Rais Kikwete na mazungumzo na ujumbe wa CHADEMA

hapa hakuna ligi, nani mshindi au nani kaogopeshwa , tunachotaka ni mabadiliko

hata cdm wakilamba soksi na madiliko yakapatikana ni vizuri pia

naona upo kiubishi ubishi na mashindano zaidi

kaivipi kiubishi na mashindano zaidi? Nimeeleza ninachokiona kwa uelewa wangu wa mambo.
 
Jana wajumbe 8 wa CDM, walienda ikulu kuongea na rais juu ya sakata la katiba, wamweleze kwa niaba ya wananchi nini wananchi wanataka katika mbio za kupata katiba mpya.

Watu wengi wameponda picha zilizopigwa, na kusema ndo maandalizi ya kuwa na CCM C yaani CCM+CDM. Inaweza kuwa kweli hasa ukizingatia tabasam waliyokuwa nayo.

Mimi Bado nina imani na CDM kwa maana hii.

Wameenda Ikulu ili kuweka kumbukumbu sahihi. Iwapo Kikwwete atakubali mswaada urudi bungeni na kutoa maelekezo yatakayowapa nguvu wananchi namna gani ya kuunda katiba, nani wawe wajumbe na idadi gani nani awachague, basi mgogoro kati ya CCM. CDM, NCCR na makundi mbalimbali ya wanaharakati utakuwa umekwisha.

Lakini iwapo rais atawapokea, wapeane mikono kama walivyofanya, apewe mapendekezo kama walivyofanya CDM, halafu Rais, kwa utashi wake wa kisiasa, ayaweke kwenye masaburi yake, ayakalie mapendekezo yale, na aamue kusaini mswaada huo kanadamizi utakotumia hela nyingi kurudisha katiba iliyopo, basi CDM, NCCR na wanaharakati, watakapoanzisha nguvu ya umma kudai umma kuwa na nguvu kwa wanasiasa na makundi mengine watakuwa na kinga kwamba tulishauri hatukusikilizwa.

Hiki ndicho ninachokiona kwa hawa CDM na wanaharakati wengine waliotangaza maandamano nchi nzima, lakini mkwara wa baba ritz1 alipoongea na CCM DSM umewaogopesha, mpaka sasa hakuna aliyeandamana na hakuna aliyeafanya mdaharo tena.

Ni mawazo yangu, tujadili kwa hoja
.

CDM wana nia ya dhati kuleta mabadiliko ya kweli. Sidhani kama wana ajenda kama ya seif hamad, ambaye sasa baada ya kupigiwa salute na kupewa madaraka watanyamaza kwa vile wamepata madaraka. Na madaraka gani, muafaka kwa katiba ile ile. I can imagine Slaa anakuwa makamu wa tatu wa Rais ananyamaza na katika inabaki vile vile kama alivyo CUF. Let us wait and see!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Wameanza kutunga makubaliano sioni mbele kuna nini. Siamini Ujumbe wa CDM unaweza kukubali uzuri wa katiba hii ya mkoloni.

Hilo ndilo lililonitatiza; ina uzuri gani kama inaruhusu rais kusimikwa bila ya kuwa na ushahidi wa kutosha kuwa kweli alichaguliwa na wanachi.
 
RAIS Jakaya Kikwete na ujumbe wa Serikali yake, jana amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na kuwahakikishia viongozi wa chama hicho kuwa yeye na Serikali yake, wana dhamira ya kuhakikisha Tanzania inapata Katiba mpya.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jana jioni, katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, yamefanyika katika mazingira ya urafiki na ujumbe wa Chadema umewasilisha mapendekezo yake kuhusu mchakato wa kuandika Katiba mpya ya Tanzania.

Serikali imepokea mapendekezo hayo, ilieleza taarifa ya Ikulu. Hata hivyo, pande zote mbili zimekubaliana kukutana tena leo asubuhi ili kuipa nafasi Serikali iweze kutafakari mapendekezo hayo.

Kwa mujibu wa Ikulu, lakini pande hizo mbili zimekubaliana kuwa Katiba ya sasa ni Katiba nzuri iliyolilea Taifa kwa miaka 50 iliyopita kwa sababu ni Katiba ya sasa iliyoliwezesha Taifa la Tanzania kuwa na amani, utulivu na kupata maendeleo makubwa ambayo nchi yetu imepata mpaka sasa.

“Pia pande zote mbili zimekubaliana kuhusu umuhimu wa kutunga Katiba mpya kama Mheshimiwa Rais Kikwete alivyoliahidi taifa wakati wa salamu zake za Mwaka Mpya Desemba 31, mwaka jana, 2010, Katiba ambayo italiongoza Taifa la Tanzania kwa miaka mingine 50 ijayo,” ilieleza taarifa hiyo.

Katika mazungumzo hayo, Rais aliwahakikishia wajumbe hao wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kuwa ni dhamira yake na ya Serikali yake kuhakikisha kuwa Tanzania inapata Katiba mpya.

Aidha, pande zote mbili zimekubaliana kuwa ni jambo muhimu kwa mchakato mzima wa kutungwa kwa Katiba mpya kuendeshwa kwa namna ya kulinda na kudumisha tunu za taifa za amani, utulivu na umoja wa kitaifa.

Aidha, pande zote mbili zimekubaliana kuwa mchakato huo uendeshwe kwa kuzingatia misingi ya mambo mengine muhimu kwa Taifa la Tanzania kama vile kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani, kuligawa Taifa kwa misingi ya udini na ukabila ama kutugawa kwa misingi ya maeneo.

Mkutano huo umefanyika baada ya kuombwa na viongozi wa Chadema ambao Jumatatu iliyopita kupitia kwa Mbowe, walitoa maazimio ya Kamati Kuu ya Chama hicho, mojawapo likiwa ni kuunda Kamati ndogo ya kwenda kumwona Rais Kikwete kumweleza msimamo wao kuhusu mchakato wa Katiba mpya.

Mbowe alisema hatua hiyo imetokana na kutoridhika na Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 uliopitishwa na Bunge, bila ushiriki wa wabunge wa Chadema na NCCR-Mageuzi, waliosusa na kutoka nje.

Miongoni mwa madai yaliyosababisha wasusie mjadala huo ni kuwa Muswada ulikuwa na upungufu na marekebisho mengi yaliyosababisha wao kuona ni bora usomwe mara ya kwanza na kurudi kwa wadau wakiwamo wananchi ili watoe maoni kabla ya kusomwa mara ya pili.

Muswada huo uliotolewa kwa Hati ya Dharura, ulisomwa kwa mara ya kwanza bungeni Aprili na kupelekwa kwa wadau na kufanyiwa marekebisho kadhaa ikiwemo kuuweka katika lugha ya Kiswahili na kisha kusomwa kwa mara ya pili katika Bunge lililomalizika Ijumaa ulipitishwa na
kusubiri kusainiwa na Rais ili kuwa sheria.

Wajumbe wa Kamati hiyo ya watu saba ni viongozi wa juu wa Chadema na baadhi ya wabunge wa chama hicho wakiongozwa na Mbowe (Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni), Makamu Mwenyekiti Bara na Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi na Makamu Mwenyekiti Zanzibar na Said Issa Mohammed.

Wamo pia Katibu Mkuu, Dk. Slaa, Mwanasheria wa Chama na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, wajumbe wawili wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Profesa Mwesiga Baregu na Profesa Abdallah Safari.
 
CDM wana nia ya dhati kuleta mabadiliko ya kweli. Sidhani kama wana ajenda kama ya seif hamad, ambaye sasa baada ya kupigiwa salute na kupewa madaraka watanyamaza kwa vile wamepata madaraka. Na madaraka gani, muafaka kwa katiba ile ile. I can imagine Slaa anakuwa makamu wa tatu wa Rais ananyamaza na katika inabaki vile vile kama alivyo CUF. Let us wait and see!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

kama itakuwa hivi, basi kundi pekee litakalokuwa limebaki kuwatete watanzania ni wanaharakati pekee. Nitaachana kabisa na wanasiasa ingawa naamini maisha bila siasa hayawezekani. Lakini kwa siasa za namna hii, basi navua gamba la kushiriki kwenye siasa nibaki mwanaharaskati
 
RAIS Jakaya Kikwete na ujumbe wa Serikali yake, jana amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na kuwahakikishia viongozi wa chama hicho kuwa yeye na Serikali yake, wana dhamira ya kuhakikisha Tanzania inapata Katiba mpya.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jana jioni, katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, yamefanyika katika mazingira ya urafiki na ujumbe wa Chadema umewasilisha mapendekezo yake kuhusu mchakato wa kuandika Katiba mpya ya Tanzania.

Serikali imepokea mapendekezo hayo, ilieleza taarifa ya Ikulu. Hata hivyo, pande zote mbili zimekubaliana kukutana tena leo asubuhi ili kuipa nafasi Serikali iweze kutafakari mapendekezo hayo.

Kwa mujibu wa Ikulu, lakini pande hizo mbili zimekubaliana kuwa Katiba ya sasa ni Katiba nzuri iliyolilea Taifa kwa miaka 50 iliyopita kwa sababu ni Katiba ya sasa iliyoliwezesha Taifa la Tanzania kuwa na amani, utulivu na kupata maendeleo makubwa ambayo nchi yetu imepata mpaka sasa.

"Pia pande zote mbili zimekubaliana kuhusu umuhimu wa kutunga Katiba mpya kama Mheshimiwa Rais Kikwete alivyoliahidi taifa wakati wa salamu zake za Mwaka Mpya Desemba 31, mwaka jana, 2010, Katiba ambayo italiongoza Taifa la Tanzania kwa miaka mingine 50 ijayo," ilieleza taarifa hiyo.

Katika mazungumzo hayo, Rais aliwahakikishia wajumbe hao wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kuwa ni dhamira yake na ya Serikali yake kuhakikisha kuwa Tanzania inapata Katiba mpya.

Aidha, pande zote mbili zimekubaliana kuwa ni jambo muhimu kwa mchakato mzima wa kutungwa kwa Katiba mpya kuendeshwa kwa namna ya kulinda na kudumisha tunu za taifa za amani, utulivu na umoja wa kitaifa.

Aidha, pande zote mbili zimekubaliana kuwa mchakato huo uendeshwe kwa kuzingatia misingi ya mambo mengine muhimu kwa Taifa la Tanzania kama vile kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani, kuligawa Taifa kwa misingi ya udini na ukabila ama kutugawa kwa misingi ya maeneo.

Mkutano huo umefanyika baada ya kuombwa na viongozi wa Chadema ambao Jumatatu iliyopita kupitia kwa Mbowe, walitoa maazimio ya Kamati Kuu ya Chama hicho, mojawapo likiwa ni kuunda Kamati ndogo ya kwenda kumwona Rais Kikwete kumweleza msimamo wao kuhusu mchakato wa Katiba mpya.

Mbowe alisema hatua hiyo imetokana na kutoridhika na Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 uliopitishwa na Bunge, bila ushiriki wa wabunge wa Chadema na NCCR-Mageuzi, waliosusa na kutoka nje.

Miongoni mwa madai yaliyosababisha wasusie mjadala huo ni kuwa Muswada ulikuwa na upungufu na marekebisho mengi yaliyosababisha wao kuona ni bora usomwe mara ya kwanza na kurudi kwa wadau wakiwamo wananchi ili watoe maoni kabla ya kusomwa mara ya pili.

Muswada huo uliotolewa kwa Hati ya Dharura, ulisomwa kwa mara ya kwanza bungeni Aprili na kupelekwa kwa wadau na kufanyiwa marekebisho kadhaa ikiwemo kuuweka katika lugha ya Kiswahili na kisha kusomwa kwa mara ya pili katika Bunge lililomalizika Ijumaa ulipitishwa na
kusubiri kusainiwa na Rais ili kuwa sheria.

Wajumbe wa Kamati hiyo ya watu saba ni viongozi wa juu wa Chadema na baadhi ya wabunge wa chama hicho wakiongozwa na Mbowe (Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni), Makamu Mwenyekiti Bara na Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi na Makamu Mwenyekiti Zanzibar na Said Issa Mohammed.

Wamo pia Katibu Mkuu, Dk. Slaa, Mwanasheria wa Chama na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, wajumbe wawili wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Profesa Mwesiga Baregu na Profesa Abdallah Safari.

Mkuu umeona zile picha , jamaa wanaingia ikulu huku wanacheka na kunywa soda, juice, chai nk unafikiri kuna kitu hapo tena mkuu.

headline_bullet.jpg
Wamkabidhi Kikwete mapendekezo ya Katiba Mpya
headline_bullet.jpg
Mazungumzo yahairishwa, yapangwa kuendelea leo
headline_bullet.jpg
Ikulu yasifu mazungumzo ya awali waliyofanyika jana
headline_bullet.jpg
Yasema yafanyika katika mazingira ya urafiki

Mbowe Jk(1).jpg

Rais Jakaya Kikwete, akitazama nyaraka alizokabidhiwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe Ikulu jijini Dar es Salaam jana kuhusu mapendekezo ya Chadema ya kuundwa kwa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.(Picha: Khalfan Said)

Rais Jakaya Kikwete, jana alikutana na viongozi waandamizi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kufanya nao mazungumzo ikiwa ni kutekeleza ahadi yake ya kukutana nao baada ya chama hicho kuomba kuonana naye..

Rais Kikwete alikutana na viongozi wa Chadema Ikulu jijini Dar es Salaam jana wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa, hakuweza kuhudhuria kikao hicho kwa kile kilichoelezwa kwamba alipatwa na msiba wa ndugu yake wa karibu.

Taarifa fupi ya Mbowe kwa vyombo vya habari jana jioni ilieleza kwamba viongozi hao walikutana na Rais Kikwete kuanzia saa 9:30 alasiri hadi saa 12 jioni.

"Kikao kitaendelea kesho saa 4 asubuhi (leo), taarifa kamili ni baada ya kumalizika kwa kikao," alisema Mbowe katika taarifa hiyo.
Mbowe aliongoza Kamati ndogo iliyoundwa na Kamati Kuu kwa ajili ya kwenda kuzungumza na Rais Kikwete, kuhusiana na msimamo wa chama hicho juu ya kuboresha mchakato wa kupata Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Viongozi wengine wa Chadema waliohudhuria kikao cha jana ni Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, Said Amour Arfi na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Issa Mohammed wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu na Profesa Abdallah Safari.
Wengine ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Katibu wa Kamati hiyo.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari mapema wiki iliyopita, Mbowe alisema mazungumzo kati ya kamati hiyo na Rais Kikwete, yanalenga kutaka kumpa msimamo, mawazo na ushauri wao namna ya kuuboresha mchakato huo.

Alisema Kamati Kuu inaamini kuwa pamoja na sheria hiyo kupitishwa, bado kuna fursa za kisiasa na kijamii katika kujenga mwafaka wa kitaifa juu ya haja, nia, mchakato na misingi ya Katiba mpya.

Alisema ushiriki wa Chadema katika mchakato wa kupata katiba mpya uliowekwa na sheria hiyo, utategemea utayari wa serikali kufanya mabadiliko makubwa na ya kimsingi katika sheria hiyo kwa lengo la kujenga mwafaka wa kitaifa juu ya mchakato huo.
Katika kikao cha jana wajumbe wengine wa Chadema waliohudhuria ni Mbunge wa Ubungo, John Mnyika na Mkurugenzi wa Masuala ya Bunge na Halmashauri wa Chama hicho, John Mrema.

Kwa upande wa Serikali, mbali ya Rais Kikwete wengine waliohudhiria kikao hicho ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani.
Wengine ni Waziri wa Utawala Bora, Mathias Chikawe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu, Waziri wa Vijana, Habari, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi na viongozi wengine waandamizi wa serikali.

Katika kikao cha jana, baada ya viongozi wa Chadema kuwasili Ikulu, walikaribishwa na Rais Kikwete ambako pamoja na mambo mengine, walimkabidhi nyaraka zinazoeleza msimamo wa chama hicho, katika mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya.
Baada ya makabidhiano hayo, wapigapicha waliruhusiwa kupiga picha za matukio muhimu na kisha kuondoka ili kupisha mazungumzo ya kikao cha viongozi hao na Rais Kikwete.

Ikulu yasifu mazungumzo kufanyika mazingira ya kirafiki

Nayo taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu kwa vyombo vya habari imesifia mazungumzo ya pande hizo kuwa yamefanyika katika mazingira ya urafiki na ujumbe wa Chadema umewasilisha mapendekezo yake kuhusu mchakato wa kuandika Katiba Mpya ya Tanzania ambayo Serikali imeyapokea.

Ilieleza kuwa pande hizo zimekubaliana kukutana tena leo asubuhi ili kuipa nafasi Serikali kutafakari mapendekezo hayo.
Iliendelea kueleza kuwa pande hizo zimekubaliana kuwa Katiba ya sasa ni nzuri iliyolilea Taifa kwa miaka 50 iliyopita na iliyoliwezesha taifa la Tanzania kuwa na amani, utulivu na kupata maendeleo makubwa.

Vilevile zimekubaliana kuhusu umuhimu wa kutunga Katiba Mpya kama Rais Kikwete alivyoliahidi taifa wakati wa salamu zake za mwaka mpya Desemba 31, mwaka 2010 ambayo italiongoza Taifa la Tanzania kwa miaka mingine 50 ijayo.

Ilisema katika mazungumzo hayo, Kikwete aliwahakikishia wajumbe hao wa Chadema wakiongozwa na Mbowe kuwa ni dhamira yake na ya Serikali yake ni kuhakikisha kuwa Tanzania inapata Katiba mpya.

Iliongeza kuwa pande hizo zimekubaliana kuwa ni jambo muhimu sana kwa mchakato mzima wa kutungwa kwa Katiba Mpya kuendeshwa kwa namna ya kulinda na kudumisha tunu za taifa za amani, utulivu na umoja wa kitaifa.

Vilevile ilieleza kuwa pande hizo zimekubaliana kuwa mchakato huo uendeshwe kwa kuzingatia misingi ya mambo mengine muhimu kwa taifa la Tanzania kama vile kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani, kuligawa Taifa kwa misingi ya udini na ukabila ama kutugawa kwa misingi ya maeneo.

CHANZO: NIPASHE
 
Ngoja tusubiri hatima ya maongezi haya. Ninachoamini mimi hakuna cha maana kitachojitokeza kwenye majadiliano haya kwani CCM wana mengi ya kupoteza kama katiba nzuri itatungwa. Sioni kwa nini mwenye nacho awe tayari kugawana na asiyenacho ili naye aanza zoezi la kuombaomba. CDM lazima hili walielewe na kulijengea mikakati tofauti.

Wakuu, tusubiri ila safari ya ujenzi wa nchi yetu ni ndefu na yenye vikwazo vingi sana.
 
Tunachohitaji ni Tanzania yenye amani na maendeleo na sio zambi ikatokea kama znz au kenya cos lengo ni maendeleo tu,ccm itang'oka tu ikishindikana kwa kura,njia mbadala ni serikali ya umoja wa kitaifa mwisho wa cku tunahitaji watu serious wachapakazi na watakaokuwa na uchungu na nchi hii,all in all hayo ya ccm C ni kejeli zisizo na maana ktk maendeleo ya nchi yetu
 
Chadema are not safe from ill-will tactics of Magamba to make sure that the political opposition is crippled at all cost. They have successfully managed to silent CUF's activism buy merely engaging them into Zanzibar's government hierarchy and now Chadema seems to descend into the same trap. I advise Magwanda to be exta careful with CCM's double-dealing nature who might take an advantage of this meeting to entice Magwanda into accepting a coalition deal.
 
hapa hakuna ligi, nani mshindi au nani kaogopeshwa , tunachotaka ni mabadiliko

hata CDM wakilamba soksi na madiliko yakapatikana ni vizuri pia

naona upo kiubishi ubishi na mashindano zaidi

LAT kuna baadhi ya watu wanashindwa kuelewa kila kitu kwa wakati wake, mahali pake na namna yake. Hivi Mbowe kaenda Ikulu na anapiga picha na rais asitabasamu jamani? Ule ndiyo ubinadamu na kufanya hivyo hakumananishi ndiyo kilio chao walichokuwa wanadai kimeisha kwa kuona na kufika Ikulu au kupiga picha na rais.
 
Mazungumzo muhimu yaliyoanza jana kwa aijli ya kufunga ndoa kati ya chadema na serikali yataendelea tena leo ikulu jijini Dsm.habari zinaeleza kuwa maelezo yataendelea pale yalipoishia ambapo rais atatoa maelezo ya maombi yaliyowasilishwa kwake na ujumbe wa chadema ukiongozwa na kamanda mbowe.tutajuzana zaidi kadri ntakavyokuwa nazipata.............nawatakia kila la kheri viongozi wetu wtoke na msimamo na makubaliano yatakayokuwa na tija kwa taifa letu....Nawasilisha.
 
Tunachohitaji ni Tanzania yenye amani na maendeleo na sio zambi ikatokea kama znz au kenya cos lengo ni maendeleo tu,ccm itang'oka tu ikishindikana kwa kura,njia mbadala ni serikali ya umoja wa kitaifa mwisho wa cku tunahitaji watu serious wachapakazi na watakaokuwa na uchungu na nchi hii,all in all hayo ya ccm C ni kejeli zisizo na maana ktk maendeleo ya nchi yetu

Umoja wa kitaifa hakuna mfano ambapo umefanya kazi na ikaonekana kuwa ni nzuri. Kwani tunajifunza nini kutoka Zanzibar na Zimbabwe? umoja wa kitaifa umewasidia kwa lipi zaidi ya kutokuaminiana au mtu kusaliti alichokuwa anakiamini?

Umoja wa kitaifa unawezekana tu kwa wenye nia ya kuifilisi nchi, siyo kutofautiana katika hilo. Kama CDM nao wanalenga kuifilisi nchi, basi umoja wa kitaifa utawasaidia kufanikisha adhima yao lakini kama lengo lao ni kuirudisha nchi kwa wenye nchi, basi umoja wa kitaifa hata wasiufikirie.

Na nadhani hawatafika huku kwani wangeanza na umeya wa ARUSHA
 
chadema are not safe from ill-will tactics of magamba to make sure that the political opposition is crippled at all cost. They have successfully managed to silent cuf's activism buy merely engaging them into zanzibar's government hierarchy and now chadema seems to descend into the same trap. I advise magwanda to be exta careful with ccm's double-dealing nature who might take an advantage of this meeting to entice magwanda into accepting a coalition deal.

kweli umeokaka. Big up kwa evolution hiii
 
Back
Top Bottom