Rais kikwete haoni matatizo ya watanzania bali anapambana na chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais kikwete haoni matatizo ya watanzania bali anapambana na chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TIBANYENDERA, Mar 1, 2011.

 1. T

  TIBANYENDERA Member

  #1
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wenzangu, ndugu wantanzania na wazalendo wa taifa letu, jana tumeskia vizuri na kwaumakini hotuba ya raisi wetu wa tanzania. kiuchambuzi ni kwamba unaweza kujiuliza maswali yafuatayo;
  1. kwanini kwa mda wa miezi mitatu hakuwahi kutoa hotuba kwa wananchi?, kwa nini iwe jana
  2. kwanini hotuba ya raisi kwa wananchi iendane sambamba na lawama kwa CHADEMA
  3.Kwanini hotuba ya raisi haikuwa na lengo lakutoa suluhu la matatizo
  4. je kinachoongelewa na CHADEMA, mfano ugumu wa maisha kwa watanzania ni uongo?
  haya ni maswali yamsingi tunapochambua hotuba ya mwisho wa mwezi.
  lakini kimantiki na uharisia wenyewe ni kwamba taifa la tanzania liko ktk wakati mgumu; kiuchumi, kisiasa na hata kiutamaduni. Na chama cha siasa kazi kubwa ni kulinda ustawi wa wananchi, hivyo chadema hakina kosa lolote la kisiasa sababu lengo kubwa la chama hicho si kutekeleza sera za chama tawala bali kuonesha ubovu wa sera za chama tawala kwa kuzilinganisha na ubora wa sera zao. practically ndo maana sera za CCM zimesababisha taifa letu liwe na wakati mgumu na hasa maisha magumu kwa watanzania.
  Hivi taifa kama haliwezi kupiga hatua kimaendeleo ninani wakulaumiwa, je ni CHADEMA au ni chama Tawala pamoja na serikali yake? ktk taifa lolote ugumu wa maisha imekuwa ni kura ya turufu ya kukiondoa chama tawala madarakani kwa sababu ya kushindwa kudeliver kwa wananchi.
  jambo jingine nawaomba watanzania wenye uelewa kama wengine ni wafahamishe kuwa kujua ni lini tunakuwasema chama kinafanya kazi ya kisiasa. si wakati wa kampeni tu, kazi za siasa huendelea tena kwa kasi zaidi na ali zaidi baada ya uchaguzi. hii ni kwasababu chama pinzani lazima kiwafundishe wananchi amabao kwauelewa wao wanashindwa kujielewesha kuwa pamoja na kuwa hawajawachagua ndiyo maana wanapata matatizo ya kiuchumi.
  Siasa huendana timing, kwa hili chadema ina timing nzuri kwasababu hali ya maisha ni ngumu. hizi ni mbinu za kisiasa ndugu zangu.
  ktk hili huwezi9 kusema kwamba CHADEMA INALETA VURUGU HATA KIDOGO, NINI MAANA YA VURUGU? NA AMANI? JE MANI INATOWEKA PALE MTU UNAPOMFAHAMU MWIZI WAKO? NI KWELI KWASABABU UKIWA RAFKI YANGU NIKAJA KUGUNDUA KUWA UNATEMBEA NA MKE WANGU, LAZIMA NITANGAZE UADUI NI KUCHUKULIE HATUA ZA KISHERIA, CHADEMA INAFANYA HIVO INAWAELIMISHA WANANCHI KUJUA HALI HALISI YA TZ, ELIMU DHIDI YA HAKI ZAO,MATUMIZI YA RASLIMALI ZAO, UFISADI ILI WWANANCHI HAO WACHAGUE LA KUFANYA
  tulitegemea raisi atatoa majibu ya matatizo ya wananchi. hakufanya hivo. Lakini nihitishe kawjambo moja tu, tulikubali mfumo wa vyama vingi tuache vyama hivyo vifanye kazi zake za kisiasa.
   
 2. e

  emalau JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2011
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Nilishasema kabla ya uchaguzi kwamba amani haiji bila haki kutendeka, wameiba kura nafsi zinawasuta sasa wana hofu na hawana amani kwenye nafsi zao kwa kuwa wanajua walichofanya kwa usaidizi wa Makame, Kiravu na "Usalama wa taifa".
   
 3. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  umeme, dowans, ugumu wa maisha nk hayo ni matatizo ya watanzania SIYO ya JK. Matatizo ya JK ni chadema! hapo ndo ilipotofauti kati ya watz na JK.
  JK anaangalia ni nani anataka kumuondoa madarakani - watz wanaagalalia mlo wa siku utatoka wapi!
   
 4. A

  AlamaZA NYAKATI JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jk anatakiwa kujibu matatizo ya watanzania aache kulalamika. Alishawahi kusema kuwa wapinzani hawawezi kumnyima usingizi mbona sasa anaweweseka, ajibu hoja siyo kutuletea vioja vya ajabu na ngojera za kila siku.
   
 5. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Mkwere akisikia peoples power haja inataka kutoka maana akichunglia Misri na Libya anaishiwa nguvu
   
 6. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,635
  Likes Received: 4,746
  Trophy Points: 280
  La kuvunda halina ubani, ameharibu mwenyewe sasa anatafuta mchawi,hana jinsi itabidi aachie ngazi tuuuuuuuuuuuuuu.UWEZO WA KUTATUA MATATIZO YA WATANZANIA HANA KWA VILE YEYE MWENYEWE NDIYE TATIZO.Kwa heri mkwere kwa heriiiiiiiiii.
   
 7. bona

  bona JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  kilichotokea kule tunisia, misri na sasa uko yemen, bhrain, libya ni njaa, hamna mkate mezani propaganda za kusingizia hazitoi njaa tumboni na sasa njaa ndio itakua mkombozi wa kila mtu duniani kwani hatutasikia propaganda za hawa wapinzani au cjui wataleta vita wala sisi tunatetea dini fulani kwani njaa haichagui mwenye dini gani, chama gani, rangi gani wala kabila gani! wakati huo sasa africa ndio umefika kwa iyo kucheka cheka kwake ovyo mbele ya TV hakutamsaidia kwani mtu mwenye njaa hacheki!
   
Loading...