Rais Kikwete: Inasikitisha mkuu wa wilaya anakufa huku familia yake ikiishi guest house

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,906
22,052
Sipendi kuwa mnafiki wala kuitwa mbeya
kwa kweli kwanza naomba niwape pole kwa familia ya mh capt J. Yamungu
ni huzuni kubwa kuondokewa kwa unaempenda ....ni wakati muhimu sasa
familia kuwa kitu kimoja bila kujali itikadi zilizokuwepo na kumwomba
mungu awaongoze muweze kumpumzisha babayetu salama

Huzuni yangu kubwa ni kitendo cha kusikia kwenye redio mbili leo kwamba
mzee alikuwa akiishi guest house,,nazani kwa cheo alichokuwa nacho alistahili
kutafutiwa hotel nzuri tu tena ya heshima...nijuavyo mkuu wa wilaya na mkoa
wanamwakilisha rais..sasa hata kama nyumba yake inafanyiwa marekebisho
sidhani na bado nahuzunika kwa hili akustahili kuishi guest house

mbaya ni taarifa zinasema mhudumu wa guest house ndie aliemgongea mzee baada ya kusikia
akikoroma vibaya na alipoona ajibiwi akaita kamati ya ulinzi na kuamua kuvunja mlango

ni mapenzi yangu chini ya uongozi wako akutakuwa na wakuu wa wilaya kulala guest
house nasema hivi kila mtu anajua uchafu wa guest house ni rahisi viongozi kama hawa kudhurika
hasa ukizingatia wanakuwa kwenye channels nyingi na wakati mwingine wanaitajika kutoa maamuzi
magumu ambayo raisi wangu unayaogopa kwa wengine..sasa sitoshangaa kusikia hata mzee walimwekea kitu yakatokea haya yalipo kwa kuwa usalama ni mdogo sana guest house kuliko hotel kubwa zenye hadhi ambazo serikali mna uwezo wa kulipa

raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umwangazie apumzike kwa amani mzee wetu yamungu/j na wote mseme

amen
 
Mh! Siku hizi serikali haikai ikatulia bila makashfa ya kila aina. Poleni wafiwa wote Mungu ampe pumziko la milele amen
 
ANITHA Guest House - Mugumu

Naiuliza serikali mlishindwa hata kumlipia chumba cha sh. 25,000/= Girrafu hotel hadi mkuu wa wilaya anaenda kuishi Anita??
 
kunamambo mengi yanaweza kuwa yamechangia huyu mzee kufia kwenye mazingira hayo sometimes wanapewa hela kwenda pakubwa lakini kutokana na sababu mbalimbali km kupata hata hela za kupeleka zawadi majumbani mwao wanaenda kujibana huko .sidhani km serikali inaweza kuhusishwa moja kwa moja jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni

sory msijeniita msemaji wa serikali maana jf..................
 
shida viongozi wetu nie wezi,huyu mkuu yaweza kuwa alikuwa anajiibia mwenyewe huo mgao wa nyumba!!!
 
Sipendi kuwa mnafiki wala kuitwa mbeya
kwa kweli kwanza naomba niwape pole kwa familia ya mh capt J. Yamungu
ni huzuni kubwa kuondokewa kwa unaempenda ....ni wakati muhimu sasa
familia kuwa kitu kimoja bila kujali itikadi zilizokuwepo na kumwomba
mungu awaongoze muweze kumpumzisha babayetu salama

Huzuni yangu kubwa ni kitendo cha kusikia kwenye redio mbili leo kwamba
mzee alikuwa akiishi guest house,,nazani kwa cheo alichokuwa nacho alistahili
kutafutiwa hotel nzuri tu tena ya heshima...nijuavyo mkuu wa wilaya na mkoa
wanamwakilisha rais..sasa hata kama nyumba yake inafanyiwa marekebisho
sidhani na bado nahuzunika kwa hili akustahili kuishi guest house

mbaya ni taarifa zinasema mhudumu wa guest house ndie aliemgongea mzee baada ya kusikia
akikoroma vibaya na alipoona ajibiwi akaita kamati ya ulinzi na kuamua kuvunja mlango

ni mapenzi yangu chini ya uongozi wako akutakuwa na wakuu wa wilaya kulala guest
house nasema hivi kila mtu anajua uchafu wa guest house ni rahisi viongozi kama hawa kudhurika
hasa ukizingatia wanakuwa kwenye channels nyingi na wakati mwingine wanaitajika kutoa maamuzi
magumu ambayo raisi wangu unayaogopa kwa wengine..sasa sitoshangaa kusikia hata mzee walimwekea kitu yakatokea haya yalipo kwa kuwa usalama ni mdogo sana guest house kuliko hotel kubwa zenye hadhi ambazo serikali mna uwezo wa kulipa

raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umwangazie apumzike kwa amani mzee wetu yamungu/j na wote mseme

amen

Kwanza fanya uchunguzi wa kina kisha ndio umwagike hapa jamvini usisikilize sana mambo ya kwenye redio.Kwanza hoteli hiyo alipokuwa anaishi ina utulivu mzuri kuhusu swala la gharama sii kitu. Maana hata mzee wa Morogoro alilala hoteli ya kifahari lakini aliibiwa.Mtasema mengi sana ila siku yako kama imefika imefika tu.
 
una laana kweli kama unajiunga na JF UJUI TOFAUTI YA HOTEL NA GUEST LOH
 
Pole sana ndugu p wewe ndiye una laana kwa kuandika vitu vya kusikia ila sii vya kuona na kuthibitisha ukiwa mwandishi wa habari hufai kabisa pia nikujulishe kuwa hakuwa anaishi na familia yake alikuwa anaishi peke yake.Nakwambia hivi kwa sababu nilikuwa nafika hapo hotelini alipokuwa anaishi kwa ajili ya kumpa msaada fulani wa kiufundi wa vifaa vya umeme alivyokuwa anatumia.
 
Pia niendelee kukufahamisha ndugu p kuwa tatizo kwa mzee lilimuanza mchana siku alipokuwa kwenye mbio za mwenge hapo wilayani kwake ila alikimbizwa hospitali akapata matibabu akarudia ktk hali yake ya kawaida na kuendelea na taratibu zote za mwenge hadi usiku.
 
kunamambo mengi yanaweza kuwa yamechangia huyu mzee kufia kwenye mazingira hayo sometimes wanapewa hela kwenda pakubwa lakini kutokana na sababu mbalimbali km kupata hata hela za kupeleka zawadi majumbani mwao wanaenda kujibana huko .sidhani km serikali inaweza kuhusishwa moja kwa moja jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni

sory msijeniita msemaji wa serikali maana jf..................
flora msoffe usemayo ni kweli lakini Mkuu wa wilaya anastahili ya kupewa nyumba na siyo "subsistence allowance" (posho ya kujikimu). Wenzetu wazungu wanachukia sana hii kitu inaitwa "perdiem"; kwa hadhi ya mkuu wa wilaya alitakiwa akaa kwenye hotel na bill iende kwa mwajiri wake hadi atakapopatiwa nyumba.

Lakini kwa upande mmoja tusiilaumu sana serikali, kuna maofisa wakipewa ofisi mpya wanataka kila kitu kiwe kipya kuanzia rangi, samani, gari, wahudumu n.k. inawezekana marehemu alikuwa kwenye mkumbo huu
 
Ilikuwa lazima ifanyiwe marekebisho kwa sababu ni nyumba zile zilizojengwa enzi zile za mwl kwa hiyo miundo mbinu mingi mle ndani ni ya kizamani.
 
kunamambo mengi yanaweza kuwa yamechangia huyu mzee kufia kwenye mazingira hayo sometimes wanapewa hela kwenda pakubwa lakini kutokana na sababu mbalimbali km kupata hata hela za kupeleka zawadi majumbani mwao wanaenda kujibana huko .sidhani km serikali inaweza kuhusishwa moja kwa moja jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni

sory msijeniita msemaji wa serikali maana jf..................

Rais hasa ndie anaehusishwa na hadhi ya watu anaowateua kuwa wakuu wa wilaya na mikoa; sasa kama Rais hafuatilii ushauri wa vetting wa vyombo vya dola katika teuzi zake bali anaendekeza USWAHIBA,matokeo yake ndio hayo unakuwa na watu viongozi wasiokuwa na hadhi!! Sio siri kuwa marehemu alikuwa anapenda sana KILAJI na mambo yanayokwenda na kilaji tangu akiwa DC Singida ,hivyo guest palikuwa ni mahala barabara kwake!!
 
Ilikuwa lazima ifanyiwe marekebisho kwa sababu ni nyumba zile zilizojengwa enzi zile za mwl kwa hiyo miundo mbinu mingi mle ndani ni ya kizamani.

Ina maana aliyekuwa anaishi kwenye hiyo nyumba yeye alikuwaje?

Huu ni uchuro tu wa viongozi wetu! Unakuta nyumba imepauka kidogo tu rangi anadai ifanyiwe matengenezo makubwa. Hawa ndo wanafirisi nchi yetu! Naona umeshupalia sana hii habari lakini unshindwa kuona jinsi alvyojidhalilisha huyu Mkuu kwenda kuisi Guest House badala ya kuishi Hotel. Unataka kutuambia hapo Mugumu Anitha ndo nyumba nzuri kuliko zingine? Acha hizo bwana!!

Unalala uchochoroni huku kibindoni una milioni kadhaa siku ya siku wanakuibia huku kunguni nao wamekufaudu!!!
 
Thamani ya mtu na hadhi ya mtu haijajiwi na kutokana na sehemu au nyumba,hoteli mtu anayoishi.Nyinyi ndio huwa mnawakana wazazi wenu kwa sababu wanaishi kwenye nyumba za tembe huko vijijini mbona hayati mwl Nyerere alikuwa anaishi kwenye nyumba ya kawaida tu hadi hapo alipokuja kujengewa?.
 
Back
Top Bottom