Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,378
- 39,319
Kwa vile hakuna sheria inayomkataza Rais kufanya biashara akiwa Ikulu au hata kushirikiana na mmoja wa mawaziri wake kuingia ubia wakiwa madarakani kufanya ujasiriamali. Kwa vile mara nyingi habari za biashara za Rais akiwa madarakani hazitoki hadi akitoka madarakani; miye nimeamua kuuliza tu hivi tunapopiga kelele na porojo zetu inawezekana kabisa kuwa Kikwete na Karamagi wameanzisha kakampuni kao ka "B2MPOWERS RESOURCES"? Je, ni tutajuaje kama Rais sasa hivi hafanyi biashara yoyote Ikulu au hajaanzisha ka mradi ka pembeni ka kumuingizia kipato akitumia connection yake na access yake ya information za uwekezaji?
Binafsi naomba tuambiwe tu Rais ana hisa kwenye makampuni ya madini au nishati? na pia Waziri wake ana hisa gani kwenye kampuni gani kwani tunajua yeye ni mfanya biashara? Hivi Barrick Gold inauhusiano wowote wa kibiashara na kampuni za Karamagi?