa utengenezaji wa mikataba hiyo!Walakini hapo ni mkubwa sana!J e waliotengeneza hiyo mikataba mibovu huko nyuma ni wakina nani?na watueleze wamechukuliwa hatua gani kwa uvurundaji huo ambao sio siri haulingani na watu wenye sifa zinazostahili kuwawakilisha wananchi kwenye mikataba ya mali za taifa lao!
 
Personally nafikiri ni sawa anavyofanya Rais Kikwete,ila sijui ni coincidence ama la kwasababu inaonekana kama "ameyafanya mabadiliko hayo under shinikizo flani hivi"Ninachomuomba tu Mh Rais ni kuhakikisha anawafanyia kazi wananchi na sio the other way around,ilo ni mosi,pili asifanye kazi yake kwa interest ya tabaka lolote lile,kwa maana kwamba afanye kazi yake kama kiongozi wa watanzania wote na si wa ccm peke yake,pia asisubiri mashikizo kabla ya kufanya kile anachotakiwa kufanya ambacho ni uongozi bora na usimamiaji madhubuti wa rasilimali za Taifa letu analoliongoza pamoja na kuhakikisha kwamba wananchi wake wananufaika na rasilimali zao.
 
Kada.
Napingana na wewe kwamba wapinzani hawatakuwa na hoja tena baada ya Rais kuunda hiyo tume ya Madini If and only if atatimiza yale anayoyasema.

Lengo la akina Slaa and the rest halikuwa kwamba Rais asichukue Hatua. nadhani alichofanya Rais ni pamoja na kusikia kilio hicho. je unadhani hapo hatutakuwa tumefaidika na hoja za wapinzani sisi kama Taifa? Je kama wangeamua kukaa kimya Leo Jk angefikiri kuunda hiyo Kamati?

Binafsi nitampongeza tena sana iwapo atatekeleza hilo na lisiishie pale Kizota.
 
Hapa Raisi amechemsha tena amechemsha vibaya sana kama tu hivyo alivyonukuliwa ni sahihi,amesema anaunda kamati wakati hitimimisho anaelezea mambo yalivyo au marekebisho,nahisi angesimamisha mikataba yote kutokana na hali ya nchi ilipofikia maana Tanzania sasa hapaeleweki na yeye amezidi kukoroga,kuna kipindi alisema hakuna mikataba mpaka sheria zipitiwe au mikataba hiyo ihakikiwe tena,Tatizo lililopo ni mikataba hii inatafsiriwa vipi na katiba ya Jamhuri ya Muungano,Muungwana ni bora akubali mabadiliko ya Katiba au atangaze nia ya kuifanyia mabadiliko ya KATIBA ili yaendane na wakati,kwa kuunda kamati ni ufisadi mwengine wa kupoteza fedha za walala hoi hapa wanakaribishwa wageni wengine kula feza,hao wanasheria,vyama vya upinzani nafikiri imeonekana ipo haja ya kuwapa chochote ili wasigeuze midomo kuwa mawingu ya mvua kwa kusema sana,ila tuwe na subira kwani wakati ndio utakaotupa jibu sahihi na sio kuunga mkono au kuuvunja.
 
---mawazo ya wana JF yanaanza kuwa implemented
---there is no acknowledgement, but we don't care as long as...
---amefikia kutoa tamko hilo kutokana na mashinikizo mengi
---amefikia kutoa tamko hilo kutokana na kuona chama kinateteleka
---amefikia kutoa tamko hilo na kukubali kuwa kuna makosa
---amekubali kuna makosa hivyo merekebisho yafanyike
---kama kawaida kwenye makosa kuna mkosaji
---kama kawaida nchini mwetu wenye makosa hawawajibishwi
---kama kawaida tamko hili ni sawa tu na mengineyo mengiyo mengi
---matamko ya kurekebisha bila kuwawajibisha wakosaji
---kwa mara nyingine tena wakosaji katika mikataba hawatawajishwa
---kwa mara nyingine tena taifa lilishaingia hasara za kuepukika
---kwa mara nyingine tena hii ni uthibitisho wa kukurupuka
---kama mwalimu alivyosema madini tunge yaacha hatukusikiliza
---kamati ilitakiwa kuwepo kabla ya mikataba kusainiwa
---tutajifunza lini kuwa makini....
---MUNGU IBARIKI TANZANIA.

