Rais Kikwete na ziara ya kwanza Jijini Mwanza baada ya uchaguzi

Sasa Rais Jakaya Kikwete ameondoka Ikulu ndogo Capri-Point na kuelekea Usagara ambako atakuwa na waziri Magufuli katika uzinduzi wa barabara ya Mwanza Usagara hadi Geita.

Nafuatilia nini kitajiri baina yake na Magufuli.....!
 
Magazeti ya Leo na Ziara ya JK Mwanza.

JK – Nitaunda chombo kupambana na dawa za kulevya

Na Mwandishi wetu
30th May 2011


Rais Jakaya Kikwete, ametangaza kuwa ataunda chombo maalum cha kupambana na ongezeko kubwa la tatizo kubwa la biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini.

Aidha, Rais Kikwete amewaomba viongozi wa dini na taasisi za dini nchini kusaidiana na Serikali katika kupambana na tatizo hilo lenye madhara makubwa kwa jamii, na hasa miongoni mwa vijana ambao wanaunda asilimia 60 hadi 80 ya Watanzania wanaotumia dawa za kulevya ambazo zinaharibu mwili na akili ya mtumiaji.

Vile vile, Rais amesema kuwa wakati ni kweli kuwa mikoa yote ya Tanzania inakabiliwa na tatizo hilo, lakini ni mikoa saba inayoongoza kwa kuwa na tatizo kubwa zaidi ikiwa ni Dar es Salaam, Mwanza, Mjini Magharibi – Zanzibar, Arusha, Tanga, Mbeya na Dodoma.

Rais Kikwete alitangaza kusudio lake la kuunda chombo maalum cha kupambana na dawa za kulevya jana wakati wa sherehe za kusimikwa kwa Askofu Mteule Albert Jella Randa wa Kanisa la Mennonite, Tanzania, kuwa Askofu wa Dayosisi ya Mwanza ambako alikuwa mgeni.

Sherehe hizo zilifanyika kwenye makao ya Dayosisi hiyo Nyakato, mjini Mwanza.

Akihutubia mamia ya waumini wa Kanisa hilo pamoja na wananchi wengine waliohudhuria sherehe hizo, Rais Kikwete amewaomba viongozi wa dini, madhehebu ya dini mbali mbali nchini kuongeza juhudi za kupambana na biashara na matumizi ya dawa za kulevya.

Akisema kuwa pamoja na kwamba matunda ya juhudi za Serikali katika kupambana na tatizo hilo yameanza kuonekana bado kazi iliyoko mbele ya jamii ya Tanzania ni “kubwa sana”.

“Mwaka jana, 2010, watu 12,119 walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya. Katika kipindi hicho, dawa za kulevya zilizokamatwa ni heroine kilo 190 na gramu 780, cocaine kilo 65, morphine kilo 11, bangi kilo 279,520 na mirungi kilo 10,317. Takwimu zinaonyesha kuwa mkoani Mwanza tatizo linakua kwa kasi sana,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:

“Dawa za kulevya zina madhara makubwa kwa watumiaji na kwa jamii. Kwa watumiaji hatima yake ni mtu kuharibikiwa kimwili na kiakili. Watu huwa mazezeta na hivyo kushindwa kutokuwa na manufaa kwa jamii. Hii ni hasara kwa familia, jamii na taifa. Bahati mbaya sana waathirika wengi ni vijana. Tafiti zilizopo zinaonyesha kwamba asilimia 60-80 ya watu wanaotumia dawa hizo ni vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 30, alisema.”

Aliongeza: “Hii ni hasara kubwa kwani vijana ndio nguvukazi ya leo na kesho. Ndiyo roho ya taifa na warithi wa familia, jamii na taifa. Wakiharibikiwa taifa letu litaangamia. Tusikubali. Ni wajibu wa kila mmoja wetu kulichukia tatizo hili na kulikemea kwa nguvu zake zote ili kuokoa taifa letu. Nawaomba viongozi wa dini kushirikiana na Serikali na watu wote wenye mapenzi wa nchi yetu kupambana mpaka tufanikiwe kudhibiti na hatimaye kulitokomeza tatizo hili.”

Sherehe za leo za kusimikwa Askofu Randa (50) kuwa Askofu wa Kanisa Mennonite, Jimbo la Mwanza, pia zilihudhuriwa na mamia kwa mamia ya waumini wa Kanisa hilo na wananchi wengine.

Kwenye sherehe hizo, Askofu Mkuu wa Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT), Mhashamu Severin Watson Mang’ana amemkabidhi askofu huyo mpya nguvu kuu ishara za mamlaka na madaraka ya uaskofu ikiwamo Biblia, Katiba ya KMT, Cheti cha Uaskofu na vitabu vya taratibu ya kuendesha ibada za Kanisa hilo na nyimbo.

Kanisa la Mennonite lililoanzishwa duniani mwaka 525 na Mchungaji Menno Simon mjini Zurich, Uswisi, liliingia nchini miaka 77 iliyopita mwaka 1934 na liko katika maeneo yote ya Tanzania isipokuwa Zanzibar, Ruvuma na Pwani. Kanisa hilo lina makao yake mkoani Mara.

SOURCE: NIPASHE.

=======================================

Askofu: Viongozi wasio waadilifu wajiondoe serikalini

Sheilla Sezzy,Mwanza

MWENYEKITI wa Baraza la Maskofu wa Kanisa la Mennonite Tanzania, Askofu Stephan Mang'ana amewataka viongozi wasio waadilifu kujiondoa ndani ya Serikali ambao siyo waadilifu kujiondoa katika nafasi zao za uongozi.

Askofu Mang'ana yasema hayo jana jijini Mwanza alipokuwa akihubiria katika ibada ya kumsimika Askofu Mteule Albert Jella Randa, sherehe zilizohudhuriwa pia na Rais Jakaya Kikwete ambaye ni mara yake ya kwanza kufika mkoani Mwanza tangu alipochaguliwa kuliongoza taifa kwa awamu ya pili.


Kiongozi huyo wa kanisa alidai kuwa hakuna haja kwa kiongonzi kung'ang'ania madarakani wakati hana uwezo wa kuongoza huku akimtwisha Rais Kikwete mzigo wa malalamiko ya wananchi ambao sio wake.


“Nawahesimuni sana viongozi wetu, lakini kwa hili mtanisamehe. Nawaombeni mtoke kwa sababbu mmeshindwa kuwatumikia wananchi waliowapatieni dhama ya kuwa viongozi na badala yake mnaonekana majimboni kwenu wakati wa kuenda kuomba kura”alisema Mangana.


Akizugumzia sifa za kiongozi askofu huyo alisema kuwa kiongozi anapaswa kufahamu matatizo wanayopata wananchi na kuwa mstari wa mbele kuyatafutia ufumbuzi.


Alisema kuwa kiongozi anapaswa kuelewa alama za nyakati ili kuondoa matabaka katika jamii ambayo imekuwa ikihangaika bila ya kujua hatima ya maisha yao ikibakia na maswali yasiyo na majibu kutokana na ugumu wa maisha.


Askofu Mang'ana alisema kuwa ni muhimu kwa kiongozi kujitoa kafara kwa kundi la watu anaowaongoza huku akitoa mfano wa Mussa katika Biblia alipokuwa akiwaongoza wana wa Israel.


“Mabadiliko ya kijamii yatatokea endapo viongozi wetu wataacha ubinafsi na kuitumikia jamii yao ikiwa pamoja na kukabilina na changamoto katika sehemu anayoongaza,”alisema Mangana.


Alisema kuwa kama ilivyokuwa kwa Mussa aliyepiga magoti mbele ya Mungu wake na kumwambia kuwa hana sauti juu ya watu anaowaongoza kwa kuwa ana mdomo mzito, basi iwe hivyo kwa viongozi kurudi kwa Rais Kikwete aliyewateua na kumwambia majukumu aliyowapa hawayawezi.


Askofu huyo alionyesha kusikitishwa na jinsi rasilimali za nchi zinavyoteketea kutokana na usimamizi mbaya wa viongozi walio madarakani na migomo inayotokea kila mara.


“Tanzania haikupaswa kuwa na migomo, badala yake watu wanaweza kukaa mezani na kusuluhisha matatizo yao. Nasikitika kuona mtoto mdogo yupo katikakati ya maandamano na bango kubwa tunawafundisha nini watoto wetu?,”alihoji askofu huyo.


