Rais Kikwete kufungua benki ya wanawake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete kufungua benki ya wanawake

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MaxShimba, Sep 1, 2009.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Rais Kikwete kufungua benki ya wanawake Ijumaa Dar[​IMG]Na Sadick Mtulya

  RAIS Jakaya Kikwete atazindua rasmi huduma za Benki ya Wanawake nchini (TWB) Ijumaa.


  Pamoja na mambo mengine, Rais Kikwete atafungua rasmi huduma maalumu ya akaunti ya wajasiriamali wa aina zote.


  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Tamasha la Wanawake Wajasiriamali Tanzania (TWWT), mkurugenzi mtendaji wa TWB, Margareth Mattaba Chacha alisema Rais Kikwete atafanya uzinduzi huo saa 3:00 asubuhi.


  “Pamoja na kuwa shughuli za kibenki kuanza mwezi mmoja uliopita, Ijumaa Rais Kikwete atafungua rasmi huduma hizo ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa akaunti ya maalumu ya wajasiriamali wa aina zote,” alisema Mattaba

  Mattaba alisema TWB inatarajia kufikisha mtaji wa Sh6 bilioni mara tu baada ya akaunti ya huduma ya wajasariamali kuanza.


  “TWB ilianza na mtaji wa Sh2.5 bilioni lakini mara baada ya akaunti maalumu ya wajasiriamali kuanza tunatarajia mtaji wetu kukua hadi Sh6 bilioni,” alisema Mattaba.

  Mkurugenzi huyo alisema hadi kufikia juzi wateja walishafungua akaunti 1645 za aina mbalimbali katika benki hiyo na kwamba asilimia 75 ya waliofungua akaunti hizo ni wanawake.


  Awali, Mattaba alisema TWB inajiandaa kutoa mafunzo mbalimbali ya matumizi ya kibenki kwa wanawake ili wapate changamoto ya kutumia huduma zitolewazo na mabenki nchini.

  Alisema ukosefu wa elimu pamoja na kutojitambua ni miongoni mwa matatizo yanayowakumba wanawake wengi nchini.
  Tuma maoni kwa Mhariri
   
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  We needed our own.
   
 3. w

  wasp JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  It is high time men as a gender start their "Tanzania Mens' Commercial Bank".
   
 4. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hii ni siku muhimu sana ya kukumbukwa katika historia ya nchi yetu na hasa katika harakati za maendeleo ya wanawake.
  Serikali imefanya jambo kubwa sana katika kuunga mkono na kuhakikisha kuwa benki ya wanawake inakuwepo na inaanza kazi zake.
  Baadhi hawawezi kuona umuhimu wa benki hii lakini ukweli ni kwamba wanawake wanahitaji kuwa na chombo maalum cha kuwasidia kuweza kujiendeleza kiuchumi. Historia ya kimaendeleo kati ya wanawake na wanaume katika nchi yetu na hata baadhi ya nchi nyingine inaonesha kuwa wanawake wengi hawamiliki mali hata pale wanapokuwa wamezipata wakiwa ndani ya ndoa zao. Taasisi kama hizi zitaweza kutoa mchango mkubwa kwa wanawake kushiriki katika kujiletea maendeleo yao na kujikwamua kutoka katika hali ambayo huwakabili mara kwa mara.
  Ningependa kutoa ombi kwamba, pamoja na beni hii kuwa ni ya akina mama basi ilenge kuweka sera za kuweza kuwasaidia hasa akina maam wale ambao ni wahitaji. Elimu itolewe ya kutosha kabla ya akina mama wa kipato cha chini kupewa mikopo hiyo kwani kusipokuwa na elimu ya kutosha mikopo inaweza kupotea na hatimaye benki kupata hasara.
  Kwa upande mwingine, kuna akina mama wale ambao ni 'watoto wa mjini' hawa hukopa na baadae hukwepa kabisa kulipa (siwatofautishi na wezi/majambazi yasiyotumia silaha za moto) hawa wbanwe vilivyo ikiwa ni pamoja na uhakikisha sheria na taratibu zote nzuri zinafuatwa wakati wa kuchukua mikopo hiyo. Hii itasaidia kuziba mianya ya kukwepa kulipa madeni hayo wakati watakapokuwa wanatakiwa kufanya hivyo.
  Tatu, benki ni lazima ifanye kazi zake kiutaalam zaidi kwa kuzingatia wateja wake na kuepuka kabisa kufanya kazi kisiasa au kupokea mashinikizo ya kisiasa. Hapa si maanishi kuwa ni hizi active politics tunazozifahamu, bali benki inapashwa kufanya kazi zake bila ya kuingiza maamuzi ambayo si ya kitaalamu katika utendaji wake.
  Mwisho ninaitakia kila la heri na mafanikio tele Benki ya Wanawake
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Again, Bank hii itanufaisha wake wa vigogo na mafisadi! Mwanamke wa kawaida atakuwa hakopesheki. Wanawake wa Myobozi - Kigoma ama kule Nagurukulukuru, ama Nabengo Songea waendelee kulia tu!
   
 6. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Yes indeed you needed it, but you seem to have had a false start in the appointment of your CEO!! I heard her today being interviewed by M/S Lweno of ITV morning show; I am sorry to say that she did not seem to have it together!! Was Sophia Simba the UW wa CCM chairperson involved in her selection? If indeed that is the case, no wonder you have ended with such a product. There are so many experienced and knowledgeable women bankers you could have tapped for this appointment. Next time around try to short list M/s Atupele Ongara.
   
 7. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  1. jamani kwanini gender descrimination kwenye biashara?
  2. je ni yao ni kuwasaidi wanawake au kupata wateja kwa kutumia mgongo wa wanawake???
  3. kwani hiyo benk ingeshindwa kuitwa jina jingine alafu ikatoa huduma nzuri kwa wanawake na wanaume????
  4. je rais ni sahihi yeye ku-support gender descrimination kwenye biashara????
  5. je kuwa na bank ya wanawake ni kuwaongezea ushindani au ni kuwaambia kuwa hamuwezi kushindana na wanaume na hivyo kuwadumaza ushindani wao????
  6. je wanaume wasienda kufungua kwa ajili ya gender descrimination?
   
Loading...