SteveD.
 
Absolutely stupid! What on earth does he think about the tax payers who had been suffering all this time? The other day he promised to scrutinise all mining contracts and guess what; Karamagi made a bogus contract in London in front of his nose and now he comes with another ngonjera, to hell with his st*******.

He should cancel all mining contracts forthwith as Tanzanians are bleeding and their blood is more worth than another day of these dubious contracts signed by his friends. (Karamagi et al.) When he has taken that action then we can start to talk about the talk.
 
The man he is never sincere na anacheza na siasa ambayo inagusa maisha ya kila mtanzania .JK kama angalikuwa real anagali waambiwa watu wake Bungeni waunde kamati ya Zitto kama alivyotaka . Lakini yeye kwa mawazo alidhani anaujenga Upinzani kama haki ile ingalitolewa .

Ameshindwa kusema kwamba pressure ya Wapinzani imepelekea wahisani kumpa Ultimutam na akaahidi kusema haya kwenye mkutano Dodoma baada ya kumaliza kikao nao .Hii anwapoza hawa jamaa lakini si maamuzi yake yeye na CCM.

Waliodai haki hii ni Wapinzani mana wananchi hawajasikika kokote kwa kuwa hawana platform ta kusemea leo anashindwa kuwa jasiri na kuwapa credit badala yake anamwachia Makamba anarusha matusi mbele ya wageni wao.

Maamuzi yake yanapingaa sana na maneno yao Bungeni .Je do we still need to trust them ?

Swala la mikataba si la kisiasa yeye kalifanya kuwa la siasa .Kuibiwa uchumi wa Nchi is a serious thing na watu kuweka mikataba mibaya hawa hukumu yao si Kizota ama wapi bali Mahakamani.

Poleni sana
 
this just proves the inconsistence of his government! how many times, atawaambia watu this crap about kuunda tume kwa ajili ya mikataba?

he has to get real! ......aunde hizo tume kwanza, then he can announce, sio kuraise hopes za watanzania and then no implementation!

watu wamechoka kusikia maneno matupu ...........let him act first then we will congratulate him!

even though, i will like to congratulate upinzani kwa kufikisha ujumbe kwa serikali kuwa they are a bunch of spinners and ppl need actions
 
Nafikiri viopngozi wetu wangekuwa wanakubali ku-apologize pale wanapofanya makosa wangekuwa wanapata heshima toka kwenye jamii wanayoiongoza. Ubovu wa mikataba hata kipovu anaouona, lakini imemchukua Rais zaidi ya miaka 2 kugundua kuwa kuna tatizo, na je kama alishawahi kuunda tume nyingine ambayo KAramagi alisema imeshapitia mikataba na kutoa mapendekezo--lakini sasa hivi anaona ile tume ilicheza tu, je pesa wa zetu wanazochezea sio ufisadi huo?

I think Mr. Presida is not serious ila ni maneno tu kwani huu wimbo wa siku nyingi na sana sana akiwa kwenye majukwaaa ya siasa ndo anatoaga maneno matamu lakini utelezaji wake ni zero. Kama walitamka kusitisha mikataba mipya mbona Buzwagi wamesign, kuna haja ya ku-track ahadi zake na ku-crosscheck jinsi alivyozigeuka mwenyewe. I am not sure kama uwa anaweka rekodi za mambo aliyoyasema na utekelezaji wake.

I support hii idea ya kuunda tume ambayo ni independent ambayo ni siasa free na yenye kuweka maslahi ya nchi mbele. Memmbers wa tume wafahamike publically, hadidu za rejea ziwe wazi na ipewe muda fulani na report iwe wazi, vinginevyo utakuwa ni wimbo ule ule kuwa mikataba ni siri-na report itakuwa siri.
 
In my opinion, the President is right by admitting failure and deciding to take corrective action. Additionally, I commend his commitment to have a diversified commission to oversee the revision of the past contracts. Weldone JK. Keep it up.
 
Kada, when were you born!? I have been hearing these words since my puberty, i am almost at my 50th birthday; these are the sweet words to somebody like you; they will not change my mind hadi nione huo ukweli uko implemented! Unajua kuna kamati ngapi zimewahi kuundwa tangu Nyerere hadi Muungwana? Kamati na hope! We want to see issues implemented, we 'll know the guy is/was serious when we see things are strait'ned!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom