Rais Kikwete kuongoza uzinduzi wa Jiji la Arusha

Spike Lee

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
625
272
Wana JF.
Rais Jakaya Kikwete, kesho atazindua rasmi Manispaa ya Arusha kupanda hadhi kuwa Jiji, eneo la Mnara wa Azimio la Arusha na kuhitimisha kwa kuhutubia wananchi kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid. Meya wa Arusha, Gaundance Lyimo alisema uzinduzi huo pia utahusisha kuzindua maboresho ya miundombinu na ujenzi wa barabara kadhaa kwa kiwango cha lami unaondelea.

Pia Arusha wameweka mikakati ya kujenga jengo la kisasa litakalohudumia zaidi ya wafanya biashara 6,000 katika eneo la Kilombero maarufu kama Stendi ya Samunge na lingine katika eneo la kwa Mrombo, maarufu kwa biashara ya mbuzi.

Pia wanaendelea na mpango wa wa kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwa kujimba visima na mabwawa katika kata zote 19 za Jiji la Arusha, mpango unatakiwa kutekelezwa kupitia Benki ya Dunia.

SOURCE; MWANANCHI OKTOBA 31 2012
 
Hongera Chadema,miaka yote walizoea wapa mirungi watu pale bondeni na pangani.
 
Back
Top Bottom