Rais Kikwete, IPTL huwezi kuikwepa tunataka maelezo ya kina

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Ama kweli zimwi likujualo halikuli likakwisha.Ahadi kubwa kuliko zote alizowahi kuahidi JK(Baba Mwanaasha) ni serikali yake kuhakikisha ina nunua mitambo ya IPTL na kuahidi tatizo la umeme litakuwa ndoto, lakini mpaka leo hatuoni hatua za serikali ya chama cha mapinduzi kuhakikisha suala hili linashughulikiwa.

Tuna kila sababu kuhoji juu ya nchi yetu na ahadi tunazoahidiwa wakati wagombea nafasi mbalimbali wanapojinadi kuomba ridhaa ya wananchi.

Wengi tulijua ili kuwa changa la macho kufunika kombe mwanaharamu apite.Suala hili JK hawezi kulikwepa japokuwa mara nyingi amekuwa akilikanusha kuhusika na mkataba kandamizi wakati akiwa waziri wa nishati na madini kuhusiana na IPTL.

Hata kama lengo ni kufunika scandal ya IPTL na ameshindwa kuitekeleza basi atueleze watanzania amefikia wapi,kwani jinamizi hili litamtesa bila kutoa ufafanuzi wake kamwe hatutamwelewa,vinginevyo nawe upime uone.
 
Sana tu, najua alikuwa aziri wa viwanda enzi zile.
alikula cha juu pale, hivi unajua kama IPTL ni madalali tuu waliokula cha juu na kuajiri kampuni ya wartisila toka finland. kwa nini TANESCO hawakuwaajiri badala yake matapeli wenye ngozi chafu na nyeusi toka india wanapeta?????????
 
Ni heri mngekuwa mnamwambia mtu mwenye Masikio ya kusikia. Au Mtu nwenye akili ya kuelewa. Mie mwenzenu watu wanaomsemaga huyu jamaa wananikumbushaga sana commedy moja ya Mr. Bean. Siku Mr. Bean akiwa anataka kuvua nguo aogelee ghafla akamwona jamaa amevaa miwani meusi pembeni yake anamtazama. Kila akigeuka anakuta jamaa anamtazama. Akaangaika sana kujificha mwisho akafanikiwa kuvua suruali. Akahema kidogo kujipongeza kwa ushindi. Wakati anaanza kuvuta hatua kuelekea majini mara akamwona yule jamaa ananyanyuka na fimbo yake "nyeupe" anaanza kuondoka huku anapapasa! Sasa mnaomzema vibaya huyu jamaa jifunzeni kwa yaliyomkuta Mr. Bean! Mi naona ni bora tu nimwache itakapofika wakati" ataokota fimbo yake" ataondoka.
 
Mkuu mtoa mada kwa kiasi fulani umeniudhi! Hiyo ahadi ni ya kisanii, kama sikosei mkataba wa wizi wa iptl unaisha ndani ya miaka mitatu ijayo, angalia madai yako juu ya 'ahadi' ya msanii yasije yakachangia yeye 'kuwa msikivu', hlf serikali iinunue kampuni hiyo kwa bei mbaya! Nilitegemea unataka tutafute namna ya kuwapata wote waliohusika na wizi huo hlf wakatwe vichwa...
 
Nakubaliana nawe Punaine-Red,lakini ni lazima tuhoji tujue pesa yetu iliyotumika ilichotwa na nani,lazima atakuwa anajua kwa kuwa ndiye aliyekuwa na dhamana
 

Baada ya kuwa kwenye mgogoro wa umeme nchini Tanzani a yapata miaka karibu 15 sasa, Chanzo chetu kikaamua kufuatilia hasa tatizo lilianzia wapi na nani waliohusika.

Chanzo hicho kilianzia ndani ya Wizara ya nishati na madini kwa kufuatilia mikataba iliyoyaingiza nchini makapuni ya uzalishaji umeme,
Taarifa halisi na nyaraka zinabainisha kuwa tatizo hili lilianza baada ya mfanyabiashara maarufu bwana James Rugemalira kuiingiza nchini kampuni ya IPTL kutoka Vietnam!

Mchakato unatajwa kuwa ndugu James Rugemalira alikuwa akifanya biashara ya Mchele kutoka Vietnam mwaka 1995, katika harakati zake za kibiashara huko Vietnam aliweza kuunda urafiki na wanaotajwa kuwa wamiliki wa IPTL hii ya sasa.

Mwaka 1997 kulianza kutokea uhaba wa umeme Tanzania ambapo ndani ya Wizara ya nishati na Madini kulipendekezwa itafutwe kampuni itakayozalisha umeme wa dharula wa haraka zaidi ili kunusuru taifa:

Kamishna wake alikuwa ni Ndugu Patrick Rutabanzibwa ambae katika uchunguzi umebaini ni ndugu na James Rugemalira ambae ni mfanyabiashara na mmiliki wa Mabibo Heineken ya Ubongo,

Baada ya Rutabanzibwa kuona kuwa pale wizarani kuna mwanya wa kupiga hela aliweza kuongea na mdogo wake ambae katika nyaraka nyingi anatajwa zaidi kwajina moja tu la Rugemalira kuwa atafute kampuni ya kufanya kazi hiyo haraka sana!
Rugemalira bila kusita akawashtua washikaji zake ambao taarifa kutoka Vietnam zinasema waliokuja si wale waliokuwa na urafiki na Rugemalira bali ni marafiki wa marafiki wa Rugemalira kutoka Malaysia.

Na hawakuwa na sifa ya kiushawishi ya kufanya mradi wa kimataifa ingawa waliwezakushirikiana pamoja bila tatizo kwakuwa yalikuwa ndio malengo yao ya pamoja!

Makubaliano ya mkataba ilikuwa ni mashine zitakazoletwa na IPTL, zitakuwa na mfumo wa kutumia gesi na mafuta, hilo liliingizwa katika makubaliano ya mkabata kwakuwa tayari kulikikuwa na mradi wa songas uliokuwa ukiendelea kujengwa .

Katika uchunguzi ulioenda sambamba na mahojiano ya kijasusi, bwana Rutabanzibwa anasema miezi miwili baada ya kusaini mkataba ule alishangazwa kubaini kuwa IPTL inaleta mitambo inayotumia mafuta tu na alipouliza wasaidizi wake wakamuambia mkataba unasemaje? Akaamua kwenda kuangalia upya mikataba aliyohusika na yeye kuisaini lakini anasema "nilishangaa kuona kipengele kilichokuwa kikisema kuwa genereta hizo zitakuwa na uwezo wa kutumia gesi kimetolewa" nakuwa generata za mafuta mazito tu.

Baada ya kupandishwa nakuwa Katibu mkuu, anasema "nilizuia kuletwa kwa mitambo hiyo kwakuwa nilizungukwa na kubadilishiwa mkataba feki"
Uchunguzi umebaini Bwana Rutabanzibwa hakuzuia ama lengu la kuzuia halikutimilika na alihongwa!

Ukweli unabainika katika dokezo la 12/6/2001 toka kwa kwa kigogo mmoja wa juu wa sasa jina tunalo ilikiwa limeandikwa kwa mkono na kalamu ya wino mwekundu "Kama nilivyokuahidi jana katika kikao chetu, waambie wailete hiyo mitambo kama ilivyo na mimi nitafanya kama tulivyokubaliana" chini ikasainiwa Jina la kigogo huyo wa juu hapa nchini jina limehifadhiwa

Licha ya hivyo bado uchunguzi unazidi kubaini ushirika wa karibu wa Kigogo huyo wa juu hapa nchini jina linahifadhiwa na mtu anaetajwa kuwa ni Rugemalila anaeonekana alikuwa na nguvu ya ushawishi kwa Rutatabanzibwa na wavietnam wa IPTL.
Kwakuwa baada ya kufuatilia kwa kina imegundulika kuwa katika account ya bank (CRDB) ya biashara ya mchele ya Rugemalila, kila mwezi kiasi cha pesa Shilingi milioni 130 kilikuwa kikihamishwa kwenda kwenye account mbili tofauti lakini za mtu mmoja aliyefahamika kwa jina Asha Salum Mohamed mkazi wa Arusha mjini,

Jambo la kuvutia zaidi nikuwa pesa hizo zikifika kwenye hizo account zilikuwa zikitolewa ndani ya masaa 48, na kuingizwa kwenye akaunti ya ya Abas Zuberi Musa (NMB) na hapo hutolewa siku hiyohiyo (Cash) na kupelekwa moja kwa moja katika akaunti ya siri ya Rais Jakaya kikwete iliyopo Standard Chartered Bank

Abas Z. Musa kwa sasa ni mmoja watu ambao wako katika idara moja ya ulinzi hapa nchini tena akitumika sana kwa mambo binafsi ya Kigogo huyo wa Juu hapa nchini!
Huo ndio ushikiano wa wa Kigogo huyo na james Rugemalira katika biashara ya mchele

Bado Chanzo chetu kinaendelea kufuatilia kwa undani kujua mambo makuu mawili kwanza:
(1) Kwanini aliamua kufanya biashara hiyo ya mchele kwa siri na kuchukua faida kwa siri kubwa hivyo?
(2) Iwapo Kigogo huyo wa Juu hapa nchini alihusika moja kwa moja au kwa aina yoyote ya biashara ya IPTL
Chanzo hicho kitafanya uchunguzu huu kwa undani na kujua nini hasa kipo kwenye tatizo la umeme Tanzania, kwa sahv kinaanza na IPTL kisha wengine watafuata!
Kwasababu za kiuchunguzi nyaraka sitaziweka hapa mpaka uchunguzi ukamilike wote!


Uchunguzi: Chanzo cha matatizo katika sekta ya Umeme Tanzania na ujio wa IPTL
 
Huyu tofauti na yule wa Bean.Huyu anakomba nguo zote na kukuacha kama ulivyo kwenye swimming pool.
Anafaa kufukuzwa ndio mtu aingie kuogelea
Ni heri mngekuwa mnamwambia mtu mwenye Masikio ya kusikia. Au Mtu nwenye akili ya kuelewa. Mie mwenzenu watu wanaomsemaga huyu jamaa wananikumbushaga sana commedy moja ya Mr. Bean. Siku Mr. Bean akiwa anataka kuvua nguo aogelee ghafla akamwona jamaa amevaa miwani meusi pembeni yake anamtazama. Kila akigeuka anakuta jamaa anamtazama. Akaangaika sana kujificha mwisho akafanikiwa kuvua suruali. Akahema kidogo kujipongeza kwa ushindi. Wakati anaanza kuvuta hatua kuelekea majini mara akamwona yule jamaa ananyanyuka na fimbo yake "nyeupe" anaanza kuondoka huku anapapasa! Sasa mnaomzema vibaya huyu jamaa jifunzeni kwa yaliyomkuta Mr. Bean! Mi naona ni bora tu nimwache itakapofika wakati" ataokota fimbo yake" ataondoka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom