Rais Kikwete sasa kuunda kamati mpya ya madini

Kwa nini awajumuishe wapinzani ktk kamati, kwani mikataba imeshakua kisiasa. Ni dhahiri CCM wameshakubali kushindwa na kua hawawezi ona au fanya kitu kilicho bora kwa waTZ bila ya kuhusisha wapinzani. Na kama ni hivyo JK na CCM yao nashangaa mpaka leo hawajaona umuhimu wa kuwahusisha wapinzani kubadili katiba ili kupunguza madaraka ya raisi nk kama wapinzani wanavyosema. Katiba mbovu ndio msingi mbaya.
Au hii ni ktk kuwakatia kitumbua kidogo wapinzani ili wawe bubu na kutowajibika kwa wananchi.
JK hana lolote, ingekua kweli angeshafanya tayari. Kasoro za mikataba amezijua sio leo.
Hata hivyo, waliozileta hizo kasoro mbona wameachwa tu utafikiri hamna kilichotokea.
 
Kwa nini awajumuishe wapinzani ktk kamati, kwani ameshaamini ama CCM wameshakubali kushindwa na kua hawawezi ona au fanya kitu kilicho bora bila ya kuhusisha wapinzani. Na kama ni hivyo JK na CCM yao hawajaona umuhimu wa kubadili katiba ili kupunguza madaraka ya raisi nk kama wapinzani wanavyosema. Au hii ni ktk kupunguza tu uwajibikaji wa upinzani kwa kuwakatia kitumbua kidogo ili wawe bubu.
JK hana lolote, ingekua kweli angeshafanya tayari. Kasoro za mikataba amezijua sio leo.

Mimi naona hii ni hatua nzuri kama itatekelezwa. Transparence inatakiwa ili kurudisha imani ya wananchi kwa serikali yao. Watu tunaamini usiri wa kwenye madini, kuna jambo linatendeka. Kama serikali itatuondolea wasiwasi huu kwa vitendo, basi litakuwa jambo zuri. Ninachoomba mimi ni vyama vya upinzani kama mtapewa nafasi ya kupendekeza majina basi msimwache Dr. Khamis ambaye kupitia hii mitandao, mimi najua ni katika Watanzania wachache waliobobea kwenye nyanja hii ya madini.

Inabidi tumfagilie huyu Mtanzania mwenzetu kwa faida ya nchi yetu.
 
Hiyo kamati mpya ya madini itakayoundwa mnategemea itafanya maajabu gani mapya? Mbona mpaka sasa hamna lolote lililofanyika baada ya JK kutoa tamko la kurudishwa kwa nyumba za serikali zilizobinafsishwa kifisadi, mfano mzuri nyumba za maafisa polisi? Fungukeni macho, msishangae baada ya mkutano mkuu mkasikia Carl Peters kaelekea Uswisi then marekani kutafuta sifa zaidi kutoka kwa hao watu wanaomsifia kwamba yeye ni mchapa kazi na mwadilifu, halafu around this time hapo mwakani mkaanza kujilaumu kwa mara nyingine tena kwa kuamini mashairi yake aliyoyatoa kwenye mkutano mkuu.. Tufunguke macho na minds wadanganyika!!!!
 
Rais Kikwete sasa kuunda kamati mpya ya madini
*Itajumuisha wapinzani, wasomi na wataalam wa madini

Na Waandishi Wetu, Dodoma


RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa serikali itaunda kamati ya kutazama upya mikataba na sheria ya madini ambayo itajumuisha pia wanasiasa wa chama tawala na upinzani.


Kamati hiyo itatakiwa kushauri marekebisho ya yanayostahili kufanywa katika mikataba hiyo, ili iweze kuinufaisha zaidi nchi kuliko ilivyo sasa ambapo mikataba mingi inawanufaisha zaidi wawekezaji katika sekta hiyo.


Wengine watakaohusishwa katika kamati hiyo ni wanasheria, wasomi, wachumi, wataalam wa madini.Kamati hiyo itakayoundwa inatarajiwa kutatua matatizo ya kisheria katika mikataba ya madini, jambo ambalo limezua mjadala mkubwa kwa wananchi na wadau mbalimbali wa sekta hiyo.


�Kwa vile jambo limezua mjadala sana na kupelekea watu kudhani kuna kitu serikali inaficha, ni makusudio yangu kuunda kamati pana zaidi ya kutazama upya sheria ya madini na kushauri marekebisho yanayostahili,� alisema.


Rais Kikwete alifafanua pia kuwa, sekta ya madini nchini inakabiliwa na upungufu katika baadhi ya vipengele vya mikataba ya utafutaji na uchimbaji wa madini na ana lengo la kuifanyia marekebisho makubwa ili kuwanufaisha Watanzania badala ya hali ilivyo sasa, ambapo wawekezaji ndiyo wanaonufaika zaidi.


Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, alisema sekta ya madini nchini inakuwa kwa kasi na inayovutia wawekezaji barani Afrika na ina fursa kubwa ya kuchangia zaidi kwenye pato la taifa kwa fedha za kigeni, ingawa hadi sasa mchango wake bado ni mdogo sana ambayo ni sawa na aslimia 1.9.


Alisema kuwa, katika mikataba ya madini kumekuwapo na kipengele cha kumlinda mwekezaji iwapo anapata hasara kwa mtaji kwa kile alichodai kuwa, iwapo atashindwa kufidia gharama zake za uwekezaji hasara hiyo huhamishiwa mwaka unaofuata.


�Mwekezaji hupewa nafuu ya asilimia 15. Maana ya kipengele hicho ni kuwa, mwekezaji atachelewa kuilipa serikali kodi ya mapato na inawezekana

asilipe kabisa katika uhai wa mgodi wake,� alisema Kikwete.


Alisema kuwa pamoja na nia njema ya kuvutia wawekezaji, sheria hiyo ilijali kumlinda mwekezaji asipate hasara na ikasahau kumlinda Mtanzania anayepata hasara ya dhahabu yake inayochukuliwa kwa ajili ya kufidia hasara anayopata.


Alisema kuwa, hoja yake na Watanzania wote ni kuwa lazima mkataba ulinde pande zote mbili zinufaike sawa. Aliongeza kuwa baada ya kulizungumza na baadhi ya makampuni yamekubali kifungu hicho kiondolewe na kubaki na mfumo wa msingi uliopo kwenye sheria.


�Mfumo huo umeainisha wazi haki na wajibu wa mwekezaji. Upande wa wajibu wa mwekezaji anatakiwa kulipa kodi zifuatazo: Kwanza mrabaha wa asilimia

3, pili kodi ya mapato ya asilimia 30,� alisema na kuongeza kuwa kodi hiyo huanza kulipwa baada ya mwekezaji kufidia mtaji aliowekeza.


Alisema kuwa kutokana na hali hiyo alilazimika kupigia kelele kipengele cha nafuu ya ziada ya asilimia 15 ya mtaji kwa mwekezaji, iwapo hakufidia

mtaji aliowekeza katika mwaka husika.


Alisema kuwa kipengele hicho kinazuia na kuchelewesha Tanzania kupata kodi ama kinaweza kusababisha tukose kodi hiyo kabisa na kwamba sasa Tanzania

inapata kodi hiyo.


Alisema kuwa mgodi unapoanza kutoa gawio kwa wenye hisa, gawio hutozwa kodi ya aslimia 10 na makampuni ya madini hutakiwa kulipa kodi ya huduma za kiufundi ya asilimia 5 na kodi ya asilimia 15 ya gharama za menejimenti.


Rais Kikwete alisema kuwa kimsingi makampuni pia yanapewa nafuu ya kutokulipa ushuru wa mitambo inayoingia nchini sanjari na mahitaji ya uwekezaji kutoka nje.


�Huo ndiyo mfumo wa kodi katika mikataba ya madini. Mfumo huo ndiyo unatumika kwa kila mwekezaji wa madini. Hakuna mazungumzo wala maelewano maalum baina ya mwekezaji na Afisa wa Serikali awe Waziri, Katibu Mkuu, Kamishina au Mwanasheria Mkuu wa Serikali au Kamati ya majadiliano ya serikali.


Katika mazingira haya, kama tunapata hasara, siyo kwa hila ya mtu, bali itakuwa kwa sababu ya mfumo uliopo kwa mujibu wa sheria,� alisema Kikwete.


Alisema kuwa baada ya kubaini mapungufu kupitia kamati iliyoundwa, tayari maeneo yenye mapungufu yameainishwa na kufanyiwa marekebisho hususani katika kifungu kinachomlinda mwekezaji, bila kujali mwenye rasilimali.


Rais Kikwete alisema kuwa serikali pia inajenga uwezo wa uhakiki wa mitaji inayowekezwa na shughuli zinazofanywa na makampuni ya madini, nia ni kuwa

na uwezo wa kuhakiki taarifa za kampuni kuhusu uwekezaji na shughuli zao.


Juu ya mapambano dhidi ya rushwa Mwenyekiti huyo wa CCM, alisema kuwa katika kuhakikisha kunakuwa na mafanikio katika vita hiyo, Bunge limetunga sheria mpya mwezi Februari mwaka huu na hivyo kupanua wigo wa vitendo vya rushwa tofauti na ilivyokuwa siku za nyuma.


Alisema kuwa sheria hiyo imeongeza adhabu kwa wahalifu ikiwa ni pamoja na kufilisiwa mali ya mtu aliyekutwa na makosa ya rushwa, sanjari na hilo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa imeimarishwa.


Alidai kuwa taasisi inayo uhuru kamili wa kufanya kazi zake bila kuingiliwa na mtu yeyote na pia ina mamlaka ya kufikisha mashauri mahakamani tofauti na ilivyokuwa zamani.


Alisema kuwa taasisi hiyo inayopambana na rushwa ina mtandao mpana zaidi ikiwa na ofisi katika wilaya 113, pia imaejiri watumishi wapya 396 na utaratibu wa mafunzo umeimarishwa kwa ajili ya watumishi wake ndani na nje ya nchi.


�Nimewaahidi kuwa mimi sitawatisha wala kuwaingilia ili wasimwogope mtu yeyote�.sasa wanaendesha kesi 246 mahakamani. Hata makada wa chama tawala ni miongoni mwa watuhumiwa, pia wanaendelea na tuhuma 38 za watumishi wa umma wenye mali nyingi zisizolingana na kipato chao.�


Mimi napenda kuuliza kama uamuzi huu wa leo unakuja baada ya kupitia mikataba ama kauli ya mwanzo haikuwahi kufanya kazi ?

Baada ya kusoma paragraphs za mwishoni mwishoni naona ni bora tujiulize ni nini maana ya rushwa; Kulingana na kamusi ya kiswahili, neno RUSHWA lina maana ya kupata kisichokustahili kwa namna isiyostahili.

Kila mmoja, including yeye JK, anaelewa kwamba rais mstaafu (Mkapa) alipata mali nyingi asiyostahili kwa namna isiyostahili. Je tujiulize, kabla hajatoa maelezo yake haya mkutanoni dodoma, je alifanya nini kuhakikisha kwamba mla rushwa huyu maarufu anafilisiwa? Maana kuna data zilizotolewa hadharani kuhusiana na upatikanaji mali kwa namna isivyostahili kwa rais wetu mstaafu, ila nothing has been done mpaka leo. Yeye kama Rais ana executive powers za kuamuru Mkapa atiwe ndani kwa kulihujumu taifa. Has he executed his powers yet? What makes him asite kuzichukua hizo hatua?

Mimi nachukulia hotuba hii ni kama ngonjera tu... Tusiamini sana maneno haya ili tusije kujilaumu mwaka kesho wakati tunahakiki aliyoyasema dodoma...
 
Ninachoweza kusema kutokana na hali halisi hapa Dodoma ni kwamba Ukumbi ulijaa alio waita marafiki na watani zake wa jadi akiwa na maana wapinzani.Pia kumbuka mkutano na wafdhili umeisha juzi jana wakawa na mkutano amepewa masharti swala la madini likiwa limeshika moto. Ndiyo maana tamko limekuja ili apate sifa kwa wale wageni marafiki zao CCM. Issue ya madini haikupashwa kuwa namna hii . Hebu tujiulize leo hii Mbunge wa Upinzani akiingia wizara fulani kuomba data anapewa kirahisi ?Iweje leo mdhani kwamba CCM watatoa ushirikiano kwenye kamati hiyo ? Je kwa nini aunde kamati badala ya kuitikia wito wa Slaa wa kuundwa Kamati kule Bungeni au mwito wa Zitto?
 
sitaki kukubaliana na kuundwa kwa kamati..
kwanza nataka muungwana,EL,NK Watuambie zile dola mil. 20 walizopewa na Barick,ni zao au ni zetu,
Mrisho ametumia hoja nyepesi kuwanyamazisha wapinzani na wanaharakati..anadhani wao watoto,anataka kuwapa pipi<ujumbe wa kamati> ili wanyamaze..hoja ya wapinzani na wanaharakati ni kuundwa kamati huru ya kuchunguza mikataba ya madini haswa mkataba wa BUZWAGI,
napendekeza mwanakijiji,lissu na mtikila wawemo
 
Unajuwa kuna kitu kinaitwa nia Njema.lakini kuwa na nia njema pekee hakubadili kitu, vitendo sahihi vinatakiwa vifuatie hiyo nia njema

Kuwa na nia njema pekee haitoshi kulikabili suala.
Namna na mbinu ya kulitafutia ufumbuzi ni jambo la msingi sambamba na hiyo nia njema.

Katika hili suala la madini pia haitoshi kuwa na nia njema pekee ya kulitafutia ufumbuzi.
Suala linalo matter baada ya hiyo nia njema ni kwamba kwa kupitia kamati hiyo itakayoundwa je kuna mkakati gani mathubuti wa kuhakikisha suala la madini yetu linatafutiwa ufumbuzi?.


Yaani hiyo kamati itafanya nini hasa ndilo jambo la msingi la kukazania,

Unaweza ukawa na kamati hata saba kama kamati za harusi, lakini iwapo mipango ni mibovu tegemea hamna chochote kitakachofanikiwa.
 
Maoni yangu binafsi kuhusu kauli ya Kikwete ya Kujumuisha Wapinzani na Wasomi kwenye Kamati ya Kupitia Mikataba ya Madini:

Kauli ya Kikwete imedhirisha wazi hoja ambazo wapinzani tumukuwa tukisimamia zilikuwa ni sahihi tofauti na baadhi ya mawaziri na viongozi wengine wa chama chake walivyokuwa wakipita mikoani kubeza. Aidha kauli hii ya kukiriri mapungufu imedhirisha wazi umuhimu wa upinzani katika taifa kwa maana ya kukosoa na kutoa fikra mbadala ambazo zinapotekelezwa basi zinaleta maslahi kwa taifa kwa ujumla bila kujali itikadi.

Hata hivyo, Rais katika kukiri mapungufu hayo ametumia muda mwingi sana kujitetea kueleza kwamba tayari mabadiliko ya msingi yamekwishaanza kufanyika kitu ambacho si sahihi na itakwaza wigo wa kamati husika kubainisha mapungufu ya msingi. Bado tunasafari ndefu katika kuhakikisha rasilimali za taifa zinawanufaisha watanzania walio wengi.

Kauli ya Kikwete inadhirisha umakini wa hoja aliyoiibua Mbunge Zitto Kabwe ya kutaka kuundwa kwa kamati teule, Wabunge wa CCM wakaikataa lakini leo Mwenyekiti wao wa chama anaeleza wazi nia yake ya kuhakikisha inaundwa kamati inayojumuisha makundi mbalimbali ya kijamii ikiwemo wasomi na wapinzani.

Kuundwa kwa kamati ni suala moja tu, suala la msingi ni maoni ya wadau na wananchi kusikilizwa katika kamati hiyo, maana uzoefu unaonyesha zipo kamati za kiserikali ambazo ziliundwa lakini zikatoka na misimamo ya kiserikali badala ya kuwa na misimamo huru itakanayo na maoni ya wananchi waliowengi. Pia zipo kamati nyingi ambazo zimewahi kuundwa huko nyuma na kutoka na maoni mazuri lakini yakaishia kwenye makabati. Kwa mfano, katika sekta hii hii ya madini zipo Tume zilizowahi kuundwa mathalani tume ya Kipokola ambayo ilikuja na maoni mazuri tu lakini sehemu kubwa hayajatekelezwa. Hata katika sekta ya Mafuta iliundwa Tume ya Mboma ambayo ilitoka na matokeo mazuri tu lakini hayajatekelezwa kwa upana wake. Kinachokosekana ni dhamira ya kisiasa ya kutekeleza maoni ya wananchi. Rais Kikwete alisema toka Mwezi Disemba, 2005 katika hotuba yake ya kufungua bunge, leo takribani miaka miwili imekaribia bado mabadiliko ya kisheria hayajafanyika, pamoja na hoja hii kuwemo tayari kwenye ripoti za kamati mbalimbali. Ikumbukwe kwamba hapa katikati kumeletwa sheria nyingi sana za kufanyiwa marekebisho makubwa, ni vipi sheria ya madini hailetwi?

Rais Kikwete anazungumza kwamba Kamati hii itatumwa nje ya nchi kwenda kujifunza zaidi, huku ni kuendelea kutumia muda zaidi na fedha za walipa kodi na kuchelewesha kuchukua hatua katika jambo ambalo linafahamika tayari. Wataalamu wa Tanzania wenye ujuzi na masuala ya madini pamoja na wanasiasa wenye maono katika sekta hii wapo tayari na wengine wameshatoa maoni yao, vipi hatua zisichukuliwe?

Hata Rais Kikwete mwenyewe ameshakwenda nchi mbalimbali na kupata uzoefu. Alikwenda Botswana akasema anafurahia jinsi nchi hiyo inavyonufaika na rasilimali akatangaza kabisa kwamba angependa Tanzania iwe kama Botswana. Alienda pia Afrika Kusini akasema pia amepata uzoefu. Inawezekana kinachokosekana ni hatua za kisiasa tu za kuchukua hatua. Na hii ni dhahiri kutokana na ukigeugeu wa kauli za viongozi kuhusu sekta hii, tukumbuke ni Rais Kikwete huyu huyu alisema wakati akizungumza na watanzania waishio uingereza kwamba mrabaha wa asilimia tatu katika dhahabu ni worldwide standard; hivyo watanzania tusilalamikie suala la royalty.

Pia Rais amekwepa kabisa hoja ya ufisadi katika uungiwaji wa mikataba ya madini kwa maneno yake amesema “kama tunapata hasara, siyo kwa hila ya mtu, bali itakuwa kwa sababu ya mfumo uliopo kwa mujibu wa sheria”. Rais amekwepa kabisa kujiuliza ni kwa vipi viongozi wetu hali wakijua wanaliingiza taifa katika mikataba ya isiyolinda maslahi ya taifa, hapa kuna mazingira ya ufisadi. Ni utamaduni ule ule wa kutazama mbele, kulindana, kukwepa kuwajibisha waliohusika na mikataba mibovu na kukwepa hoja za msingi.

