Rais Kikwete na ziara ya kwanza Jijini Mwanza baada ya uchaguzi

Kwa nini asiende Tarime kwanza? Huu mgogoro ni mkubwa kabisa..it's beyond proportions..
Yaani hawa watawala wa Tz priorities zao always zimekaa kinyumenyume..bure kabisa
Very unfortunate in deed!
 
magari yametangukizwa kwa ndege ya jeshi ni kweli yuko safarini kwenda Mwanza badalaya kwenda Nyamongo anaenda kupumzika kwenye vilima vyenye upepo ana siku nzima ya jumapili akila upepo mwanana mwache akapumzike kwa hiyo amesikia walichomuambia CDM anazurura nje ya nchi tuu
 
Mi sielewi umuhhimu wa mtoa mada hapa maana ishu siyo ishu bali ni umbeya tu siinui mantiki ya kutujulisha ziara hamna jipya haoa
 
Hiyo si ziara ya kuwashukuru wapigakura ni uzinduzi wa miradi hawajasema hata siku moja iwapo atafanya mkutano wa hadhara na wananchi.
 
CCM wana mpango kabambe wa kuchukuwa Mwanza yote 2015!!! believe it or not. Taarifa nilizo nazo ni kwamba wameshaanza kupata mashabiki (kwa siri) majimbo ya Ilemela na Nyamagana. Kuna timu inamwaga sumu vibaya. Siku chache zilizopita Kikwete alichanga milioni sh. 10 kwenye jimbo la Wenje. that's starters for you. Sasa Bwana mkubwa mwenyewe anakwenda huko kwa siku kadhaa kuendeleza mapambano.

Wenje is not doing well at all.Na amekuwa mgumu kusikiliza/kufanyia kazi ushauri anaopata.( I know what I am talking about). Kwa kujikumbusha Wenje kwa kiasi kikubwa alipata ushindi kwa sababu watu wengi hasa vijana walikuwa wanamchukia sana Masha. So, yeyote angesimama kutoka chadema kumpinga Masha angepita. Alichotakiwa kufanya Wenje ilikuwa kuwa opposite ya Masha. Awe aggresive kutatua matatizo ya jimboni kwake na awe karibu nao. Watu wengi wamekuwa wanampa ideas za kujimiirisha, wengine ni wana-ccm tena wenye vyeo ccm lakini anaonekana kujiamini kupundikia. Mwanaccm mmoja ambaye ameshaampa ushauri anasema "tatizo wenje ni bishoo, aache ucheki-bobu".

Mimi nashauri Chadema makao makuu waanzishe kitengo maalum kitachokuwa kinaratibu/kufuatilia utekelezeji wa mipango ya maendeleo kwenye majimbo waliyoshinda ili kuziba hii hatari ya kuyapoteza 2015. Kitengo hiki kwa kushirikiana na uongozi wa juu wa chama wawe wanatoa ushauri pale kasoro zinapotokea. Ni hivi kwa majimbo ambayo tayari yako chadema basi wafanye wafanyavyo kuhakikisha yanakuwa 'Locked in' meaning wawe karibu na wananchi, watatue matatizo yao. basi.

Sasa, majimbo yanayonyemelewa kwa udi na uvumba kwa taarifa nilizo nazo:
1. Ilemela
2. Nyamagana
4. Singida mashariki (Tundu Lissu)
5. Kawe - Halima Mdee
6. Arusha Mjini
 
afike pia magu maana alitoa ahadi ya kusambaza maji vijiji vyote pale magu baada ya kusikia ngongoseke wa upinzani ana nguvu,bangosha najua mta mtulaga nkoi.du kama mura.
 
Wananchi wana haki ya kumzomea Mwizi, Fisadi papa au muuaji kila mtaa na hoteli yoyote atakayoonekana hadi akimaliza ziara yake tusikie maneno ya Fisadi lililokubuhu au jizi hilo fisadi hilo nk.
 
Sasa nimepata picha. Zitto kabwe ni mshiriki mkubwa wa kikwete. Ni zitto aliyewakilisha mchango wa tsh 10mil kutoka kwa jk, ktk hafla ya kuchangia mfuko wa elimu, wenje akiwa muandaaji, kumbe mil 10 ilikuwa ni kisafisha njia? Jk, kwa nn amtume zitto wakat kandoro mwakilishi wake yupo? Naanza kushawishika na mawazo ya weng kuhusiana na zitto.
 
Kwa nini asiende Tarime kwanza? Huu mgogoro ni mkubwa kabisa..it's beyond proportions..
Yaani hawa watawala wa Tz priorities zao always zimekaa kinyumenyume..bure kabisa
Very unfortunate in deed!

Bado anaomboleza msiba wa Mlinzi wake.
 
Sasa nimepata picha. Zitto kabwe ni mshiriki mkubwa wa kikwete. Ni zitto aliyewakilisha mchango wa tsh 10mil kutoka kwa jk, ktk hafla ya kuchangia mfuko wa elimu, wenje akiwa muandaaji, kumbe mil 10 ilikuwa ni kisafisha njia? Jk, kwa nn amtume zitto wakat kandoro mwakilishi wake yupo? Naanza kushawishika na mawazo ya weng kuhusiana na zitto.

Usiwe na hofu mkuu, wamezoeana tu na walitaka kumtumia hapo awali wakagonga mwamba. Zitto ni CDM pyua.:smow:
 
Wananchi wana haki ya kumzomea Mwizi, Fisadi papa au muuaji kila mtaa na hoteli yoyote atakayoonekana hadi akimaliza ziara yake tusikie maneno ya Fisadi lililokubuhu au jizi hilo fisadi hilo nk.

Bado ni Rais wetu ingawa amewekwa na NEC. Cha maana wambane kuhusu ahadi zake, hasa ya ile Meli kubwa ya kisasa ya kwenda Bukoba.
 
Sijui kama kuna wanaotegemea kumwona huyu fisadi Mwanza ...

Tunawaomba wenyeji wa Mwanza na Familia zenu kaeni mbali na kama wanawapa pesa kumpigia makofi kikwete zichukueni kwasababu ni mali zenu na mlishe familia zenu. Kama mkiweza mzomeni kikwete na mafisadi wao watakaoongozana nae huku Mwanza.

Ziara za Kuwanunua Watanzania zimeanza na kama huu sio violation of democracy ni nini? Alimchagua na kumpigia kikwete kura Mwanza ni nani?

"Hata ukitumia pesa za serikali na vyombo vya ulinzi Tanzania wote hawa ni ndugu zetu na Hawakutaki kikwete, Mungu Apendi Uongo Hata Mara Moja"

Usiemtaka ni wewe na siasa zako za chuki....
 
Kuna safari ya nje ndefu inafuata, anazuga katikati ya nchi tudhani yupo yupo.

Ziara ya Rais ya kumsimika Askofu na kukagua ujenzi wa chuo cha polisi ambacho hakijaisha, come on now!
 
Asante kwa taarifa mkuu Katulanda ingawa hiyo ya mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama kuwa meya haijakaa sawa.
 
Kuna safari ya nje ndefu inafuata, anazuga katikati ya nchi tudhani yupo yupo.

Ziara ya Rais ya kumsimika Askofu na kukagua ujenzi wa chuo cha polisi ambacho hakijaisha, come on now!
akizunguka nchini mnachonga, akienda nje mnachonga...wabongo bana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom