Rais Kikwete (mwenyekiti wa CCM Taifa), umepata pa kuanzia

Lowasa kwa nini alikuwa kimya muda wote watanzania hatuwezi kuamini atakachokiongea kuanzia sasa kuhusu richmond .
VOTE FOR UKAWA
Fikiria kama watu sote duniani tukikaa kimya ni nini kitatokea ...Akina Zitto (Buzwagi), Dr. Slaa (EPA), Kafulila (Escrow) nk!! Kitendo cha EL kukaa kimya karibia miaka nane juu ya suala lililoumiza na linaloendelea kuumiza vichwa vya watu ni uhaini mwingine na ishara ya wazi asivyostahili kushika nafasi ya juu.
Niliamini, ninaamini na nitaendelea kuamini kuwa siku moja mmiliki halisi wa Richmond atatajwa hadharani na kuondoa utata wa yule ustaadh aliyejifanya anakagua mitambo pale Ubungo. Safari imefika pazuri!

Ukimtazama EL hatikisiki anapoongea kama kapigwa kipapai tatizo ni nini?
 
Ukimtazama EL hatikisiki anapoongea kama kapigwa kipapai tatizo ni nini?

Makomandoo na wenye uhakika na mambo wanayofanya HAWATIKISIKI...amtikisikie nani..!!? kwani anataka sympathy ya mtu...eboo...mwenzako kajiandaa kisawa sawa...!!! Safari ya matumaini, like Musa kuleee Misri kuvuka bahari ya Sham...CCM yangu hiyoooo...down to earth..!!! Only Lowassa can make CCM alive again...!!!
 
Tatizo ukweli ndio unaokataliwa na ccm, Ukiangalia alichpkisema Lowassa kwa jana ni kweli kabisa. Haiwezekani ktk kashfa kubwa kama ya Richmond ainzishwe na kuhitimishwa na mtu mmoja. Haiwezekani hata kidogo kwamba mkubwa wake wa kazi wakati huo awe hakujua kinachondelea...!!

Na ndiomaana tunaona bila busara za Mkapa kwenye kikao kile cha Nec habari ingekuwa nyingine, na pengine utawala wa Kikwete ingefikia kikomo kwenye NEC ile.

Lakini pia ni kweli kwamba kilimo kwanza hakikuwa kipaumbele kwa Nchi yetu, leo na mpaka kesho. Bila Elimu huwezi kufanikiwa pakubwa. kwa jambo lolote lile. Na kuthibitisha kushindwa kwa sera ya Kilimo kwanza, hebu tuambieni Tunda.walau moja linaloashiria Uzuri na umakini wa sera ya kilimo kwanza. Mpaka leo hata kutamkwa tu kwa kilimo kwanza ni nadra na kama ikisikika ikitamkwa basi ni kwa kujutia kama alivyojutia jana Lowassa.

Lowassa pia amesikika akiwataka wale wanaoitumia afya kama kigezo cha kuwachafua wengine na kuwaumarisha wengine waache kufanya hivyo. Na kama wanataka ushahidi wa uimara wa mtu basi watengeneze itaratibu wa kichama kila mtu anayeihitaji nafasi ya Urais apimwe afya yake..!!! Jamani ccm walitaka Lowassa asemeje???

Simkubali Lowassa, lakini siku zote ukweli ni mchungu haijaloshi unasemwa na nani. Na huwa mchungu zaidi pale unapokuhusu wewe.

BACK TANGANYIKA
 
Mzee Tupatupa nimekuasa kama bintiyo,huko siko waache hao hawajakutana barabarani.Tusonge mbele.Vipi wewe wataka kugombea jimbo gani tujitayarishe kupiga kampeni za kujiandikisha ili usipate taabu ya kupata hizo KURA
 
Hivi richmond Na ESCROW ipi babu kubwa? hivi kuna maamuzi yoyote yanatolewa nchi hii bila baraka za rais na baraza la mawaziri? Mbona Pinda hakuwajibika kwa nafasi yake?

Sasa ndio tunajua tatizo ilikua uwaziri mkuu!!
 
Dah hadi raha aiseee, yaani ukitaka kupunguza stress basi soma hadithi za CCM na CCM wake
 
Kusema ambaye hamtaki yeye ahame Chama hizo ni kauli za dharau na kejeli kwenye Chama na kamati zake.

Hii inaonyesha bila Lowasa Urais CCM haiwezekani.
 
Jiandae kuwa mkimbizi, Edo ndio huyooo October...fanya fasta, sbb mmasai ni warrior by NATURE...not by training...Maasai are naturally warriors...Lowassa si mchezo...anza kujiandaa kwenda Burundi au cjui wapi..!! utajiju, mdomo ulikuponza..!!!
na wewe nani alikuambia Lowassa mmasai?
 
sidhani kama ameponda sera ya kilimo kwanza ila tu ametoa mtazamo wake na kipaumbele chake, si lazima uunge kila kitu mkono hata kama sio priority kwako, nadhani ni haki ya kila mmoja kuamua vipaumbele vyake,katiba inaruhusu pia, +
Thumb Up my sweet dada. Everybody is entitled to his/her opinion !
 
Mzee Mamvi ingawaje ni kubwa la Mafisadi, ila jana kamchana kinoma Prof Samwel Luhanga. Ni aibu sana majirani zetu Rwanda, Uganda na Burundi locked land zisizokuwa na resources za maana zmechepuka, na kutupiga bao na bado znasonga na znafanya vizuri. Ama kweli serikali ya mr dhaifu ilikuwa ni legelege cjapata kuona, thanks God tumesota miaka 10 ya taabu na hatimaye sasa tunahesabu miezi kadhaa, tupumue ndani ya serikali makini ya UKAWA.
 
unnamed%2B%252852%2529.jpg
 
kama Lowasa hajahusika atuambie nani alihusika kwakuwa yeye ndiye alikuwa waziri mkuu kwahiyo bila kutuambia nani mhusika wa richmond basi Lowasa ndiyo anahusika.

Na wewe ndiye labda ujuaye haya yoote! Huko chamani huwa hamli kwa pamoja?
 
Tatizo ukweli ndio unaokataliwa na ccm, Ukiangalia alichpkisema Lowassa kwa jana ni kweli kabisa. Haiwezekani ktk kashfa kubwa kama ya Richmond ainzishwe na kuhitimishwa na mtu mmoja. Haiwezekani hata kidogo kwamba mkubwa wake wa kazi wakati huo awe hakujua kinachondelea...!!

Na ndiomaana tunaona bila busara za Mkapa kwenye kikao kile cha Nec habari ingekuwa nyingine, na pengine utawala wa Kikwete ingefikia kikomo kwenye NEC ile.

Lakini pia ni kweli kwamba kilimo kwanza hakikuwa kipaumbele kwa Nchi yetu, leo na mpaka kesho. Bila Elimu huwezi kufanikiwa pakubwa. kwa jambo lolote lile. Na kuthibitisha kushindwa kwa sera ya Kilimo kwanza, hebu tuambieni Tunda.walau moja linaloashiria Uzuri na umakini wa sera ya kilimo kwanza. Mpaka leo hata kutamkwa tu kwa kilimo kwanza ni nadra na kama ikisikika ikitamkwa basi ni kwa kujutia kama alivyojutia jana Lowassa.

Lowassa pia amesikika akiwataka wale wanaoitumia afya kama kigezo cha kuwachafua wengine na kuwaumarisha wengine waache kufanya hivyo. Na kama wanataka ushahidi wa uimara wa mtu basi watengeneze itaratibu wa kichama kila mtu anayeihitaji nafasi ya Urais apimwe afya yake..!!! Jamani ccm walitaka Lowassa asemeje???

Simkubali Lowassa, lakini siku zote ukweli ni mchungu haijaloshi unasemwa na nani. Na huwa mchungu zaidi pale unapokuhusu wewe.

BACK TANGANYIKA

Leo ndio akili zinamrudia alikuwa wapi huyu msanii mwingine tu!
 
Acheni kumsakama huyu mzee bila sababu za msingi, kumbuka Lowassa na Kikwete hawakukutana barabarani...
 
Back
Top Bottom