VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Bado nakereketwa na matamshi aliyoyatoa Ndugu Edward Ngoyai Lowassa jana Dodoma. Aliitisha mkutano wa wanahabari na kuzungumza nao mambo mbalimbali. Mawili yanakugusa mwenyekiti wa CCM na rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete. Moja, Lowassa amedai kuwa amesingiziwa na kuzushiwa kuhusu kashfa ya Richmond. Ni wewe mwenyekiti Kikwete uliyeridhia Lowassa aachie uwaziri mkuu kwa kashfa hii.
Ukiwa kama mwenyekiti wa CCM na rais wa Tanzania, ulikuwa fully informed na kadhia nzima. Uliletewa taarifa za mdomo na nyaraka. Uliletewa ripoti na kuipitia ipasavyo. Ukaridhika nayo na kuridhia Lowassa ajiuzulu. Mwenyekiti Kikwete, naamini ulijiridhisha vya kutosha. Jana, Lowassa anadai alizushiwa na kusingiziwa. Mwenyekiti na Rais atatengwaje na uzushi huu? Yaani Rais aendeshwe na uzushi? Si tu kumchokoza mwenyekiti, bali pia ni dharau na kiburi kwa chama na serikali yake.
Pili, Lowassa ameponda sera ya Kilimo Kwanza. Si hulka ya CCM kupondana hadharani. Ni hulka ya kichama kupongezana kwa ubunifu na utekelezaji wa Ilani. Ndiyo ilivyo. Sera zote huzaliwa na Ilani. Kuponda sera ni kuponda Ilani. Iweje kada, ananyemelea urais na uenyekiti aiponde Ilani waziwazi na abaki salama kichama? Haiwezekani. Lowassa ameonesha dharau na kiburi cha wazi kwa Ilani ya 2010-2015. Si mfano mwema.
Mwenyekiti Kikwete, umepata pa kuanzia. Umeanza kuiona sasa sura halisi ya kauli za Lowassa. Ongoza vyema chama chetu katika haki na wema huk ukizingatia kauli jana za Lowassa pale Dodoma. Kila la kheri Mwenyekiti Kikwete na timu yako.
Mzee Tupatupa wa Lumumba (safarini kwenda Kanda ya Kati)