muonamambo
JF-Expert Member
- Sep 3, 2010
- 875
- 545
Naomba kukumbushwa wanajamvi hivi ni mwaka gani JK Alisuka mpango wa kuhamia CDM?
Mara nyingi CDM wamekuwa hawazingatii nini wanataka na kwa njia gani mbadala, maana busara chache nguvu nyingi katika kukabili masuala nyeti. Sasa wametumia busara wanasikilizwa. Nadhani wataendelea kujifunza busara zaidi. PEACE!Nimefurahi sana kuona hii movement.CCM na CDM vinaunganika pamoja kuitengeneza tanzania tuitakayo.
Mwanzoni hili waliliweza CUF na sasa naona CDM wameingia. Kwa mantiki hii upinzani Tanzania sasa basi.
Politics is the art of looking for trouble, finding it whether it exists or not, diagnosing it incorrectly , and applying the wrong remedy.
Anayeoa ndiye humfuata anayeolewa kwa maana hiyo Unamtusi Mkuu Wa Kaya maana ndiye aliyefuatwa hapo Ikulu.Hawa viongozi wa CHADEMA wamenihuzunisha sana leo. Yaani wanapiga picha na Rais wasiyemtambua huku wanacheeeeeeka meno yote 32 nje. Hapo unategemea nini zaidi ya kushuhudia ndoa nyingine ya mke wa pili wa CCM mwaka 2015. Kweli siasa za Tz ni vichekesho tupu.
Mkuu, unaweza kuwafahamisha watanzania walichokubaliana pale Ikulu?
Nadhani tutafika pale tunapopataka sasa, JK awe msikivu sasa
Hapo Mkuu wa kaya anaenda kutafuta ushauri kwa akina kingunge! Ngoja tusubiri atakuja na nini kesho!
Hiyo haiwezekani, tatizo sio JK kama yeye, bali akisema afanye haki na kusimamia katiba bora ni lazima itakula chama chake na washirika wake waliotuibia kwa miaka nenda rudi, sio kwamba ccm hawajui katiba ina matatizo wanajua, ndio mianya wanayotumia katika kulitafuna taifa.Nadhani tutafika pale tunapopataka sasa, JK awe msikivu sasa
Today i will sticky with you for a while, CHADEMA wamechagua kujidhalilisha, yote waliyokwisha sema kuhusu kikwete, wananchi kuwa mahakama ya mwisho na kutoka bungeni kaaa.Kikwete hakurupuki, bado hujamjuwa tu?
Mawazo yako kama yangu, kama katiba ni nzuri na imetuletea maendeleo kwa nini tupoteze muda na pesa kuibadilisha? Wajumbe wa cdm watueleze wazi kama ni kweli walikubaliana hivyo, kama si kweli tafadhali wakanushe mara moja kwa sababu huu ni upotoshaji wa hali ya juu. Kwa nini taarifa hiyo inazungumzia ubora wa katiba tu bila mapungufu yake, in actual fact, hivi kuna mtanzania sasa hivi ana interest ya kujua kama katiba ya sasa ni nzuri au la? Kuna umuhimu gani wa taarifa hiyo kutuambia kuwa wamekualiana kwamba katiba ya sasa ni nzuri. Kwa nini watanzania tunafanywa misukule? narudia tena, katiba ingekuwa nzuri kungkuwa na haja ya cdm kufanya mkutano na jk leo na kuendelea kesho????????? Chadema watch your step.
.....Aidha, pande zote mbili zimekubaliana kuwa mchakato huo uendeshwe kwa kuzingatia misingi ya mambo mengine muhimu kwa taifa la Tanzania kama vile kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani, kuligawa Taifa kwa misingi ya udini na ukabila ama kutugawa kwa misingi ya maeneo.
Imetolewa na:Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu,DAR ES SALAAM.27 Novemba, 2011
umesahau alivyokurupuka na falsafa ya kujivua gamba na ilivyomuumbua juzi dodoma!?Kikwete hakurupuki, bado hujamjuwa tu?
Jana wajumbe 8 wa CDM, walienda ikulu kuongea na rais juu ya sakata la katiba, wamweleze kwa niaba ya wananchi nini wananchi wanataka katika mbio za kupata katiba mpya.
Watu wengi wameponda picha zilizopigwa, na kusema ndo maandalizi ya kuwa na CCM C yaani CCM+CDM. Inaweza kuwa kweli hasa ukizingatia tabasam waliyokuwa nayo.
Mimi Bado nina imani na CDM kwa maana hii.
Wameenda Ikulu ili kuweka kumbukumbu sahihi. Iwapo Kikwwete atakubali mswaada urudi bungeni na kutoa maelekezo yatakayowapa nguvu wananchi namna gani ya kuunda katiba, nani wawe wajumbe na idadi gani nani awachague, basi mgogoro kati ya CCM. CDM, NCCR na makundi mbalimbali ya wanaharakati utakuwa umekwisha.
Lakini iwapo rais atawapokea, wapeane mikono kama walivyofanya, apewe mapendekezo kama walivyofanya CDM, halafu Rais, kwa utashi wake wa kisiasa, ayaweke kwenye masaburi yake, ayakalie mapendekezo yale, na aamue kusaini mswaada huo kanadamizi utakotumia hela nyingi kurudisha katiba iliyopo, basi CDM, NCCR na wanaharakati, watakapoanzisha nguvu ya umma kudai umma kuwa na nguvu kwa wanasiasa na makundi mengine watakuwa na kinga kwamba tulishauri hatukusikilizwa.
Hiki ndicho ninachokiona kwa hawa CDM na wanaharakati wengine waliotangaza maandamano nchi nzima, lakini mkwara wa baba ritz1 alipoongea na CCM DSM umewaogopesha, mpaka sasa hakuna aliyeandamana na hakuna aliyeafanya mdaharo tena.
Ni mawazo yangu, tujadili kwa hoja.