Rais Kikwete na ziara ya kwanza Jijini Mwanza baada ya uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete na ziara ya kwanza Jijini Mwanza baada ya uchaguzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fred Katulanda, May 27, 2011.

 1. Fred Katulanda

  Fred Katulanda Verified User

  #1
  May 27, 2011
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  RAIS Jakaya Kikwete kesho ataanza ziara ya siku tatu mkoani Mwanza hii ikiwa ni ziara yake ya kwanza baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba mwaka 2010 na chama chake kupoteza majimbo ya Nyamagana na Ilemela.


  Katika ziara hiyo mara baada ya kuwasili Rais Kikwete atahudhuria Ibada ya misa takatifu ya kuwekwa wakfu kwa Askofu Mteule Albert Randa wa kanisa la Mennonite Mwanza.


  Rais Kikwete ambaye atawasili kwa njia ya ndege atapokelewa na viongozi mbalimbali ya wa mkoa wa Mwanza, ikiwa ni pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama huku mwenyeki wake akiwa ni mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbasi kandoro na Meya wa Jiji la Mwanza ambaye ni kutoka chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Josephat Manyerere ndiye takaye mpokea kama mwenyeki wake.


  Kwa mujibu wa ratiba yake iliyotolewa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza chini ya Abbas Kandoro, baada ya ibada hiyo ya kuwekwa wakfu kwa Askofu huyo atapumzika mpaka Jumatatu ambako atashiriki sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Usagara- Geita ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami.


  Baada ya kumaliza uzinduzi huo Rais Kikwete atatembelea kukagua ujenzi wa chuo cha mafunzo ya Polisi Marine ambacho kinajengwa Nyegezi jijini Mwanza kwa uhisani wa serikali ya Marekani.


  Serikali ya Marekani ilifadhili kiasi cha Dola za kimarekani 3 milioni baada ya kuliana saini mkataba wa kujenga chuo hicho kwa lengo la kusaidia kukomesha uhalifu ziwani Victoria.


  Mkataba huo wa ujenzi wa chuo hicho ulisainiwa na Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wakati huo, Lawrence Masha katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza Februari 18 mwaka 2010.


  Mbali na kufadhili ujenzi huo pia serikali ya Marekani ililizia kutoa msaada wa boti 10 zitakazokuwa zikifanya operesheni katika visiwa vilivyomo ndani ya Ziwa Victoria, msaada ambao utatekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia mwaka jana hadi mwaka huu.
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  vipi ana walinzi wa kutosha?


  Source please au wewe ndo Salva?
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  dALILI za kuanguka zaja!
   
 4. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ulinzi kama kawa yeye ni amiri jeshi mkuu na rais wa watanzania pamoja na wanachama wa CDM akiwemo Dr. Slaa
   
 5. Fisadi Mkuu

  Fisadi Mkuu Member

  #5
  May 27, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chadema wanaweza wakampopoa mawe kama alivyopopolewa kule Mbeya wakati ule
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ni bora kwasababu Mwaka 2005 Mwanza Mjini ilimpa kura zaidi ya Majimbo yote Tanzania alipata zaidi ya asilimia 95%

  Lakini baada ya kuwa na Lau Masha na Ubinafsi wake inasemekana Lau Maeneo ya Mabatini Polisi Lau alipata kura 4 na rais alipata asilimia 15 tu na Pale Mabatini ndio Nyumba za Polisi na Familia zao wanakoishi...

  Lau ndio aliyemuangusha Rais Mwanza ... KAZI IPO!!!
   
 7. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Who replaced sheik yahya?
   
 8. MANI

  MANI Platinum Member

  #8
  May 27, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Wamuulize ile ahadi ya meli !
   
 9. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,948
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  Hana maana hiyo ya polisi. Mwanza alishadondoka na sasa mchawi wake keshakufa. Ameshapata mchawi mwingine? Au ndo wewe?
   
 10. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  anajipendekeza kweli kwenye makanisa mzeee wa kicheni part!
   
 11. h

  hans79 JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  sio cdm waliotenda hayo bal waliomfumania,anzie Mbeya kule walikomfunza adabu huon kaul kama ukitaka kula lazima uliwe kidogo haziongei
   
 12. L

  LAT JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Ambilikile Mwasapila is the possible candidate for replacement
   
 13. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Me nilikuwa nafikiri anaenda kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kwa mara ya pili kurudi Magogoni, kumbe anaenda kuzindua barabara na jengo la polisi marine, halafu na kudoea mnuso wa kanisa, khaaa rais mlafi huyu, uo uzinduzi ungefanywa hata na Kandoro ingekuwa poa tu. Mami, Ngosha akija huyo mfanyeni kama Nyambari Nyangwine.
   
 14. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Huko mwanza visiwani kuna vizisiwa wala hawjui raisi wala hawana umuhimu wa serikali kuu. Kuna visiwa wana systm zao mahaama zao na sytem zao za utawala wao na maisha yao.

  Na Hayo Majambazi sugu ambayo ndiyo yanamiliki au marais wa visiwa hivyo ndo wafadhili wakubwa wa CCM.  Tushukuru serikal ya USA kwa kujali usalama wa watumiji wa ziwa victoria
  . Hivi na vifaa vya kijeshi huwa tunomba misaada ?
   
 15. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,948
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  Babu wa Loliondo's kikombe will make him resign ha ha ha. His option is a witch
   
 16. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Shekhe ndo kaondoka tena
   
 17. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #17
  May 27, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,651
  Likes Received: 21,866
  Trophy Points: 280
  Reverend nakuonya acha sasa tabia ya kutesa wenzio kwa kicheko. Pengine utabiri wako ukatimia katika kumsimika askofu, mie nimejawa na hofu.
   
 18. domo bwakubwaku

  domo bwakubwaku Member

  #18
  May 27, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  JK anakuja mwanza kuwaangukia wafanyabiahara wa mwanza baada ya kupoteza majimbo yanyamagna na ilemela na anaeinjinia ni gachuma hiyo ya barabara ni danganya toto
   
 19. n

  niweze JF-Expert Member

  #19
  May 27, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sijui kama kuna wanaotegemea kumwona huyu fisadi Mwanza ...

  Tunawaomba wenyeji wa Mwanza na Familia zenu kaeni mbali na kama wanawapa pesa kumpigia makofi kikwete zichukueni kwasababu ni mali zenu na mlishe familia zenu. Kama mkiweza mzomeni kikwete na mafisadi wao watakaoongozana nae huku Mwanza.

  Ziara za Kuwanunua Watanzania zimeanza na kama huu sio violation of democracy ni nini? Alimchagua na kumpigia kikwete kura Mwanza ni nani?

  "Hata ukitumia pesa za serikali na vyombo vya ulinzi Tanzania wote hawa ni ndugu zetu na Hawakutaki kikwete, Mungu Apendi Uongo Hata Mara Moja"
   
 20. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #20
  May 27, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Akitoka hapo aende Tarime
   
Loading...