Rais Kikwete na Mnyika ndani ya nyumba uzinduzi wa Hospitali ya Sinza!

Mkomawatu

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
267
118
Ndugu wadau bila shaka nyote ni wazima.

Nipo hapa Sinza Palestina ambapo Rais Kikwete atakuwepo katika kuzindua Hospitali ya Sinza, viongozi mbalimbali wa serikali za mitaa kata ya Sinza na maeneo mengine ya Jiji la Dar.

Mheshimiwa Mnyika amewasili pamoja Na Diwani wa Sinza Ndugu Renatus Pamba.

Ndugu nitazidi kuwaletea yatakayojili.
 
John Mnyika. Ni moja ya vijana ambao wapo makini wanao hitaji support ya wananchi makini na wenye uchungu na nchi hii.
 
Rais Kikwete anategemewa kuwasili muda wowote kuanzia sasa,shamrashamra na unazi wa kisiasa umechachamaa hapa,naona wana CCM wanaingia kwa vikundi na vidufu vyao bila kujali hii ni hafla ya kitaifa na sio mkutano wa siasa!
 
Endelea kutuambia yananayojir. hyo john ona atakavyojichekesha kwa MNENE

Sikuzote mwenye tabia yakucheka cheka ovyo ni J.K na siyo Mnyika! j.k hadi misibani huwa anacheka! remember kuzama kwa meli kule zanzibar
 
Ni jambo zuri na la maendeleo kwa taifa letu!

Ni kweli kabisa! ila hali ya ccm kuvaa kichama kwa jambo km hilo ni kero..wengine wana aleji na hayo mavazi yao, ni kwanini mambo yakimaendeleo tusiweke tofaut zetu mbal
 
acheni Majungu Watanzania, mwacheni azindue kwani Kila kitu cha Afya basi lazima Aende waziri husika au cha Ardh lazima aende waziri wake Acheni hizo afanye nn mseme Ndiyo, Hongera JK ni moja ya Maendeleo na Mboreshe huduma za Afya,
 
Mambo ya mavazi yao ya ccm...yanatukela...ifike mahali wapige marufuku mavazi ya chama kwenye hafla za kitaifa
 
Mnyika amepata nafasi ya kuonana na Rais uso kwa macho wakiwa pamoja katika ufunguzi wa mradi wa maendeleo. Sikumbuki kumuona kwenye picha mnyika siku Rais anafungua mradi wa mabasi yaendayo kasi. Kuhudhuria shughuli kama hizi ambazo zinawahusu wananchi ni muhimu sana kwa mbunge.

Mnyika atumie wasaa huu kumuomba Rais ili CCM itekeleze ilani yake kwa kujenga barabara pamoja na kuleta maji katika jimbo la Ubungo!
 
aiseeeeeeee babaangu vipi mama salma na vice p wanaumwa nini??? Cozi ndizo kazi zao
 
Huyo raisi nae, hizo si angeacha waziri wa afya ndio azundue?

Jamani kweli binadamu hawana shukrani. Mnalalamika sana kwamba Raisi kazi yake ni kusafiri tu hafanyi kazi yoyote hapa Tanzania, leo anafanya kazi yake ya kuongea na wananchi mnaanza kuzusha upumbavu wenu. Kweli kabisa shukrani ya punda ni mateke.
 
Ni kweli kabisa! ila hali ya ccm kuvaa kichama kwa jambo km hilo ni kero..wengine wana aleji na hayo mavazi yao, ni kwanini mambo yakimaendeleo tusiweke tofaut zetu mbal
Itachukua muda mrefu sana hawa jamaa wa CCM kubadilika kwani fikra zao zinaonye wao wana haki miliki ya hii nchi,wananchi wengine au wale wapinzani wa chama chao ni wageni na wamekuja kuvuruga amani ya nchi yao!
 
Rais Kikwete ameingia na jopo lake pamoja na Balozi wa korea kusini,naona Ephraim Kibonde ndio anawatambulisha wageni waalikwa,,Mnyika anatambulishwa lakini baadhi ya wana CCM wanazomea!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom