Rais Kikwete kuwasili Houston na msafara wa kitajiri Oktoba 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete kuwasili Houston na msafara wa kitajiri Oktoba 3

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kinepi_nepi, Sep 15, 2009.

 1. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Raisi wa Jamhuri ya Watu wa Tanzania atawasili Houston, Texas USA kwa ziara ya siku mbili kuhudhuria ufunguzi wa DICOTA iliyoandaliwa na baadhi ya watanzania waishio marekani wakishirkiana na balozi Sefue. Dicota inasemekana ni mchakato wa kukusanya na kutafuta wawekezaji walioko Marekani na kuwaunganisha na Tanzania.

  Wanaohudhuria mkutano huo ni pamoja na balozi Sefue balozi wa tanzania nchini marekani pamoja na maofisa ubalozi, Bernard Membe waziri wa mambo ya nje wa Tanzania, Mr Emmanuel Ole Naiko(TIC) na msafara wa raisi na ule wa waziri wa mambo ya nje pamoja na TIC.

  Ni mwaka mmoja tu tangu kikao cha kwanza cha chombo hiki kufanyika nchini marekani jijini Houston na iliwahusisha maofisa mbali mbali kutoka tanzania na ubalozi wa Tanzania nchini marekani, na safari hii karibu sura zote zinarudi tena houston safari hii na raisi anaonekana atajumuika nayo. Chanzo cha habari hii ni mwaliko uliopo kwenye website ya DICOTA inayoonyesha wageni wote waalikwa akiwemo mheshimiwa raisi.

  Safari hii ni mjumuiko wa safari za Raisi zinazopigiwa kelele nyingi na watanzania kuwa amekuwa na safari nyingi zinazoitia nchi hasara. Kumsafirisha Raisi wa nchi kwa ajili ya ufunguzi ni gharama kubwa sana kwani fedha anazotumia yeye na msafara wake ungeweza kujenga clinic kadhaa nchini.

  Mkutano wa kwanza uliofanyika Houston inasadikika ulifadhiliwa na fedha za walipa kodi wa tanzania na kusafirisha viongozi mbalimbali kutoka ubalozini na TIC tanzania, na hakuna anayejua ni kiasi gani kilitumika. Au nini walikiongea au walikipata. Hii imekua ni kawada ya nchi yetu kutumia fedha za walipa kodi bila ya kutangaza matokea ya matumizi hayo kwamba tumeliwa au tumepata faida.

  Habari za kichunguzi zinaonyesha kwamba huu ni mradi wa baadhi ya viongozi wa kutengeneza safari za nje kwa kisingizio cha mikutano na hivyo kujiongezea vipato kwa ile staili ya malipo ya safari na kujikim pamoja na marupurupu ya safari. haiingii akili kama nia ni kuwapata wafanyabiashara, kwa nini balozi asifanye hizi kazi na kutembea sehemu mbali mbali ndani ya eneo lake la kazi na kutangaza nchi huku akitoa maelezo ya maeneo ya uwekezaji. Kwanini kuhamisha wizara na taasisi za kiserikali na kutumia gharama kubwa kila mara kwa kisingizio cha kutafuta wawekezaji.

  Kinacho shangaza ni pale viongozi wanzilishi wa chombo hiki pamoja na Balozi sefue kwa makusudi kutowaambia watanzania kupitia vyama vyao vya majiji na majimbo ya Marekani kwamba chombo hiki kimeanzishwa. Inaonekana kwa sasa wanahitaji watanzania kuhudhuria sana mkutano huu ili kujaza ukumbi. Wanzania waishio Marekani wanasema kuna vyama vya watanzania vingi Marekani na kama vingeshirikishwa zoezi hili lingeweza kuwa na manufaa zaidi. Kwani watanzania wengi wanafanya kazi mbali mbali kwenye makumpuni mbalimbali na kuwa na info tofauti. Viongozi wa vyama vya watanzania wanashangaa kwa kutoshirikishwa kulitafutia Taifa wawekezaji na Balozi Sefue kuamua kutafuta kajikundi kwa ajili ya kupitishia sera zake.

  Tangia waanzishe DICOTA na kuleta ujumbe mzito sana je ni mangapi tayari yamefanikiwa au wawekezaji wangapi wamepatikana na kuona uwezekano wa kulipa gharama zinazotumika za mamilioni ya shilingi kwa kisingizio cha utangazaji.

  Wakati viongozi wanchi wakinadi kutafuta wawekezaji huku nyumbani umeme hautapatikana kwenye mikoa kama sita hivi, Mwanza, Kilimanjaro,Dodoma,Arusha, Shinyanga na Tabora. Tatizo la umeme naona linakuwa sugu. Ni mwekezaji gani atawekeza gizani?

  Wazo la DICOTA ni zuri sana na linaweza kuisaidia nchi kwa kiwango kikubwa, ila likiendeshwa kiutapeli au kiujanja ujanja linaweza kuliiingizia Taifa gharama kubwa sana.

  Naomba kutoa hoja.
   
 2. O

  Ogah JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Karibuni kiwanja Wakuu
   
 3. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Sijaona hata umuhimu wowote wa yeye kama rais kuwepo kwenye huo mkutano wa DICOTA. Hiyo DICOTA yenyewe yangu macho!!!!
   
 4. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Labda ujio wa kina Abromoavich..will smith ..watu kibao kuja bongo pamoja na kanye..

  anyways..Mkulu anapenda issue za namna hiyo...alafu kwa wale ambao hamkupata Nafasi ya kumuuliza swali ukimpigia anytime anapokea hasa muda wa jioni...
   
 5. K

  Keil JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii ni njia nyingine ya kutuletea wawekezaji wababaishaji wa jamii ya IPTL, Richmond, NetGroup na wengineo. Ni mradi mwingine wa ufisadi ambao unaandaliwa kwa ajili ya lala salama ya JK, 2011 - 2015. Ukishaona siasa inaingizwa kwenye uwekezaji basi hapo lazima kuna ufisadi unaandaliwa ama kuna wawekezaji njaa wamepatikana ila hawana confidence kama wanaweza kufanya biashara Tanzania, na hivyo wanahitaji watu walio na connections ili wawashike mikono kwenye kufanya madudu yao (ufisadi wa mikataba mibovu).

  Mfano, Ami Mpungwe, alikuwa balozi wetu Sauzi, baada ya kuwa-identify makaburu ambao ni potential investors, aliwashika mikono na kuwaleta Tanzania. Hayo aliyafanya baada ya kuomba kustaafu kabla ya umri ili afanye kazi zake. Already the guy had connections na alijua anaanzia wapi na kuishia wapi. Leo hii jamaa yuko kwenye bodi nyingi za makampuni ya makaburu ambayo yana asili ya Sauzi. Na kuna baadhi ya makampuni ana hisa kwa kuwa aliwekeza "technical know who".

  Sasa huo mtandao wa watanzania wanaotaka kutuletea wawekezaji, hivi ni lazima JK aende US kuhudhuria mkutano wao? Kwa kipi hasa? JK anaacha kazi zake anakwenda kwenye mkutano ambao hana hakika kama utakuwa productive au la, kwanini asitume mwakilishi? Ama ndio zile sehemu ambazo alikuwa akisema juzi kwamba, "asipoenda yeye mwenyewe, basi Tanzania hatuwezi kupata kitu". Kwamba asipoenda kwenye huo mkutano basi wawekezaji hawawezi kuja Tanzania.

  Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza, Tanzania hata tuanzishe mitandao hiyo kweye nchi zote za Ulaya Magharibi, Marekani, Canada na Japan, hatuwezi kupata wawekezaji genuine iwapo hatuna miundo mbinu ya uchumi, vitu kama reli, barabara, airport, umeme, bandari na mawasiliano. Tutaendelea kupokea wawekezaji uchwara watakaokuwa wanatuingiza kwenye mikenge kila siku kwa kuwa wanajua kwamba mazingira ni magumu na inawezekana wasipate faida, kwa hiyo njia pekee ni kuomba wanasiasa wakubali mikataba mibovu ambayo haina maslahi kwa Taifa. Kampuni inakuja ikijua kabisa kwamba sasa ni zama za soko huria, lakini bado inataka ipewe upendeleo wa kubaki yenyewe tu bila mshindani kwa miaka 25, mfano ni akina TICTS. Tumeingizwa kwenye hiyo mikenge na watu kama akina Karamagi ambao walikuwa na connections na ndiyo jamii hiyo hiyo inajifanya imeunda mtandao wa kusaka wawekezaji na kumbe wanatuletea ufisadi mwingine na kuharibu hata kile kilichokuwepo.

  Haya ndiyo ambayo yametuletea akina RITES ambao badala ya kuleta ahueni wamekuwa ni mzigo kwa serikali na hatima yake haijulikani. Tanzania tutaendelea kukamuliwa hivi hivi kila kukicha kwa sababu ya kuendekeza politics kwenye mambo yanayohitaji taaluma ya fani inayohusika.
   
 6. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hakuna kitu kipya zaidi ya kufanya safari kama hizi, na pia itakuwa ni busara kwa Jk kubaki na kubuni mbinu nyingine za kupata wawekezaji na kukusanya kodi kubwa sana toka ndani, na pia ni jambo la ajabu kuona kuwa VIcoda ndio wanampeleka huko,Sijakubaliana na jambo hili hata kidogo
   
 7. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Masikitiko yangu makubwa ni kwamba hii Diaspora hailengi sababu kubwa zilizofanya nchi zilizoendelea kuendelea hasa zile zilizotumia rasilimali watu waliopo nje ya nchi zao. Ni ukweli usiopingika wawekeza hawasaidii sana kufanya nchi kuendelea zaidi ya kuchuma na kuondoka.Wawekezaji wengi ni sawa na wakoloni tofauti ni mazingira.Kila mwekezaji ana malengo yake ya kuchuma kwa muda gani na kisha kurudi kwao akiwa tajiri hiyo ndio nia ya wawekezaji wengi.

  Diaspora zilizotumika kuendeleza, Israel, Italy, Singapore, Malyasia nk. Hawa walitumia wananchi wao waliohamia nchi nyingine na kupata utaalamu mbali mbali, ujuzi naudhoefu katika nyanja mbali. Wahamiaji hawa walipata elimu, na mitaji kwenye nchi walizokuwa wakiishi. Baada ya nchi zao kugundua hilo walitengeneza network ili kuwajua na kuwavuta nyumbani kuwatumia kujenga nchi zao. Hii ni kuanzia fundi mchundo mpaka profesa. Nchi hizi zilitengeneza njia nzuri ya kurudisha mtaji nyumbani na kutoa ushirikiano mzuri sana.

  Ukiangalia mtawanyiko wa Tanzania wengi duniani kuanzia Japani, china, Australia, Uingereza, Marekani nk wengi wao wamepata utaalamu mwingi sana wa mambo mbalimbali.Wapo wenyeuwezo wa kuassemble magari, kompyuta, ndege, meli,nk na wapo wenye uwezo wa usanifu wa vitu hivyo, wapo maprofessa, wapo phds, wapo degree, diploma, highschool nk.

  Kama hawa watu wametumiwa na nchi tajiri na kuzifanya kuwa tajiri madufu, na kazi zao ndizo zinazotufanya kwenda hizo nchi na kutafuta eti wawekezaji, kwanini tusitumie hawa wataalamu tukatengeneza wenyewe.

  Mfano wapo watanzania wengi wenye uwezo wa kutengeneza magenereta makubwa ya kufua umeme ambayo yanatengezwa na makampuni kama GE, Cuttlerhammer, nk. Kama hawa watahakikishiwa mitaji na ushirikiano wakitumiwa vizuri matatizo ya umeme leo yangekuwa historia. Tuna wasanifu wazuri wa uchoraji na mainginia kama hawa wangetumiwa vizuri tatizo la barabara na msongamano lingekuwa historia.

  Sasa badala ya diaspora kufanya mambo kama haya ya maana tunarudi pale pale eti watafutwe wawekezaji, kwani ninyi watanzania mliopo ulaya na marekani hamwezi kufanya wanayofanya huko mlipo , tofauti ya kukaa ulaya na marekani na Tanzania ni nini? Kweli mpaka waje wakope bank zetu halafu wafanye. Mbona msikae mkatoa utatuzi tatizo likawa fedha? Kwani nani kasema tatizo la Tanzania ni fedha?
  Tatizo kubwa la Tanzania ni kupata watu wenye uwezo wa kufikiri sawa sawa na kutenda kutoa majibu yanoyotakiwa.

  Inashangaza kuona PHDs holder tena mainginia nao wako kwenye bakuli la kuomba yala badala ya kutoa mwongozo na kusema nini wanaweza. Ni kwanini wasomi wetu hawajiamini mara pale wanapostaafu kazi ambapo waliweza kuwafanyia wazungu mambo makubwa ila tunaporudi nchini kwetu wanarudi kuwaomba hao wazungu eti wawasaidie, kwanini wasiombe fedha kwenye serikali zao na kuziambia ni nini wanaweza kufanya kutatua tatizo A, B, C............Najua tatizo ni wanasiasa, ila wenzetu waliweza kwa kutoa kauli na vitendo vyenye mshindo wa dhati.

  Leo hii wasomi nao wanatafuta mwekezaji wa kutengeneza jembe, Trekta, au kuchimba madini wakati wao walifanya sana wakiwa kwenye hayo makampuni.

  Tanzania inahitaji kujua hatuwezi kuendelea kwa wawekezaji wanaotuachia asilimia tatu, wala hatuwezi kuendelea kwa wawekezaji wafanyabiashara. Ni lazima kuanza kufikiri kama wao na kutenda kama wao, haihitaji mtaji mkubwa sana, bali serikali kuelewa mtaji pekee iliyonayo na wananchi wake majasiri na wananchi kujua kwamba wao ndio serikali. Lets go lets do it time is now.
   
  Last edited: Sep 15, 2009
 8. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  well nchi hii bado ni 'BIKIRA' i can say,tuna vyanzo vingi sana, resources nyingi sana(hapa ni watu pamoja na vitu/malighafi).inakuwaje aende marekani?wamarekani wenyewe watakuja kama mazingira ya kazi yanavutia,sijaona mtu kulazimishiwa kwenda mahali kufanya biashara wakati mwekezaji mwenyewe anafanya market research atatupata tuu.JK abaki nchini kwa 90% ya mua wake,naamini akisimamia miradi ya humu ndani yeye paersonally italeta faida zaidi kuliko kuenda USA personally kwa gharama kubwa bila faida,hakua business man atarisk kuleta hela yake hapa wakati umeme,maji,barabara,elimu vyoote unreliable.Nilisema nchi hii kuna watu wanawaza kuezeka wakati hata ukuta haujajengwa!tujenge kuta na kuimarisha msingi then tutapaua kwa wakati muafaka!Otherwise JK namwona kama lyfist flani hivi!!
   
 9. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hapo kwenye red umenikuna mwanangu per diem zinatuua watanzania JK kaziba masikio kwenye suala la umeme toka mtambo wa rafiki yake ukataliwe maneno ya Idriss Rashid sasa tunaanzxa kuyaona tutajuta
   
 10. C

  Chongowela Member

  #10
  Sep 15, 2009
  Joined: Sep 5, 2008
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lo. Mpaka huyu Sind Bad aondoke IKULU, NCHI ITAKUWA IMEFILISIKA! Sijui tufanyeje.
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huu wizi mtupu.
  Mmetudanganya kwenye sulivan tukapanda mawe hakuna tulicho vuna sasa mnapanda hiyo nayo dah kweli waTZ kiboko kwa kutafuna chaneli za kupatia pesa dah.
   
 12. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sehemu ambazo anakwenda kuomba misaada ya chandarua? Badala ya kuomba misaada ya kujenga viwanda vya vyandarua ambavyo vingeweza kutuhakikishia kuwa na vyandarua hivyo kwa wingi na kwa muda mrefu zaidi, anajivunia kuomba ugali gengeni.

  Wakati mwingine tunaomba mambo ya kutudhalilisha sana. Viwanda ndivyo vinavyohitajika nchini, sio vyandarua ambavyo kesho vitakuwa majalalani na matatizo yetu kubaki pale pale.

  Kweli kabisa Keil.
  Hakuna mwekezaji wa kweli atakaekuja nchini na kuwekeza pesa nyingi na kuwa makini bila kuona na kuamini kuwa mazingira ya nchi yetu yanaweza kuhimili na kumuwezesha kupata mapato mengi na ya muda mrefu. Bila kupata uhakika huo, ataishinikiza serikali kulinda uwekezaji wake kwa ku-compromise sheria za nchi na rasilimali zake. Hapo ndipo serikali inapojikuta ikisaini mikataba ya kijinga.

  Nchi yetu inatakiwa iweke vipaumbele katika mambo muhimu ya maendeleo. Iangalie matatizo yaliyopo, na iyatafutie utaratibu wa kudumu wa kuyatatua moja kwa moja na kwa utaratibu wa kudumu. Haiwezekani mwekezaji akaja nchini akijua kuwa masaa mengi nchi haina umeme wa kutosha (kwa mwaka). Hawezi kuja akijua pia kwamba, nchini hakuna Bank inayoweza kumhakikishia flow nzuri ya pesa zake na kukidhi mahitaji yake kifedha. Hawezi kuja akijua pia kuwa, hakuna wataalam waliobobea na wa gharama nafuu wenye uwezo wa kufanya kazi nae. Hawezi kuja akijua kuwa, viongozi wa serikali wanapenda kutembeza bakuli, hasa kila ifikapo uchaguzi mkuu. Hawezi kuja akijua hakuna barabara, hakuna hospitali, hakuna usalama wa kuaminika wake yeye na mali zake. Nchi yetu iko categorized katika class ndogo sana ya uwekezaji.

  Hata Rais akienda wapi haitasaidia. Kitakacho saidia ni jitihada za ndani kurekebisha hali. Kinachofanywa na mikutano kama hiyo sijui ya DICOTA, ni namna ya lobbying tu kwa decision makers wetu. Haina nia tofauti. Wenzetu huko wanatengeneza pesa kuwaunganisha wafanya biashara hao.
   
 13. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #13
  Sep 15, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kuna siku tutajua tu sababu haswa za safari za JK kwenda USA, wawekezaji hawatoki US tu asitudanganye, kuna kausanii ka waTZ walioko US wanacheza na huyu bwana, hebu angaliza hata wakati alisema alienda kuonana na Obama, alikuwa kuwa kule kabla na baada na hata meeting yao ilikuwa very brief lakini aliendelea na ziara zisizo na tija US.
  huu si wakati wa yeye kukimbia nchi...kuna matatizo mengi ambayo angeshuhurikia hata hao wawekezaji wangefurahia;
  1. angeangalia kwanza mwenendo wa wawekezaji waliopo sasa na manufaa yaliyoluwepo, matatizo wanayopata na wanayotoa kwa taifa, kampuni za madini, richmond/dowans, TRL....
  2. aonyeshe kwa vitendo mapigano dhidi ya rushwa, ufisadi....kesi za epa,uhujumu uchumi, asisingizie mahakama kwakuwa kuna zingine zipo kwenye uwezo wake.
  3. ujenzi wa miundombinu, ni aibu mpaka leo hii umeme ni tatizo nchini kwetu.
  4. aangalie hizi dalili mbaya za kisiasa nchini, pemba, ccm na ufusadi....waraka wa kanisa, mwongozo wa shura ya maimamu....nchi inaenda wapi na kwanini?

  kwa ujumla mi naona JK anamengi ya kufanya kuliko kwenda nje, asijeakalaumu wananchi watakapo anza kutafuta au kufikiria mabadiliko ya uongozi nchini....

  "watanzania ni wajasiri ila wanahitaji motivation kidogo..."
   
 14. Companero

  Companero Platinum Member

  #14
  Sep 15, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hivi mnajua Birthday ya Libra JK ni lini?
   
 15. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #15
  Sep 15, 2009
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35


  hili ni bonge la point. nchi nyingi zinatumia watu wake waliopata ujuzi nje kuendeleza ndan mwao, Tanzania ingekuwa na busara wapo WA TZ wengi wenye ujuzi ingewatumia hawa leo hii hata makandarasi wa barabara wangekuwa wabongo tu, lkn tatizo ni Percent mtu kutoka nje ataombwa Percent ili mkataba wake upitishwe lkn Mbongo itakula kwake Mengi R case study Campisky Hotel.
   
 16. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #16
  Sep 15, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  HIVI HII DICOTA HAIFANANI NA KITU KINGINE ILIYOWAHI KUFANYIKA UK????


  Tanzania Diaspora and Skills Forum

  His Excellency President Jakaya Mrisho Kikwete has kindly agreed to launch Tanzania Diaspora and Skills Forum in London on the to be the 18th April 2008.


  President Kikwete will deliver the keynote speech at the one day event to be held at the Savoy Place at the first Ever Tanzania Diaspora and Skills Forum to be held in London , United Kingdom.

  The proposed conference organised by Tanzania High Commission, Tanzania Association UK and Africa Recruit is aimed at mobilizing and engaging the Tanzanian Diaspora, particularly in Europe and mainly in the United Kingdom to ensure that there is greater skills utilisation and investment by the Diaspora communities to the country.
  During the conference, key speakers will be invited from Tanzania and the Diaspora to inform and engage these groups on the various opportunities in the country.
  To register for the forum click below:
  http://africarecruit.com/Tanzania_Event/index.php

  Target Audience
  Tanzanian Diaspora
  Private Sector from Tanzania
  Government Officials
  Donors/Multilateral organisations
  Diaspora Media
  Engaging Skills of the Diaspora in Tanzania

  The knowledge and skills of the Diaspora is an additional source of engagement for countries to tap into in building the capacity and capabilities of organisations and ultimately the country. The event is aimed at galvanising the Tanzanian Diaspora of all generations in harnessing their skills, knowledge and investment in the continued economic development of Tanzania.

  AfricaRecruit survey of the Diaspora in 2006 indicated that over half left Africa for career professional reasons with a least over 70% of the respondents indicating that they had plans to return back home at some point in time and will like to explore how they can use their knowledge and skills in their country of origin development. Creating an environment to engage directly with potential employers will enable the Diaspora to make informed decisions.

  The Diaspora confrence aims to fulfil key Government mission of endeavouring to create a platform of universal inclusionfor Tanzanian Diaspora Communityin the United Kingdom and Europe, so that they participate in the development of their country.
  It will also host specific sessions devoted to employment opportunities in Tanzania, cost effective migrant remittances, how to engage with the host government and systems, role of the Diaspora in the development of Tanzania, issues relating to Brain Drain and Reversal thereof, the case for dual Citizenship, Investment opportunities in both Tanzania and the UK, opportunities in both Tanzania and the UK, opportunities to market Tanzanian products in the United Kingdom , methods of productive access to the Government and other institutions back home and , crucially how to create and maintain a conact network.
   
 17. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #17
  Sep 15, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kule UK wajanja akina J Pinto walileta haya haya leo ni Mkugrnzi wa Jambo kashidwa TZ kaenda UK kachukua pesa za wa TZ kaja kuwekeza na katulia sasa . Dicota nayo mtasikia endeleeni kufuatilia . Mwaka 2010 inaleta shida sana .
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Sep 15, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Miafrika mipumbavu sana! Basi kwenye hilo limkutano lao mijitu itajipendekeeeza weeee.....yaani Miafrika mijinga sana
   
 19. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #19
  Sep 15, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  October 3 nitakuwa nabeba mabox, ningezuka.
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Sep 15, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Kutakuwa na pilau?
   
Loading...