SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 43,707
- 60,758
Siyo siri kuwa muasisi wa siasa za maji taka hapa Tanzania ni JK na genge lake la wanamtandao. Mbinu hii aliizanza mapema kabla ya uchaguzi wa mwaka 2005, na wahanga wakubwa wa siasa hizi za kishenzi ni Fredrick Sumaye, Salim A. Salim, Prof.Mark Mwadosya na wengineo, na wahanga hawa walilengwa kwani walionekana kuwa tishio kwa malengo ya JK kuukwaa urais hivyo ilikuwa lazima wachafuliwe kiasi cha kutosha ili wanuke na wakati huo magazeti yakimpamba JK kwa sifa asizostahili, na kweli mbinu hii ya kishenzi ilifanikiwa na JK akawa rais.
Mwaka huu kwa vile kanuni za CCM zilikuwa zinamlinda JK asipate mpinzani toka ndani ya chama hicho hakuwa na haja ya kutumia mbinu hiyo na akawa anajiandaa kushinda kwa kishindo, lakini ghafla upepo ukabadilika baada ya mzalendo wa kweli Dr Slaa kuteuliwa na Chadema kugombea nafasi ya urais, JK baada ya kuona kuwa maji ni marefu kwake na chama chake akarudia tena mbinu yake ya maji taka na ndipo zikasikika habari za Dr Slaa kuchukuwa mke wa mtu, lakini kwa vile watanzania wa leo siyo wale wa mwaka 47, waliimpuuza JK na siasa zake hizo chafu wakaendelea kumuunga mkono Dr Slaa.
Baada ya JK na genge lake kuona kuwa mbini hii haifanyi kazi akaamua kutumia SILAHA YA MAANGAMIZI - UDINI.
Ukazushwa uvumi kuwa Dr Slaa ametumwa na Kanisa Katoliki, mbinu hii ilikolezwa na magazeti ya fisadi Rostam Aziz na mengine kama Habari Leo, AL HUDA, AL NUR, na kama haitoshi zikatumwa sms kwa mamilion ya wapiga kura kumchafua Dr Slaa na kuhusisha na udini.
Siyo siri kuwa silaha hii imeacha majeraha mengi miongoni mwa Watanzania na mfano hai ni hata hapa jamvini hangover ya siasa hizi za udini zilizo asisiwa na Kikkwete mwenyew e ipo. Dini ni jambo nyeti sana na likitumiwa vibaya linaweza kuilipua nchi nzima na hiki ndicho alichokifanya JK.
NATOA MWITO KWA WACHA MUNGU WOTE TUOMBEE NCHI YETU IONDOKANE NA SUMU ILIYOMWAGWA NA JAKAYA MRISHO KIKWETE