Alimwomba askofu mteule Randa kuwa mtumishi wa wananchi badala ya kuwa kiongozi wa wananchi na kuwa mstari wa mbele katika kuliongoza kanisa.


Kwa upande wake, Rais Kikwete alisema kuwa Serikali imetenga Sh70 bilioni kwa ajili ya ruzuku kwa hospitali za taasisi za kidini ili ziweze kutoa huduma nzuri kwa jamii na kudumisha uhusiano wao na serikali.


Alisema kuwa madhehebu ya dini yanatoa mchango mkubwa kwa jamii na taifa kwa kuchangia katika kutoa elimu na huduma za kiafya akisema kuwa yeye pamoja na viongozi wenzake wanaheshimu mchango wa taasisi hizo za kidini.


Akitoa taarifa kuhusu dawa za kulevya nchini, Rais Kikwete iliziomba taasisi za dini kuongeza juhudi katika kukemea tatizo hilo huku akibainisha kuwa mkoa wa Mwanza unaongoza kwa kuwa na watumiaji na wauzaji wa dawa hizo huku mkoa wa Mara ukiongoza kwa kulima bangi.


Alisema katika kipindi cha mwaka 2010, kilo 12,196 za dawa hizo zilikamatwa huku Mkoa wa Mwanza ukiongoza kwa kukamata kilo 268 na kuongeza kuwa wanaothirika ni vijana wenye umri wa miaka 15-30 ambao ni nguvu ya taifa.


Rais Kikwete aliwaasa Watanzania kuwa macho na watu wenye lengo la kuvuruga amani ya nchi kwa madai kuwa watu hao hawapo tayari kuona Tanzania ikiwa na amani wakati kwao kuna machafuko.


SOURCE: MWANANCHI
=======================================

Askofu amtaka Kikwete kutowavumilia wazembe


Imeandikwa na Nashon Kennedy, Mwanza;
30th May 2011

MWENYEKITI wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT), Askofu Steven Mang’ana amemtaka Rais Jakaya Kikwete kutokuwa tayari kuwavumilia viongozi wazembe serikalini ambao hawatekelezi na kutimiza wajibu wao kwa wananchi.

Askofu Mang’ana aliyasema hayo jijini hapa wakati wa sherehe za kusimikwa kwa Askofu Mteule Albert Randa kuwa Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mwanza, ambazo Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi.

Alisema ifike wakati kila mtendaji serikalini aone kuwa ana jukumu kubwa la kutanguliza uzalendo na mapenzi ya nchi yake kwa kutumia nafasi aliyonayo, ashughulike na changamoto lukuki zinazowakabili wananchi, zikiwemo zile za huduma muhimu za kijamii.

Alisema wapo viongozi walioteuliwa na Rais katika nafasi nyeti serikalini, lakini utendaji wake umekuwa sio wa kuridhisha na kumtaka Rais Kikwete achukue hatua mara moja za kuwawajibisha.

“Mheshimiwa Rais anamteua mtu kushika nafasi nyeti serikalini na badala ya yeye kuwajibika na kumsaidia, anabaki kucheza tu, Rais nakuomba uwaondoe viongozi wa aina hii…wapo wengi na wenye uwezo wa kufanya kazi, viongozi wa aina hii hawakusaidii,” alisema.

Aliwataka viongozi wa madhehebu ya dini kutokuwa mahiri katika kukosoa serikali, bali waipe ushirikiano wa kutosha.

“Viongozi wa dini msiwe wepesi katika kuilaumu na kuikosoa serikali, tambueni kuwa Mungu anawapeni nafasi hiyo ili kusaidia taifa letu na Rais wetu ni msikivu ana hekima, busara na upendo hivyo mpeni ushirikiano,” alisema Askofu Mang’ana na kuongeza: “Katika nchi yetu, tunawataka viongozi wawajibikaji walio na uchungu na nchi, wanaomsaidia Rais wetu katika kutekeleza majukumu ya msingi ya kulihudumia taifa, sio Rais wetu aende kushughulikia tatizo dogo la ukosefu wa maji Ubungo, ilihali wasaidizi wake wapo.

“Tunawataka watendaji wa mitaa, serikali za vijiji, wabunge na mawaziri wawajibike kwa wananchi.”

Aidha, aliwataka baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini kuacha tabia ya kushiriki kwenye maandamano kwa lengo la kujipatia umaarufu wa kisiasa na kusema kuwa kufanya hivyo ni kuingiza nchi katika machafuko na kusababisha kupotea kwa amani nchini kama hali ilivyo katika nchi za Libya na Misri.

“Viongozi wetu lazima wawe tayari katika kuilinda amani iliyopo nchini, kushiriki katika maandamano kama njia ya kuishinikiza serikali ili kudai haki sio sawa, hivi hakuna njia nyingine ya kudai haki, sharti watu washiriki kwenye maandamano tu?” Alihoji askofu huyo.

Kwa upande wake, Rais Kikwete aliwataka viongozi wa dini nchini kuwapatia fursa za nafasi za kusoma kwenye shule zao vijana watakaokuwa wanajiunga na shule za sekondari za kidato cha tano na sita kwa kuwa mahitaji ya shule hizo kwa sasa yatakuwa makubwa kwa miaka ijayo kutokana na wingi wa wanafunzi wanaofaulu kutoka katika sekondari za kata nchini.

“Niwaombe viongozi wa madhehebu ya dini na shule zenu muwapatie fursa vijana wetu wanaochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na sita kwa miaka ijayo ili waweze kusoma maana mahitaji ya nafasi hizo ni makubwa na serikali peke yake haiwezi, maana nikiri kuwa tulijenga sekondari za kata bila ya kuwa na maandalizi ya nafasi za shule kwa ajili ya kidato cha tano na sita,” alisema Rais Kikwete.

Kuhusu udhibiti wa dawa ya kulevya nchini, aliyaomba madhehebu ya dini nchini kwa kushirikiana na wananchi kuongeza udhibiti wa vitendo vya dawa za kulevya, kwani alisema hali sio nzuri kwa sasa.

Alisema mwaka jana, watu 12,119 walifikishwa mahakamani kutokana na kupatikana na dawa za kulevya, ambapo kiasi cha kilo 190 na gramu 780 za heroini zilikamatwa, kilo 65 za kokeini na kilo 27,9520 za bangi na mirungi kilo 10,310 ilikamatwa.

