Rais kikwete bora uahidi vyumba vya madarasa kwanza kabla ya kompyuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais kikwete bora uahidi vyumba vya madarasa kwanza kabla ya kompyuta

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magezi, Jun 10, 2010.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hali halisi ya elimu ktk sehemu nyingi za nchi ni kama inavyoonekana ktk picha hii hapa chini. Nakumbuka Rais Kikwete alisema na kuahidi kwamba ktk miaka 5 ijayo kila mwanafunzi wa sekondari atakuwa na kompyuta yake. Je kama vyumba vya madarasa ni tatizo, hizo kompyuta zitawekwa chini au??? Tafakari
  tarime.jpg
  Wanafunzi wa shule ya sekondari Rebu katika wilaya ya Tarime mkoani Mara wakifanya mtihani wao wa kumaliza muhula chini ya miti kutokana na shule kukabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa kama walivyokutwa mwishoni mwa wiki. (Picha na Shadrack Sagati - Habari Leo).
   
 2. bona

  bona JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  nakumbuka kipindi niko primary enzi za mzee ruksa awamu yake ya kwanza tulikua darasa la la kwanza na pili, tunaandika chini(ardhini) ili kusave madaftari na kalamu kwa madarasa ya kuanzia la tatu! tumetoka mbali!
   
 3. K

  Kikambala Senior Member

  #3
  Jun 10, 2010
  Joined: Jun 28, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kuku na yai kipi kilitangulia?maana anataka wawe na computer wakati 89%ya wanafunzi wanakaa sakafuni.vyumba havitoshi hata vyoo hakuna.why asiache usanii na kulaghai watu wakati huu wa kampeni
   
 4. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  jana tar 15/09/10 akiwa katika mkutano wake wa kampeni huko tarakea rombo, mgombea urais wa ccm mhe jakaya kikwete alitoa ahadi kuwa serikali yake itahakiksha kuwa inafikisha teknolioia ya habari katika kila sekondari hapa nchini zikiwemo zile za kata, akirejea ahadi yake ya awali ya waalimu kutumia teknolojia hiyo kufundishia na kila mwanafunzi kuwa laptop yake mwenyewe.

  Kwa kuwa najua na yeye anajua kuwa hadi sasa ni asilimia 10% tu ya watanzania wanafikiwa na nishati ya umeme ambayo ni ya lazima kwa teknolojia hii kufanya kazi. Ni wazi kuwa ahadi hii ni hewa, kwa hakuna uwezekano wa kutekelezwa kwake.

  Najua akina tandale one, yaya, matejoo n.k watakuja hapa kudai kuwa seriklali itatumia umeme wa nguvu za jua yaani (solar) kufikisha teknolojia hiyo katika sekondari za kata. Lakini ni serikali hiyo hiyo ya ccm ambayo kwa miaka 20 imejaribu bila mafanikio yoyote ya kuridhisha kusambaza teknolojia ya umeme wa solar na friji za mafuta ya taa kwa ajili ya kuhifadhi chanjo katika zahanati na vituo vya afya visivyokuwa na nuishati ya umeme katika sehemu mbali mbali hapa nchini.

  Kwa kuwa watanzania wengi hasa wa vijijini hawajawahi kumshuhudia kiongozi wa kitaifa kama vile rais akisema uongo hadharani wanaweza kumwamini na kumpatia kura zao.

  Hii ni kwa sababu ya wananchi kunyimwa fursa huru ya kuuliza maswali kuhusu utekelezaji wa ahadi zilizopita n.k. Na uwezekano wa ahadi mpya kutekelezwa. Sababu ingine inayoweza kufanya wananchi kuingia mkenge ni ccm kukataa kushiriki midahalo ambapo wagombea wake wangehojiwa na wagombea wenzaop kuhusa ahadui wanozotoa.

  Kwa hali hiyo ni vyema wagombea wa chadema na vyama vingine vya upinzania kuwaeleza wananchi kinagaubaga kuwa ahadi kama hiyo haiwezi kutekelezwa hata kwa miaka 20 ijayo.

  Wapinzani watumie ushahidi wa kukosekana kwa umeme kuwafafanulia wananchi kuwa ahadi hizi hazitekelezeki hata kidogo.

  Tunaomba pia mwenye data kuhusu waalimu kama alivyoahidi kikwete jana atumwagie humu kwa ajili ya kutumiwa na wagombea wa upinzania kupinga hoja za chama tawala, hiyo ndio demokrasia.
   
 5. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Jakaya na chama chake tulishasema ni wasanii; AHADI ZA 2005 KEDE KEDE HAWAJATIMIZA KAMA VILE KUIMALISHA SHIRIKA LA NDEGE LA ATCL na bado wanatoa ahadi hewa!! Hawaoni hata aibu waziri wa miundombinu kulidanganya Taifa kupitia bunge kuwa majadiliano na muwekezaji yalikuwayanakamilika huo ukiwa mwaka 2009 na mpaka leo wafanyakazi wanalipwa kutokana na kodi zetu bila kufanya kazi!! Hii ni dhahili kuwa kazi imewashinda achieni ngazi.
   
 6. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2015
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Magufuli amekata na kubandika. Watanzania tuwe makini na hizi ahadi zisizokuwa na kichwa wala miguu. Nafikiri Magufuli ni JK 2.0 (version 2)
   
 7. swissme

  swissme JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2015
  Joined: Aug 15, 2013
  Messages: 12,562
  Likes Received: 14,978
  Trophy Points: 280
  Point.yule shetani FaixaFOXY WAPI? Bora hatete hii point kuliko kujikomba na Bakwata.
   
Loading...