Rais Kikwete, hivi ni lazima uwalinde mafisadi kama Dk. Idris Rashid, Hosea, n.k.?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete, hivi ni lazima uwalinde mafisadi kama Dk. Idris Rashid, Hosea, n.k.??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magezi, Sep 17, 2009.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kwa mudamrefu nimekuwa najiuliza hivi ndugu kikwete ni kweli unashindwa kuamini kwamba Dr. Idris Rashid alihusika ktk kashfa ya rada, IPTL? mpaka unaendelea kumpa vyeo ambavyo hata hivyo ameshindwa kufanya mabadiliko yoyote pale TANESCO?

  Sasa tuna mgao wa umeme mikoa sita, Rashid amekaa kimya na kwa sababu alisha sema kuwa nchi itakuwa gizani serikali isipo nunua mitambo ya dowans, ameona wala asiseme lolote kwani anajua alisha toa tahadhari.

  Mkulu Rais jakaya kikwete, huoni kwamba unapoteza credibility ya kuwa rais pale unaposhindwa kuchukua uamuzi sahihi ktk uteuzi wa baadhi ya watendaji??

  Kikwete, unazidiwa hata na rais wa Zambia mwanamke amemsimamisha kazi mkuu wa taasisi ya kuzuia rushwa nchini humo baada ya kuboronga kesi ya Chiluba!! Wewe mafisadi, akina Hosea et al wanakula nchi tu na wewe unacheka nao??

  Angalia bandarini kulivyo oza, siku moja ukadiriki kusema unawajua wala rushwa pale bandarini, je, umewafanya nini watu hao?? mbona uozo pale unaendelea huku TICTS wakiendelea kuwabambikiza storage charges wafanya biashara wanaopitisha mizigo pale???

  Ni seme wazi Rais Kikwete unatukera kwa kutofanyia kazi maoni yetu hapa JF, lakini kumbuka JF inaweza kukushauri vyema kuliko hao akina kingunge na wenzake.
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kwa tangazo la kazi la MD-Tanesco, je, mkataba wa Idris rashid umekwisha au anaandaliwa mashtaka??
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Lazime awalinde maana ndio waliomuweka madarakani pamoja na kusaidia kukwiba fedha kwa ajili ya kumnadi. Au mmesahau kama CCM walichota hela pale BOT habari ambayo imeshatiwa kapuni na kuzikwa.
   
 4. c

  chiswera New Member

  #4
  Sep 19, 2009
  Joined: Sep 8, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tutasikia mengi.Kuna yeyote anajua aliko Zakia Meghji?hebu leteni janvini.
   
 5. K

  Keil JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Naona joto limezidi huko jikoni, kama kilichoandikwa hapa ni sahihi basi tunaweza kusema kwamba Dr Rashid hatarudi TANESCO baada ya mkataba wake kuisha. Lakini tusije tukashangaa iwapo JK atamteua tena, maana Rais wetu siku zote huwa hatabiriki na huwezi kujua anafikiria nini.

  Pia Dr Rashid mwenyewe ni kigeugeu tusije tukashangaa tukisikia nae ni mmoja wa waombaji wa hiyo post maana mzigo wa Bwana (mitambo ya Dowans) haujafika na hivyo kumkabidhi punda mwingine (new MD) ambaye hajawa trained kubeba mizigo yenye miba, anaweza akarusha mateke na hatimaye zigo likabwagwa. Nina uhakika RA lazima yuko mbioni kusaka nani anafaa iwapo Dr. Rashid atagoma kabisa kurudi TANESCO.


  Dk Rashid kuachia ngazi Tanesco

  MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Dk. Idris Rashid ataachia ngazi katika shirika hilo Novemba mwaka huu.

  Dk Rashid amesema jana kuwa, hana mpango wa kuendelea kuiongoza Tanesco atakapomaliza mkataba wake, anahitaji kupumzika.

  Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo imetangaza nafasi ya kazi ya Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe mbili mwezi ujao.

  “Mimi sitaomba tena nafasi hii na sina interest (nia) kabisa ya kuendelea kuliongoza shirika hili”, amesema na kubainisha kwamba, umri wake ni wa kustaafu.

  “Umri wangu ni zaidi ya miaka 60, huu ni muda wa kustaafu na ndiyo umeshafika nahitaji kupumzika” amesema kiongozi huyo aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT).

  Kwa mujibu wa tangazo hilo lililochapishwa jana kwenye vyombo vya habari, Bodi ya Wakurugenzi imetangaza nafasi hiyo kwa mtu mwenye sifa ya shahada ya Uhandisi wa umeme au Uongozi na uzoefu wa kazi wa miaka si chini ya 15.

  Kuna taarifa kwamba, kutangazwa kwa nafasi ya Dk. Rashidi kunatokana na shinikizo kutoka ngazi ya juu ikiwemo Wizara ya Nishati na Madini.

  Chanzo cha habari kimeeleza kwamba, Dk. Rashid amekuwa na msimamo na kutokubali kuyumbishwa katika uamuzi asiokubaliana nao.

  “Wizara (Nishati na Madini) imeishinikiza bodi itangaze nafasi hiyo ili aombe mtu mwingine katika nafasi hiyo ambaye ataonekana kukubaliana na maagizo kutoka juu”, kimesema chanzo hicho cha habari.

  Dk Rashid ameakanusha kuwepo kwa shinikizo hilo na amesema “hizo ni ngonjera za mitaani hazina ukweli”.

  Miongoni mwa msimamo uliowahi kuonyeshwa na Dk. Rashid ni pale alipojiuzulu wadhifa wake huo kutokana na kutokubali kubadilisha msimamo wake dhidi ya Kampuni ya Saruji Tanga ilipojipatia umeme kwa kupitisha pembeni ya mita ya Tanesco na kulipa kiasi kidogo cha fedha.

  Katika uamuzi wake Tanesco iliipiga faini kampuni hiyo Sh milioni 55 na ilipokataa ikakatiwa umeme. Hali hiyo ilisababisha kuwepo shinikizo kumtaka Dk. Rashid arudishe umeme, alikataa lakini umeme ulirudishwa katika mazingira yasiyoeleweka kwa kisingizio kwamba hatua hiyo ingesababisha hasara.

  Dk Rashid alipinga uamuzi huo, akajiuzulu.

  Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Aloyce Tesha, amesema,hatua ya bodi kutangaza nafasi hiyo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco ni utaratibu wa kawaida na kwamba Dk. Rashid ana kazi ya kuomba nafasi hiyo tena.

  “Muda wake (Dk. Idris) unamalizika, hivyo ndiyo maana nafasi imetangazwa. Alikuwa na contract (mkataba) ambao unamalizika mwisho wa mwezi huu. Anayo fursa ya kuomba kama atapenda,” alisema Tesha na kuongeza:

  “Huu ndio uwazi na ndio utaratibu wa sasa wa Serikali kwa nafasi kama hizo za Mkurugenzi Mtendaji, Kamishina…kutangazwa na Watanzania wenye sifa kugombea nafasi. Hakuna uhusiano wowote na Bodi kumkataa au Wizara.

  “Na uteuzi ukifanyika majina yanakwenda kwa Rais ambaye anachagua anayefaa. Lakini akiridhia, anaweza kuendelea aliyekuwepo.”

  Source: HabariLeo
   
 6. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mafisadi wanatengenezwa na mazingira wanayoyakuta, so ni jukumu la aliyeandaa hayo mazalia kuyalinda kwa maslah ya pande hizo 2
   
 7. K

  Kinyikani Member

  #7
  Sep 19, 2009
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 65
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  huwezi kuwa fisadi bila ya kuwa CCM wala huwezi kuwa CCM bila ya kuwa Fisadi
   
 8. A

  Amulike Noel Member

  #8
  Sep 20, 2009
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani umesahau kuwa kabla ya ubwana mkubwa nilikuwa Bernard Membe na baadhi ya mikataba kama IPTL na suala la nyumba ya ubalozi wa Tz kule Italy vinaweza kunipitia so i've to be xtra careful.
   
 9. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hii statement ni correct !perfect! Inashangaza kuona kuna wanaotegemea hawa jamaa washtakiwe, mwingne atakayechukua nafasi afanye vizuri zaidi. Hili halitatokea Tanzania tukiendelea na katiba iliyopo.

  So long as Waziri pia anabakia kuwa Mbunge, so long as Raisi ndiye mteuaji wa kila kiongozo hadi Wakuu wa wilaya bila hata kuwepo a body that scrutinizes these appointments, a body that is able to reject such leaders who may not be qualified and thus fail to deliver, nothing will change, at least not soon.
  Ni kwanini mashirika ya Umma yanakufa na hawajali, wale Mameneja na Wakurugenzi kama Dr. Idris nyakati za uchaguzi hutakiwa watoe mchango kwa chchm. Huo ni wajibu, wengine hutoa mpaka linakufa na wafanyakazi kukosa ajira. Wengine huchukulia huo kama mwanya wa wao kujinufaisha, kuchota saana. Ndiyo maana hata likifa shirika wala hawashtakiwi wala kuchukuliwa hatua yoyote ya kinidhamu, badala yake hupewa cheo na kuongezewa madaraka zaidi. Ni nani asiyejua kuwa bila CRDB chcchm inaweza ianguke? Dhibiti ile BoT leo, dhibiti CRDB uone kama kutakuwa na viji-T-Shirt vya njano viwanja vya mikutano.

  HADI NCHI ITAKAPOKUWA TAYARI KUREKEBISHA KATIBA IFANANE NA YA NCHI INAYO AMINI KATIKA DEMOKRASIA TUTAENDELEA KUONA UFISADI UKISHAMIRI NCHINI.
   
 10. M

  Magezi JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Lakini ndugu wana JF tufanye nini sasa kumshauri rais kikwete ili abadilishe mambo??
   
Loading...