“Hali sio nzuri kwa Mkoa wa Mwanza juu ya kuwa na wingi wa dawa ya kulevya, naomba kwa pamoja viongozi wa dini na serikali tushirikiane katika kuidhibiti hali hiyo,” alisema Rais Kikwete.
SOURCE: HABARI LEO
==================================
Askofu amshangaa Kikwete
• Ahoji kuwagwaya viongozi mizigo
Na Sitta Tumma, Mwanza
MWENYEKITI wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa la Mennonite Tanzania, Askofu, Steven Mang'ana, ameelezwa kushangazwa na Rais Jakaya Kiktwete kushindwa kuwafukuzwa kazi viongozi wanaoonekana kuwa mzigo katika serikali yake.
Akizungumza kwenye misa takatifu ya kumsimika Mhashamu Askofu, Albert Jela Randa wa Kanisa la Mennonite (T), Dayosisi ya Mwanza, Jimbo la Nyakato jijini hapa, Askofu Mang’ana, mbali na kushangazwa na hatua kitendo hicho, pia amehoji sababu za Rais Kikwete kushindwa kuchukua maamuzi magumu, ili kuweza kulinusuru taifa.
“Madini, misitu, samaki zote zinakwenda na wawekezaji wakati serikali na viongozi wapo wa kudhibiti hali hii. Ikumbukwe kwamba, utu wa mtu haulinganishwi na kitu chochote...ee bwana waondoe hawa viongozi unaowaona ni mzigo," alisema.
Alisema kamwwe viongozi hao hawapaswi kufumbiwa mambo, kwani wamekuwa wakimwamisha maendeleo mbalimbali nchini ikiwamo kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Pamoja na hayo, alisema kuna baadhi ya wanasiasa wana tabia ya kulipiza visasi na kubainisha kuwa viongozi wa aina hiyo hawastahili kuwapo katika Tanzania ya sasa, kwani wanatishia uvunjivu wa amani nchini.
Kwa upande wake, Raish Kikwete alikiri kushamiri kwa biashara ya dawa za kulevya nchini na kusema serikali bado inakabiliwa na mtihani mgumu wa kudhibiti biashara hiyo haramu.
Katika kuthibitisha hayo, Rais Kikwete ameutaja mkoa wa Mwanza kuwa miongoni mwa mikoa inayoongoza nchini kwa biashara na matumizi ya dawa hizo, hali ambayo imemlazimu kutangaza kuunda chombo maalumu kinachojitegemea kupambana na janga hilo nchini.
Akizungumza katika misa hiyo, Rais Kikwete alisema licha ya serikali kuziunganisha Idara za Usalama: Jeshi la Wananchi (JWTZ), Polisi na Usalama wa Taifa katika kupambana na uingizwaji, utumiaji na usafirishaji wa dawa hizo za kulevya, bado mambo si shwari.
Alisema ingawa vita ya kutokomeza dawa hizo bado haijafanikiwa, mwaka jana watu 12,119 walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kujihusisha na biashara hiyo.
“Tatizo la dawa za kulevya nchini bado ni kubwa, na Mwanza ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa biashara ya matumizi ya dawa hizi.
“Niliamua kuziunganisha Idara ya Usalama wa Taifa, polisi na JWTZ katika kupambana na vita hii kwa vile kila kitengo kinawajibika kiusalama.
“Kikosi kazi hicho kipo, kinafanyakazi nzuri lakini mambo bado hayajawa mazuri, tunahitaji nguvu na ushirikiano zaidi,” alisema Rais Kikwete ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika kumuweka Wakfu Askofu Randa wa kanisa hilo.
Rais Kikwete hakuishia hapo, bali aliweka wazi takwimu za dawa hizo zilizokamatwa kwa kipindi cha mwaka jana kuwa heroine kilo 190 na gramu 780, cocaine kilo 65, morphine kilo 11, bangi kilo 279,520 na mirungi kilo 10,317.
“Kati ya gramu hizo 780, gramu 260 zilikamatwa mkoani Mwanza na watu 26 kutiwa nguvuni,” alisema bila kutaja iwapo watu hao 26 walishafikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria ama la.
Katika hali nyingine, jana Rais Kikwete wakati akielekea kwenye misa hiyo ya kanisa la Mennonite alijikuta katika wakati mgumu baada ya kupokelewa njiani na makundi ya watu wengi huku wakimuonyesha alama ya vidole viwili, alama ambayo inatumiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Hali hiyo iliyoonekana kumshtua zaidi Rais Kikwete na msafara wake wa zaidi ya magari 20, likiwemo gari la kubeba wagonjwa (Ambulance), lenye namba za Usajili STK 8134, ilijitokeza kiongozi huyo alipofika maeneo ya stendi kuu ya mabasi Buzuruga, ambapo karibu watu wote waliokuwa wamejipanga barabarani walikuwa wakimuonesha alama ya V.
Source: Tanzania Daima
========================================
 
Staili ya Kikwete siku hizi ni kuunganisha ziara zake na matukio ya makanisa ili kuondoa aibu ya kukosa wahudhuriaji, maama pesa ya kukodisha magari ya kusomba watu hakuna.
 
Staili ya Kikwete siku hizi ni kuunganisha ziara zake na matukio ya makanisa ili kuondoa aibu ya kukosa wahudhuriaji, maama pesa ya kukodisha magari ya kusomba watu hakuna.

hiyo ni kujivua gamba la UDINI alilova wakati wa kampeni , sjui la uchaga atalivua vipi?
 
Akumuulize Nyambari Nyangwine yaliyomkuta Tarime alipokwenda kichwa kichwa japo ndio mbunge wa huko kama alivyo yeye ni raisi
 
JK muoneeni huruma, leo nimeongea na rafiki yangu yuko halmashauri ya manispaa ya shinyanga kanihakikishia kuwa hawajapata mishahara ya mwezi mei, wakati majeshi yote kayalipa on 16th May.Mjue kuwa analipa mishahara kwa mafungu.Hana kete ya kubadili upepo lake zone, kumbukeni waliokufa Tarime wana ndugu zao Mwanza.Watajibeba mwaka huu
 
ataenda Bujora kunakila ulinzi wa kutosha hapo kama uchawi atapa maana ndio walinzi wake ndio maana ameamua haraka haraka kwenda Mwanza baada ya mzee kutangulia mbele ya haki
 
Back
Top Bottom