Rais Kikwete (mwenyekiti wa CCM Taifa), umepata pa kuanzia

Hata kama akiongea na Watanzania wote hakuna Mtanzania atamuamini
Lowasa amesema hawezi kuhama CCM, akasema ambaye hamtaki CCM ndiyo ahame.
Lowasa ni kama uji wa moto, haumezeki, wala hautemeki.

Tunasubiria kuona nani atamfunga paka kengele!
 
haa haa lowasa kamnanga hadharani jk na pinda kwamba serikali yao haina maamuzi ni legelege. pia kaponda sera ya kilimo kwanza..
 
haa haa lowasa kamnanga hadharani jk na pinda kwamba serikali yao haina maamuzi ni legelege. pia kaponda sera ya kilimo kwanza..

As if yeye sio sehemu ya chama tawala. Alikuwa wapi kutoa ushauri wakati anajua zilikuwa ni sera fake??!!
 
As if yeye sio sehemu ya chama tawala. Alikuwa wapi kutoa ushauri wakati anajua zilikuwa ni sera fake??!!

mkuu tatizo viongozi wengi ndani ya ccm ni wanafiki na si wakweli kamwe. miaka karibu mitano serikali inahangaika na sera ya kilimo kwanza lakini lowasa yuko kimya tu. wala hasemi chochote pale bungeni ili kuishauri serikali. ni unafiki kwa kwenda mbeld. leo anatoka usingizini na kuponda sera hiyo.
 
Tatizo ukweli ndio unaokataliwa na ccm, Ukiangalia alichpkisema Lowassa kwa jana ni kweli kabisa. Haiwezekani ktk kashfa kubwa kama ya Richmond ainzishwe na kuhitimishwa na mtu mmoja. Haiwezekani hata kidogo kwamba mkubwa wake wa kazi wakati huo awe hakujua kinachondelea...!!

Na ndiomaana tunaona bila busara za Mkapa kwenye kikao kile cha Nec habari ingekuwa nyingine, na pengine utawala wa Kikwete ingefikia kikomo kwenye NEC ile.

Lakini pia ni kweli kwamba kilimo kwanza hakikuwa kipaumbele kwa Nchi yetu, leo na mpaka kesho. Bila Elimu huwezi kufanikiwa pakubwa. kwa jambo lolote lile. Na kuthibitisha kushindwa kwa sera ya Kilimo kwanza, hebu tuambieni Tunda.walau moja linaloashiria Uzuri na umakini wa sera ya kilimo kwanza. Mpaka leo hata kutamkwa tu kwa kilimo kwanza ni nadra na kama ikisikika ikitamkwa basi ni kwa kujutia kama alivyojutia jana Lowassa.

Lowassa pia amesikika akiwataka wale wanaoitumia afya kama kigezo cha kuwachafua wengine na kuwaumarisha wengine waache kufanya hivyo. Na kama wanataka ushahidi wa uimara wa mtu basi watengeneze itaratibu wa kichama kila mtu anayeihitaji nafasi ya Urais apimwe afya yake..!!! Jamani ccm walitaka Lowassa asemeje???

Simkubali Lowassa, lakini siku zote ukweli ni mchungu haijaloshi unasemwa na nani. Na huwa mchungu zaidi pale unapokuhusu wewe.

BACK TANGANYIKA

Umeongea kama mtu huru mwenye kuegemea ukweli....lakini mbona kabwe akisema ukweli huwa unapata ukakasi kuukubali?
 
watanzania tuunganishe nguvu tuitoe ccm madarakani mwaka huu tusidanganyike tena na ccm na zawadi zao mwaka huu vijana tujiandikishe ,walimu tujiandikishe, wakulima tujiandikishe kwa hasira ya kudhurumiwa pesa za mahindi,kahawa,na pamba .wafugaji ,wa machinga onyesheni hasira zenu kwa kuitoa ccm madarakani maana mmenyanyasika sana mama ntilie muda huu mkajiandikishe,wafanyabiashara na wafanyakazi zile kodi tunazo kata tena mwenge tunalazimishwa kuchangia 20000 sasa muda huu si wa kulalamika nenda kajiandikishe ili tuitoe ccm madarakani
 
Muda wa kampeni haujafika mkuu
 
kikwete anahusika na richmond na escrow..jumamosi ndio mboga na ugali unamwagwa...hakuna rangi mtaacha kuona mwaka huu

aione Vuta ni Kuvute(akiwa safarini kanda ya kati) na Foxxxy akiwa Kona Bar
 
Dr Harrison Mwakyembe bado analo deni kubwa kwa watanzania kuhusu suala la Richmond.

Aliwahi kusema kuwa kamati yake haikutaka kusema "mambo yote" (read kuwaambia watanzania ukweli wote), ili kulinda heshima ya serikali. Sasa kwa waliyoyasema, yalitosha kuiangusha serikali baada ya PM kujiuzuru.

Sasa hayo ambayo hawakuyasema ni yepi? Walikuwa wanamlinda nani? Ni vema mambo haya yakawa wazi na huyo mamvi akose cha kujitetea kabisa.
 
Yetu macho na masikio, hivi huyu Mwakyembe atauficha wapi uso wake ikiwa itadhihirika bila chembe ya ukakasi kuwa babu hahusiki na Richmond,, ni vyema basi angalau akamalizia na yale yaliyo nyuma ya pazia
 
Umeongea kama mtu huru mwenye kuegemea ukweli....lakini mbona kabwe akisema ukweli huwa unapata ukakasi kuukubali?

Mkuu Mcubic, heshima yako.

Utakuwa umenisoma kuhusu Zitto kwenye baadhi ya Mada tu na si zote. Mimi ninamkubali sana tu Zitto Kabwe na mara kadhaa nimekwazana na Makamanda wenzangu humu ndani kuhusiana na Zitto. kwani hapo awali mimi nilikuwa mmoja wa wale tuliokuwa tukitaka Zitto na chama wafikie Muafaka nje ya Mahakama lakini kwa bahati mbaya mambo yakaenda mbali zaidi kuliko vile tulivyokuwa tukidhani..!

Mpaka leo mimi niliapa kwamba, Nitamuunga mkono Zitto arudi Bungeni nikirejelea kazi alizozifanya hapo awali akiwa Mbunge. Search hii ipo humu ndani.

Sema kwa siku za hivi karibuni Zitto alianza majidai ambayo mimi binafsi hayakunivutia. Alidai kwamba yeye anang'ang'aniwa na Wananchi wa Majimbo ya Ubungo, Kawe, Kahama na kwingineko. Nahisi hapa ndipo uliponisoma wewe na kuja na hoja yako hii. Ila mimi binafsi bado sijabadiri matamanio yangu kwa Zitto kurudi Bungeni na hili nimekuwa nikilikumbuka ktk sala zangu kila nipatapo nafasi kusali.

Labda uniambie mkuu ukakasi unaodai kwamba mimekuwa nikiuonyesha kwa Zitto ni upi ktk mada Ipi? Pamoja na watu wa Zitto kuwa na dharau nyingi kwa viongozi wetu lakini mimi nimekuwa nikijitahidi kujiepusha na kashfa kumwelekea Zitto, kwasababu ninaamini hawatumi. Kusema huwa nakuwa na ukakasi kwa Zitto naona kama hujanitendea haki mkuu.!

Kiukweli mkuu sina la kusema..umeongea kiuungwana na ukweli kabisa....mkuu tuendeleze gurudumu la kutaka mabadiliko...heshima kwako...
 
Similar Discussions

8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom