Rais Kikwete punguza safari za nje

sweetlady

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
16,947
8,409
Tumepata kuandika na leo tunaandika tena tukimsisitiza Rais Jakaya Kikwete na washauri wake kupunguza safari za nje ya nchi kikazi wakati taifa likiwa kwenye hali tete.

Licha ya misafara yake kulalamikiwa ndani na nje ya nchi kwa sababu ya kuongozana na msururu wa watendaji ambao wengine hawana umuhimu, safari hizo hazizingatii utulivu wa nchi.

Ni mara kadhaa wananchi wamewahi kuhoji majukumu ya rais na wasaidizi wake kwa sababu sio lazima kila safari nje ya nchi anatakiwa aende, ndiyo maana wapo wasaidizi wake katika ngazi mbalimbali ambao wanaweza kumwakilisha. Pamoja na ushauri tunaompa rais kupitia vyombo vya habari hususani magazeti, watendaji wake huibuka na kumjibia kwamba safari hizo zina tija hivyo lazima asafiri, wanasahau kwamba wasaidizi wanaweza kwenda ili rais abaki nchini kumaliza kero za waliomwajiri kupitia sanduku la kura.

Tunafahamu kwamba nyingi ya safari hizo ni kutembeza bakuli kuomba msaada ambao hana muda wa kufuatilia matumizi ya fedha hizo kwa sababu anakuwa nje ya nchi. Kwetu tutaendelea kulisema tukiamini ipo siku rais Kikwete ataona umuhimu wetu japo atakuwa amechelewa.

Wataalamu wanasema msafara wa watu 20 ambayo ni idadi ya kawaida kwa msafara wa rais Kikwete hasa anapokwenda nje ya nchi wastani wa matumizi kwa siku huweza kufikia dola 15'000 za maarekani ambazo ni zaidi ya sh milioni 20.

Sasa gharama hiyo ni kwa siku, wakati mwingine ziara zake huchukua hadi siku 10 au zaidi na idadi ya wasindikizaji huweza kuongezeka hadi kufikia 40; tutafakari ni kiasi gani taifa linapoteza fedha nyingi pasi na sababu za lazima? Takwimu zinaonyesha mpaka sasa rais na wapambe wake wamesafiri zaidi ya mara 320 tangu aingie madarakani Desemba mwaka 2005 tukisema kila safari amekaa huko kwa siku tano, tunaona jinsi Taifa letu linavyotiwa umaskini na wachache wanaozunguka meza ya rais.

Tunaamini kwamba matatizo yanayotokea hivi sasa kama mauaji ya raia kule Songea, migogoro kwenye Bodi ya Pamba, mfumko wa bei unaosababisha kuyumba kwa uchumi wetu, migomo ya walimu wanaodai marupurupu, madaktari na mengine mengi angeweza kuyasimamia kwa karibu zaidi na kuyamaliza.

Alipata kunena aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Hayati Daudi Balalli akiishauri serikali kuacha kuwa omba omba badala yake tutangulize uzalendo kwa kulinda maliasili.

Source: Tanzania Daima - Jumanne julai 17,2012
 
sweetlady leo umeingia kwenye siasa
huku unaweza jikuta unapigwa ban bure bora twende kwenye jukwa letu la chit chat bana
Maana huchelewi kukasirika na kujikuta umetukana
 
Last edited by a moderator:
Eti anaenda kuemea!!!!!!!!!!!na cha ajabu zaidi anayekupa misaada anapanda daladala,anayeenda kuomba anakwenda na taxi.
 
nyie watu ni bora kumuomba mchungaji asihubiri siku ya jumapili kuliko kumwomba JK asisafiri
 
Hiv hili swala halipo mahakamani kweli? Maana naogopa kuchangia nisije nikaingilia uhuru wa mahakama!
 
Muhimu hapo ni kwamba apunguze safari ili kuokoa pesa za walipa kodi. Kimsingi suala la yeye kuwepo au kutokuwepo halizuii shughuli za serikali kufanyika, labda kusaini miswada (kuwa sheria) na kusaini wafungwa wa murder wanyongwe ndo kutamsubiria
 
Hivi kati ya Kikwete na Membe nani anasafiri zaidi kumshinda mwenzake?


Kikwete atakuwa anasafiri zaidi kuliko Membe.....mimi huwa nahisi wakati mwingine anamwomba Membe apumzike yeye aende badala yake!
 
Muhimu hapo ni kwamba apunguze safari ili kuokoa pesa za walipa kodi. Kimsingi suala la yeye kuwepo au kutokuwepo halizuii shughuli za serikali kufanyika, labda kusaini miswada (kuwa sheria) na kusaini wafungwa wa murder wanyongwe ndo kutamsubiria

Haswaaa wala hujakosea hapo red.....ndio mana tunamwomba apunguze safari manake zina gharimu vinginevyo afute wizara ya mambo ya nje manake ni kama vile haina kazi!
 
Kumbe majibu yapo!
Kwani huyu mhariri anataka nani aende kutembeza hilo bakuli kama si mkulu wa kaya..!

Kutembeza gani bakuli kila siku?.......hatukatai kuwa JK ni omba omba ila basi ifike mahali akishatembeza bakuli apumzike aangalie kama bakuli aliloleta limefanya yale aliyokusudia.....huoni kama hizo safari zake zinamaliza hata hilo bakuli?
 
Aibu kwa Taifa km hili kuomba

Yaani ni zaidi ya aibu......rasilimali tulizonazo tunawapa wageni wanaondoka nazo afu sie tunapeleka bakuli.....nahisi watakuwa wanatucheka sana ila ndiyo kama hivyo ukila na kipofu usimshike mkono!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom