Rais Kikwete mbona hajaenda kuwashukuru wapiga kura wake?

Landala

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
997
473
Ni miezi kama sita imekwisha pita toka rais Jakaya Mrisho Kikwete achaguliwe kuongoza Tanzania kwa awamu ya pili,swali ambalo wananchi wengi wanajiuliza ni kuwa mbona toka achaguliwe hajafanya ziara hata mkoa mmoja kwenda kuwashukuru wapiga kura wake waliomrudisha tena madarakani?Jk nakushauri ulitafakari hili kwa umakini na uchukue hatua,mbona safari za nje anaenda,je nje ndio walio mchagua awaongoze?Yeye kazi yake imebaki kulalamika tu pale white house hata wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa ameshindwa kuteua.
 
mambo yanayotokea wanachi kuwabonda viongozi linamtisha sana rais wetu,ndugu zangu watanzania tubadilike tupende viongozi wetu!!
 
Nadhani hii iko wazi kabisa! Si unajua matokeo alichakachua kwa hiyo anaogopa wananchi watamuuliza aliko toa kula za kumfanya kuwa mshindi.
 
Tuache kumuandama kwa Baba wa watu!
Mbona alifanya ziara dodoma, mbeya na musoma?! au unataka aende nyumbani kwako ndo ulidhike kuwa amefanya ziara?
 
Ni miezi kama sita imekwisha pita toka rais Jakaya Mrisho Kikwete achaguliwe kuongoza Tanzania kwa awamu ya pili,swali ambalo wananchi wengi wanajiuliza ni kuwa mbona toka achaguliwe hajafanya ziara hata mkoa mmoja kwenda kuwashukuru wapiga kura wake waliomrudisha tena madarakani?Jk nakushauri ulitafakari hili kwa umakini na uchukue hatua,mbona safari za nje anaenda,je nje ndio walio mchagua awaongoze?Yeye kazi yake imebaki kulalamika tu pale white house hata wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa ameshindwa kuteua.
Awashukuru kwani walimchagua yeye alishawashukuru tume ya uchaguzi Nec inatosha.
 
Si aliiba kura jamani,yeye huwa anakwenda kuwashukuru tume ya uchaguzi waliomsaidia kuiba kura.
 
mambo yanayotokea wanachi kuwabonda viongozi linamtisha sana rais wetu,ndugu zangu watanzania tubadilike tupende viongozi wetu!!
Mwacheni raisi wetu achape kazi muda wa yeye kutidha maandamano haupo nyie cdm ndio mnatakiwa kwenda kutoa shukrani kwa hicho kidogo mlichopata kwa bahati
 
anashindwa kuwatembelea wananchi wake na kupiga picha na watoto, na walemavu mana hiyo haina tija tena kwani yeye si ameshapat ailichokuwa anakitafuta. tumsubiri rais mwingine lakini kwa huyu wa sasa hakuna haja tena ya kuumiza vichwa mana maisha bora kila mtanzania yamekuwa kama hadithi za abunuasi ! poleni wote mliompigia kura, na hilo liwe fundisho kwa wenye kun'gang'ania chama badala ya mtu!
 
Mwacheni raisi wetu achape kazi muda wa yeye kutidha maandamano haupo nyie cdm ndio mnatakiwa kwenda kutoa shukrani kwa hicho kidogo mlichopata kwa bahati

Hiyo sasa ni chuki kwani mada inazungumzia Chadema?Nenda ktk mada husika acha kuwashwa na Chadema.
 
Jamani si tumeonywa mambo kadhaa tusihoji likiwemo ili la raisi na Uraisi wake....mkuu hapo juu anasema eti JK hana haja ya kwenda kuandamana kama CDM,hii inamaana kwamba watanzania hawakuichagua ccm bali waliichagua CDM hivyo ndo wanaotakiwa kwenda kushukuru japo..teh teh teh teh teh
 
Awashukuru kwani bado anawahitaji?, wewe kama unasubiri kuja kushukuriwa umeula wa chuya. Kingine akija kuwashukuru mtajitokeza kama mnavyofanya kwa CDM?. Acha apige kazi kuwatumikia watanzania mlomchagua na ambao hamkumchagua ikiwa pamoja na kuwashughulikia mafisadi.
 
km that tym alitupiwa mawe this tym si ndio atachapwa bakora kabisa? Mh. endelea kutulia magogoni tu!
 
Anaogopa kuanguka hadharani jamani, na sasa majini yaliyokuwa yanamlinda yamesepa baada ya muundaji wake kuvuta.Tehe tehe tehe...
 
Mbona alishawashukuru TISS,Tendwa na NEC tayari! Kuna wengine waliomuweka madarakani?
 
Tuache kumuandama kwa Baba wa watu!
Mbona alifanya ziara dodoma, mbeya na musoma?! au unataka aende nyumbani kwako ndo ulidhike kuwa amefanya ziara?

Hapo palipowekwa rangi ya njano tuthibitishe tarehe zipi na alitembelea sehemu ipi ya Mara/Musoma
 
Kutokana na hilo wanaCCM wamekuwa wanyonge, na siku akija kutoa shukrani hali itakuwa mbaya maani bei ya unga itakuwa 1000 hivyo kuweka uwezekano wa kutupiwa mawe. Ni bora asiende tu.
 
Ni miezi kama sita imekwisha pita toka rais Jakaya Mrisho Kikwete achaguliwe kuongoza Tanzania kwa awamu ya pili,swali ambalo wananchi wengi wanajiuliza ni kuwa mbona toka achaguliwe hajafanya ziara hata mkoa mmoja kwenda kuwashukuru wapiga kura wake waliomrudisha tena madarakani?Jk nakushauri ulitafakari hili kwa umakini na uchukue hatua,mbona safari za nje anaenda,je nje ndio walio mchagua awaongoze?Yeye kazi yake imebaki kulalamika tu pale white house hata wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa ameshindwa kuteua.

Mkuu Landala,
Hata JK anajua kuwa hakupigiwa kura za kutosheleza kuwa Raisi wa nchi yetu. Anaelewa A to Z kilichotokea hadi akarudi hapo Magogoni. Haoni kama kuna umuhimu wa kwenda mikoani kuwashukuru wananchi kwa sababu hawakumchagua yeye kuwa Raisi halali. Anajua anachokifanya.
 
Back
Top Bottom