Hivyo, hoja ya Rais kutaka kamati ya kupitia mikataba ijumuishe wapinzani isitumike kabisa wala isitafsiriwe kwamba imeondoa hoja yetu ya msingi ya kutaka kuundwa Tume Huru ya Kuchunguza ufisadi ikiwemo katika Sekta ya Madini. Hoja hii inamsingi wake kwa kuwa ziko taarifa za kuaminika kuwa baaadhi ya vigogo serikalini wana hisa katika makampuni haya ya madini- katika mazingira haya ni wazi kuwa baadhi ya maamuzi ya kusaini mikataba hii yanafanyika kwa hila, na mianya ya kisheria inatumika tu kuhalalisha hila hizo. Ni vyema watanzania wakarejea pia katika Orodha ya Mafisadi(list of shame) iliyotolewa na Dr Slaa na ushirikiano wa Vyama vya Upinzani kujua asili ya mikataba yetu mingi.


Kauli hii ya Kikwete isiwapumbaze watanzania na kuzima mjadala wa kitaifa unaoendelea hivi sasa kuhusu hatma ya madini yetu na rasilimali nyingine za taifa. Kuundwa kwa tume yenye wadau mbalimbali ni hatua moja tu; cha msingi ni kuendeleza mjadala na harakati za nguvu ya umma katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha kila jamii iliyoko katika maeneo yenye rasilimali inanufaika na rasilimali hizo. Masuala ya msingi ya kujadili katika sekta ya madini ni pamoja na umiliki wa watanzania katika migodi; kuboresha mifumo ya ukaguzi kujua kiwango cha madini kinachopatikana; madini kuongezewa thamani(processing) ndani ya nchi; muunganiko wa kisekta(forward and back ward linkage) ili kupanua ajira; kodi na kuhakikisha mzunguko mkubwa wa kwenye fedha zinazotokana na madini unakuwa ndani ya nchi yetu. Mapato yetu ya madini ni madogo na mchango wa madini katika pato la Taifa ni mdogo kutokana na mianya iliyopo, kama mianya hii ikizibwa ni wazi kwamba Madini yakachangia kuboresha sekta zingine hususani kilimo na elimu hatimaye na hivyo kuharakisha kasi ya kuleta maendeleo. Ipo mifano mingi ya nchi duniani ambazo kwa kutumia madini ama nchi nyingine kwa kutumia mafuta, sekta zingine na uchumi mpana wa mataifa hayo umeweza kuendelezwa.
 
Kwa muda sasa hivi nimekuwa nikijaribu kuutazama mfumo wa kisiasa nchini na utekelezaji wake ili kupata kina cha mzizi wa matatizo yetu (uwekeshaji nchini) unatokana na kitu gani.
Nadhani la msingi hapa sio kuwepo kwa kamati bali madaraka yanayoshikiliwa na baadhi viongozi hasa rais na Mawaziri wenyewe. Katiba imewapa watu hawa madaraka makubwa sana kiasi kwamba wanaweza kusimamisha maamuzi yoyote ya Kitaalam na kuchukua njia za mkato kwa sababu zao binafsi.
Tumeyaona haya ktk mikataba yote toka NBC wakati wa Mkapa hadi majuzi ktk wa Richmond ambapo KIGOGO fulani amekuwa mtoa jibu la mwisho ktk uwekaji mkataba. Rais ama Waziri wana uwezo wa kutumia simu tu kuhakikisha mwekeshaji fulani amepata tender ama kibali fulani bila kutoa maelezo kimaandishi ambayo yatakubaliana na yale ya wataalam. Mkataba wa Buzwagi tumeona mkono wa Karamagi tu...mwanasiasa ambaye alishiriki ktk kutunga policy za madini kisha ndiye tena tunamkuta ktk kuweka mikataba na kuchagua nani apewe mkataba huo.. This is too much Power kwa mtu mmoja.
Tazama swala la Mkapa ni katiba imemlinda kwanza kabla hata hatujafikiria kuwepo kwa kamati na kibaya zaidi ni pale Rais JK aliposema mwacheni Mzee wa watu astaafu' -Hapa tumefunga ukurasa wa hoja yeyote kutokana na nguvu za hawa watu.
Kwa hiyo Kikwete anaweza toa ahadi 100 na kuweka kamati za kila aina lakini muhimu ni kutazama nguvu za hawa viongozi wetu ktk maswala ya kitaifa.
Binafsi naamini kabisa kwamba maamuzi ya mwisho ktk maswala yoyote ya uwekeshaji nchini yafanywe na kamati ya Wataalam ktk fani hiyo. No politicians at all ktk utekelezaji wa uwekeaji mikataba hii ila Policies za uwekeshaji zitajengwa na wanasiasa.
Kwa hiyo tutakapo weza kuondoa mikono ya vigogo wanasiasa ktk maamuzi muhimu kati ya kampuni inayowekesha na Wataalam wetu itabadilisha kabisa mfumo mzima wa maslahi ya nchi. Wanasiasa wetu wataweka mikataba ya kitaifa na wanasiasa wenzao toka nchi za nje na pengine kupendekeza kimaandishi kampuni fulani lakini hasipewe nafasi kabisa ya Karamagi kuweka mkataba Hotelini London na kudaiwa kuwa sio kosa.

Mwisho nitaendelea kupinga swala ama matumizi ya mali za Kitaifa kama vile ni mali ya makampuni binafsi. Ninapinga waziri kwenda weka mkataba London Hotelini na kudai ati hakuvunja sheria ni jambo la kawaida huku akifananisha sheria za Makampuni na sheria za nchi (katiba).
Ni marufuku nyaraka zozote za kitaifa ama serikali kutolewa barabarabani.. Passport, hati za kumiliki ardhi ama nyaraka yoyote ile ya kiserikali sio hruhusa kuipatia mtaani ila ofisi ya serikali tofauti kabisa na kitambulisho cha kampuni ama nyaraka zozote za kampuni binafsi ambazo unaweza kuzipata mahala popote maadam shirika lenyewe linaafikiana na sheria za mahala hapo.
Siku hizi kuna ma meli makubwa ya kifahari Crusership ambayo hutia nanga katikati ya bahari zetu - No mansland kuwakutanisha wafanya biashara wa makampuni ili kuweka mikataba nje ya sheria za nchi yeyote ile. Meli hizi zinapigwa vita lakini imeshindikana kwa sababu wametinga nje ya mipaka ya nchi yeyote, leo hii sisi tunakuja weka mkataba wa Kitaifa London tukidai kuwa ni jambo la kawaida. Then next Karamagi mwingine waziri wa mambo ya ndania atakuja gawa Passport nyumbani kwake achilia mbaya nchi ya nje hotelini na mihuri ya serikali mkobani.

Kwa hiyo, kamati inahitajika sasa kwa sababu ya madai ya Zitto basi -kaput. Isije kuwa tunaunda kamati ili kutatua matatizo ya baadaye wakati pakacha zima zimesha oza. Haya yatakuwa makosa makubwa ya JK kwani hatuhitaji kamati kwa kila kitu - Bunge litatazama mikataba na kuikubali kulingana na policy yetu ktk kodi, asilimia ya ubia na umilikikaji kisha wataalam watachagua nani apewe hiyo tender ama mwekeshaji mzuri atapatikana vipi. hapo hakuna mkono wa rais ama waziri unless swala zima zinaingiliana na msimamo wetu ktk siasa.
.
Naomba kuwakilishga!
 
In my opinion, the President is right by admitting failure and deciding to take corrective action. Additionally, I commend his commitment to have a diversified commission to oversee the revision of the past contracts. Weldone JK. Keep it up.

lakini watu wanamponda ! ama kweli hakuna jema atakalofanya akiwa ofisini watu wakaona ni jema kwao !

kweli hiyo ni siasa, lakini akitoka ofisini wapinzani hao hao watamsifia kweli kwa kuadmit makosa na kuyarekebisha !
 
Hii makinikia ilianza mbali.....


Angalau saivi kila mtu atapewa Noah yake...Asante JPM...


sema tu sijajua hizo Noah zinakuja lini...
 
Duh tuliyazungumza haya miaka 10 iliyopita!, hii ya makinikia imekua kama saa, mshale umezunguuka then baada ya miaka kumi umerudi palepale!
 
Back
Top Bottom