Rais Kikwete na safari za nje

mzeewabusara

Member
Jun 7, 2006
12
24
Pamoja na kufurahi kumuona Rais wetu akisafiri katika mikutano ya kimataifa, nimefuatilia na kuona kuwa rais wetu anasafiri sana na kuhudhuria mikutano mingine ambayo ingeweza kuwakilishwa na makamu wake, waziri mkuu au mawaziri maalum wa wizara husika.

Mfano mkutano wa juzi wa Afrika Kusini kukutana na Bill gate angeweza kuhudhuria waziri anayehusika na technology. Hii itampa muda wa kutosha raisi kukaa ofisini kwake na kutoa mwongozo wa taifa.

Anyway ni small observation. Nahisi kuna baadhi ya watu huenda pia mmeiona.
 
Ile picha na Bill Gates niliona tu kwenye gazeti. Halafu haikuelezwa kirefu alkuwa anasaini kitu gani.
Huko nyuma tumeongelea hili suala la huyu jamaa kusafiri. Zaidi ya yote ni ile gulf stream, inakunywa mafuta kiasi gani? Hii bajeti ya huyu rais ni kubwa mno. Kuna mtu anaweza kukadiria. This hollywood star is making a big hole in the budget. Six to seven month in office, how much spent on him ?
 
Mzee wa Busara,
Mimi naona ilikuwa fit kabisa kwa rais wetu kukutana na Bill Gates. Waziri wa teknolojia angepwaya pale.
Bill Gates rika lake ni akina Mandela, Bill Clinton na waheshimiwa wa hadhi kama hiyo :D
 
Kwa hiyo sasa serkali ta Tanzania imeisha jitia kitanzi cha kutumia microsoft katka ofisi za serikali na institution zake!

Tumekwisha,
nchi za Ulaya wanaikimbia Microsft kwa kuwa gharama zake(software) ni kubwa.

Nchi za dunia ya tatu zinapaswa kutumia LINUX ambayo software nyingi ni za bure!!!

Nchi kama Germany wanatumia LINUX katika ofisi zake zote za serikali!

Bill Gate sasa amehamia Afrika Ulaya hapawezi!


Sisi Tutaweza kulipia hizo software?
 
A negative comment over JK never expected from you it will be a miracle if you would say otherwise .Mbuzi anakula urefu wa kamba yake and yo are proving this to us kwa hiyo tuachie na wengine tujadili maana una majbu yako .It is impossible useme JK kafanya vibaya hata siku moja tukiangalia historia yako na utawala huu .
 
Lile dege wala likate mawingu na mcheza Cinema wa Hollywood ale pesa yetu akirudi huko kutakuwa na kutano lingine Canada ataenda iko kazi sana .Mimi yangu macho naumia kwa kutumia pesa ya kodi yangu vibaya lakini kura sikumpa ila kuna watu wanaumia mara 2 yaani pesa ya kodi kutapanywa na walihangaika kupanga mistari na kumpigia kampeni juani na sasa wanalia sawa na mimi lakini nina nafuu kidogo .
 
Uchumi wa Tanzania unadorora kwa kasi kubwa kuliko wengi wanavyotambua. Kila saa kisingizio ni UKAME, lakini sio jibu sahihi kwani hata Kenya walipata ukame kama sisi na uchumi wao unazidi kupata nguvu.

Kwa kipindi hiki (June Quarter) balance of payments in Kenya ni +US$600 million. Yaani waliingiza kiasi hicho zaidi ya walivyotumia. Kwa upande wa Tanzania, JK alipokea nchi iliyokuwa na stock of foreign reserves za kutosha kulipia imports za miezi 8. Sasa, nusu mwaka tu baadaye, zimebakia fedha za kigeni za kutosha imports za miezi 4.5 tu.

Wako hapa baadhi ya watu ambao hawakuwa na macho ya kuona Mkapa alivyokuza uchumi. Mkapa alipoingia madarakani, alikuta foreign reserves kiasi cha US$ 267 million tu, lakini wakati anaondoka alikuwa ameshazikuza hadi kufikia US$ 2,300 million that is a 861% increase).

Huwa naogopa ninapotazama mwaka mmoja mbele. JK ameweka watu kama Ngasongwa wasiojua hili wala lile kuendesha uchumi wa nchi. Angemwacha Kigoda kwenye nafasi yake. Na apunguze matumizi ya kuruka huku na kule kila leo. Kwani anadhani amechaguliwa wa kusafiri tu?

Augustine Moshi
 
Moshi,
Ndiyo hasara ya kumpa foreign minister urais. Amezoea sana kusafirisafiri.
 
Rais Kikwete ashauriwa kupungaza safari ughaibuni

Na Shadrack Sagati

CHAMA cha Wananchi (Cuf) kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kupunguza safari zake za nje ya nchi, badala yake atulie nchini kushughulikia matatizo ya kiuchumi yanayowakabili wananchi likiwemo suala la umeme.

Tamko la Baraza Kuu la CUF lililosomwa jana na Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, limeeleza kuwa manufaa ya safari za Rais Kikwete kiuchumi ni madogo ukilinganisha na gharama anazotumia.


Prof. Lipumba alisema tangu uongozi wa Serikali ya awamu ya nne uingie madarakani umetoa ahadi nyingi ambazo kiongozi wake mkuu ameshindwa kuzitekeleza badala yake muda mwingi anautumia kwa safari za nje ya nchi.


"Marekani ameshaenda mara mbili eti anaenda kuitangaza Tanzania na kuwakaribisha wawekezaji.., utavutiaje wawekezaji wakati hauna umeme," alihoji Prof Lipumba.


Alisema hakuna wawekezaji watakaokubali kuja kuwekeza katika nchi ambayo umeme unakoma saa moja asubuhi. Alisema utatuzi wa mambo ya ndani ya nchi utafanyika nchini na sio kwenda nje mara kwa mara.


Mwanasiasa huyo alichambua kuwa, Marekani ambako Rais Kikwete amekwenda mara mbili misaada yake kwa Tanzania katika muda wa miaka miwili ni dola za Marekani 11 milioni, kiasi alichodai ni kidogo ukilinganisha na nchi zingine za Ulaya.


"Nchi za Ulaya kama Sweden misaada yake kwa taifa ni kati ya dola 200 na 300 milioni, Uingereza nayo imekuwa inatoa fedha nyingi tu. Misaada ya namna hii anaweza kuisaini akiwa hapa nchini sio lazima aende nje," alisema mwenyekiti huyo ambaye ni mtaalam wa mambo ya kiuchumi.


Akichambua hali ya uchumi ilivyo, alisema tangu Rais Kikwete aingie madarakani ukali wa maisha na kupanda kwa bei za bidhaa muhimu nchini umeongezeka kwa ari, kasi na nguvu mpya.


Alisema hali hiyo imetokana na viongozi wa serikali kuendesha nchi kiusanii wa kuwadanganya na kuwalaghai Watanzania wakidhani wananchi hawaelewi ukweli wa mambo ulivyo.


Aliongeza kuwa uzembe wa Serikali ya CCM kukabiliana na matatizo makubwa yaliyoletwa na sera mbovu zisizo na dira wala mwelekeo wa chama tawala, ndio mwanzo wa kuporomoka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania, kuwepo kwa mgawo wa umeme ambao umevuruga uchumi wa nchi.


Alisema kuongezeka kwa tatizo la ajira kwa vijana na kushamiri kwa tatizo la rushwa kumetokana pia na sera mbovu cha uongozi wa serikali ya CCM. "Katika hali hii maisha bora kwa kila Mtanzania yataendelea kubakia kuwa ndoto isiyotimia."


Mwanasiasa huyo pia amesema chama chake kimesikitishwa na Serikali kushindwa kutekeleza mpango ulioelezwa na Rais Kikwete Februari mwaka huu kuwa, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeridhia fedha za msaada wa madeni zitumiwe kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura na kununua jenereta ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi.


Akizungumzia mpasuko wa kisiasa wa Zanzibar, Prof. Lipumba alisema dawa ya kutafuta ufumbuzi wa mpasuko huo ni kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kama ambavyo ilani ya uchaguzi ya chama hicho inavyoeleza katika chaguzi zilizopita.


Alisema hata Cuf kikishinda uchaguzi wowote huko Zanzibar kwa kutambua historia ya kisiwa hicho na majeraha ya kisiasa yaliyo miongoni mwa Wazanzibari, suluhisho pekee ni kuunda serikali hiyo.


Mwenyekiti huyo alisema pamoja na msimamo huo wa Cuf, chama hicho kinamtaka Rais kuchukua hatua kutokana na ahadi yake ya kushughulikia mpasuko huo.


"Sasa umefika wakati wa Rais kutekeleza ahadi yake kabla wananchi kuchoka kusubiri, uvumilivu una mwisho," alisema Prof. Lipumba.


Kiongozi huyo pia amemwomba Rais Kikwete kuandaa mkutano wa kitaifa utakaojumuisha viongozi wa vyama vyote vya siasa, taasisi za kijamii na wasomi kubadilishana mawazo juu ya namna taifa linavyoweza kukabiliana na matatizo yanayoathiri maisha ya Watanzania.
 
Kikwete na Lowassa wametumia fedha kiasi gani katika hizi ziara zao? wahariri wameuliza hilo kwenye mkutano wao ikulu?
 
Hawa wahariri jana waliniacha hoi sana,Rais kaenda kuongelea safari ya Cuba na Marekani,wao wanaanza kuulizia kuhusu vyeti feki!!
Sikusikia hata Mhariri mmoja ambaye alitaka kujua huo mkutano wa Non Aligned Movement Cuba ni wa nini wakati hizo pande walizokwepa kuji-align nazo sikuhizi hazipo?
 
Mzee Mwanakijiji said:
Raisi alisema nini kuhusu vyeti feki?

............ Aidha, wahariri hao walitaka kujua ni hatua gani zinachukuliwa kwa wabunge waliobainika kuwa na vyeti feki.

Rais Kikwete alijibu kuwa suala hilo limeshakabidhiwa kwa Spika wa Bunge ili lifikishwe kwenye Kamati za Maadili kwa uchambuzi. "Siyo mtu ana cheti cha kidato cha nne kumbe hata darasa la nne hajafika," alisema rais na kusababisha kicheko.

from:
http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2006/10/03/75674.html
 
Zanaki,
Huwa wanasema kuwa "all news is local." Yaani habari zinazointerest ni za hapo hapo nyumbani. Mambo ya non-alignment na kukutana na Bush yanaboa. Ila mimi ningekuwa na maswali zaidi kuhusu nyumba za serikali. Inavyoonekana watakaonyang'anywa ni wale small fish mikoani. Wale wa Mikocheni na Oysterbay watapeta.
 
Jasusi,
Umelenga kwenyewe haswaa... na ndio maana ametolea mfano wa Ma-OCD na sio Mawaziri wastaafu wanaoishi karibu na Ikulu.
 
Kulikoni said:
............ Aidha, wahariri hao walitaka kujua ni hatua gani zinachukuliwa kwa wabunge waliobainika kuwa na vyeti feki.

Rais Kikwete alijibu kuwa suala hilo limeshakabidhiwa kwa Spika wa Bunge ili lifikishwe kwenye Kamati za Maadili kwa uchambuzi. ”Siyo mtu ana cheti cha kidato cha nne kumbe hata darasa la nne hajafika,” alisema rais na kusababisha kicheko.

from:
http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2006/10/03/75674.html

Yaani hilo jibu la Rais limewaridhisha waandishi wetu maana wameangua kicheko tu?

a. Mhe. vipi kama baadhi ya mawaziri wako au viongovi wengine uliowateua watagundulika na vyeti feki utawafukuza kazi?
 
Rais Jakaya Kikwete amekuwa akifanya safari katika nchi tofauti kujitambulisha kama Rais Mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wafanyabiashara wa Tanzania kupata fursa ya kukutana na wafanyabiasha wengine na kuuwalika wawekezaji.

Mtandao wa JamboForums.com umeanza mpango wa kupata maoni ya wananchi kuhusu masuala muhimu yanayoikabili nchi yetu hivi sasa.

Nini maoni yako kuhusiana na suala zima la Safari za Rais Kikwete?
 
Huu mkakati anotumia JK naona kama umepitwa na wakati, nionavyo mimi unatakiwa ubunifu uchukue mkondo wake, suala la kujitambulisha halina manufaa kwa taifa, amekuwa mwaziri wa mambo ya nje kwa miaka 10 anafamika vilivyo.JK awaamini watendaji wake na akazimu madaraka kwa taasisi zinazo husika zifanye kazi yake matokeo tutayaona, kwa mtindo huu anaokwenda nao atashindwa kubeba miziko ya kashfa kwani mikataba ikibuma hatakuwa na kisingizio.

Nionavyo mimi,
mosi, kwa upande wa kutafuta wawekezaji Tanzania Investment Centre inafanya kazi gani, mabalozi walioko huko ng'ambo wanafanya kazi gani, kama hizi taasisi hazifanyi kazi ni bora zifutwe ili JK awe na kisingizio cha kusafiri, baadhi ya mikutano si lazima aende yeye akasimu madaraka kwa mabalozi au waziri wa mabo ya nchi za nje, akifanya hivyo taifa litaokoa gharama, na kufanya shuguli za maendeleo.

pili, mkakati wa kupata wawekezaji unaweza kufanikiwa hata JK akiwa hapa nchini si lazima asafiri, serikali ya marekani haina pesa, pesa wanazo wamarekani, balozi zetu kushirikiana na TIC wapewe jukumu na malengo, kuwashawishi wafanya biashara wakubwa watembelee nchi yetu kwa mwaliko wa Rais, wawekezaji hawa watapata furasa ya kuona sehemu watakayo wekeza badala ya kwauzia mbuzi kwenye gunia.

tatu, utaratibu wa raisi kutembea na utitiri wa wawafanya biashara umeshaanza kuleta wasiwasi kwa wananchi, hatujatangaziwa ni utaratibu gani unatumika kuwachagua hao wafanya biashara wanaongozana na muheshimiwa, wamachinga wamekuwa wa kwanza wanataka nao wakaone wenzao wanafanya biashara ng'ambo nao pia wataka kuingia ubia na wamachinga wenzao ng'ambo, kesho utasikia mama lishe, keshokutwa wabeba mizigo watalalamika wanaumia migongo kubeba lumbesa watataka kutafuta wabia ng'ambo ili wapate vifaa vya kubebea mizigo, malamiko haya yanakwenda mbali wengine wahisi labda JK analipa fadhila kwa wafanya biashara walio muwezesha kupita mchokato mzima wa uchaguzi, na pengine anajaribu kujenga uwezo kwa kuwazesha hawa wafanya biashara ili waje wamchangie pesa za uchaguzi 2010.

haya si maneno yangu na nisiukumiwe, ni maneno yanayosemwa mitaani
 
Mgumu

Nakuunga mkono kabisa! MABALOZI WETU WANAFANYA KAZI GANI? SWALI LINGINE NI KWAMBA, HUYU BWANA KAMA RAISI ANAKWENDA KUTAFUTA WAWEKEZAJI, JE HAYO MAZUNGUMZO YA UWEKEZAJI YANAKUWA YAKO KATIKA STAGE GANI? NAAMINI WANAENDA NA SHIDA ZETU TU KWENYE KARATASI KITU AMBACHO NI UPOTEZAJI WA MUDA NA KODI ZA WANANCHI.

Hawa wafanya biashara wanatakiwa waongee na balozi husika kupitia TIC, Wizara ya Biashara na Viwanda, Wizara ya Mambo ya Nje na vyombo husika kama wanataka kushirikiana na International Community na sio kutumia vyeo katika kufanya biashara.

This shows how INCOMPETENT we are in the global arena!!! SHAME
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom