Rais Kikwete awasili mjini Blantyre, Malawi kushiriki mazishi ya Mutharika

Idara ya mawasiliano Ikulu inatia aibu. Sasa siamini kama ina watu makini, wasomi na wenye uelewa. Kama sivyo basi inalengo la kuanika ubovu wa Rais Kikwete na Serikali yake kwa kuonyesha kuwa haina uwajibikaji na haina mawasiliano mazuri baina watendaji wake hata kwenye maswala yenye maslahi kwa Taifa. Nikinukuru sehemu ya taarifa ya Ikulu hapa chini ni wazi kabisa kuwa ama Waziri mkuu Pinda amezidharau kelele au michango ya waheshimiwa wabunge. Km PM aliwadharau wabunge waliongea kwa uchungu basi PM ni mnafiki au hafai au na yeye ni sehemu ya ufisadi au kuna jambo linafichwa. Kama Pinda angekuwa amesikia vilio vya wabunge basi angenyanyua simu na kumpigia Rais kokote aliko na kumwelezea yaliyojiri wakati hayupo. Lakini pia nashindwa kuiamini na kuielewa taarifa ya Ikulu kama ni ya kweli au la kwa maana siamini kama kweli Katibu mkuu wa Rais Bw. Sifue alilazimika kufunga safari akaenda Dodoma kuonana na wenyeviti wa kamati, spika na wabunge wengineo iweje hata yeye asimjulishe Rais walau kwa ufupi tu kiasi kwamba Rais asiwe na taarifa kabisa? Kama taarifa ingesema Rais amepokea taarifa kwa ufupi anahitaji muda wa kupitia ripoti kwa ukamilifu na kisha kutoa taarifa rasmi hapo ningeelewa. Lakini kwa sasa sielewi idara hii ya mawasiliano inaundwa na nani, kama siyo inaundwa na swahiba au watoto wa familia ya kikwete na swahiba wake ambao wanajibu kwa jaziba tu bila hekima. Hata kama Kikwete amewasiri leo kutoka Brazil yaani anafika ofisini asiambie hata yaliyojiri wakati hayupo? Kama ndivyo ilikuaje akajua msiba wa Mwakanjuki hadi akaenda kuaga mwili na asijulishe swala nyeti lililojiri bungeni kwa kweli haiingii akilini kabisa. Jamani hebu soma nukuru ndogo ya taarifa hapa na nyie muone "Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Brazil, amerejea jana Aprili 21, 2012 jioni. Hajaonana wala kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Mhe. Pinda.Hivi sasa Mhe. Rais anasubiri kupata taarifa rasmi kutoka Bungeni Dodoma".
 
Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Hata akiwalinda maswahiba wake kwa hali yoyote ile, nguvu ya umma inakuja.Natamani Mtoto wa mkulima aresign mwenyewe amuachie jamaa magarasa yake.Hapo atakuwa shujaa.
 
Kweli jamaa ameamua kumchinjia baharin mwenzie PM . jamaa anarud jion hakuna maamuzi kwhy kina zitto watakuwa wameshapelekea hoja kwa spika .ina maana hata akija na maamuzi ya kuwatoa kuna uwezekana hoja kutolewa sheria inasemaje? naomba mnijuze
 
Mungu atusaidie jamani twafa!!!!!!!!!!!!!!!!! uwuwiiiiiiiiiiiiiiii!!! huyu ni kiongozi au mtalii??????
 
Mapungufu makubwa ya JK kwa upande mwingine yametufumbua macho watanzania kuwa karibu na serikali na kujua jinsi hawa ccm wanavyoitendea vibaya tz.
 
Anatoroka kupagawa na mapepo Ikulu, maana yamejaa tele.Raisi ajaye ana kazi.
Tanzania nchi yangu nakupenda kwa moyo wote. Nitafia hapahapa Tanzania.

Rais...amewasili...Malawi leo jioni kuhushuria Mazishi...anatarajia kurejea nchini kesho tarehe 23 April mara baada ya maziko - P. Kibanga





TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI




Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Blantyre ,Malawi leo jioni kuhushuria Mazishi ya Profesa Bingu wa Mutharika, aliyekuwa Rais wa Malawi., aliyefariki tarehe 5 April, 2012 Kufuatia matatizo ya Moyo

Rais Kikwete ni miongoni mwa Viongozi wakuu Saba kutoka nchi jirani na Malawi.

Nchi hizo ni Afrika Kusini, Benin, Kenya, Msumbiji, Zimbabwe na Zambia.


Wakati huohuo Ikulu inapenda kukanusha taarifa zilizonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari kudai kuwa Rais ametofautiana na Waziri Mkuu kuhusu aina ya hatua za kuwachukulia Mawaziri wanaotuhumiwa na ubadhirifu katika Wizara zao.

Napenda kueleza Umma kuwa taarifa hizo si za kweli.

Pia nitumie nafasi hii kuwatahadharisha waandishi wa habari kuwa makini, waangalifu na wachambuzi wakati wa kupokea, kusikiliza na kuandika au kutangaza taarifa wanazopata.

Rais kikwete aliwasili kutoka Brazil alipokuwa amekwenda Kwa Ziara ya kikazi ya siku tano tarehe 21 April, 2012.

Kwa hivyo basi Rais hajapata taarifa yeyote rasmi kutoka kwa Waziri Mkuu, na bado anasubiri kupewa taarifa hyo rasmi Kwa vile suala la tuhuma hizo limetokea Bungeni.

Na kama kuna Waziri ambaye ameandika barua ya kujiuzulu, basi atakua amemuandikia Rais na kama zipo Rais ndiye atakaye zipokea na kuamua hatua inayofuatia.


Kwa hivyo sio busara hata kidogo kwa vyombo vya habari kueneza uongo na fitna zenye lengo la kuchonganisha si viongozi tu, bali hata viongozi na wananchi kwa ujumla.


Rais Kikwete anatarajia kurejea nchini kesho tarehe 23 April mara baada ya maziko.


Imetolewa na Premi Kibanga,


Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi

Blantyre -Malawi.

22 April, 2012
 
Tupeni na mchanganuo wa safari yake tena kama hajatumia mamilion yetu.Hajapumzika huyo tena.Yuko wapi makamu wake?
 
Duu!. hii kali.! Waziri mkubwa hajalala tangu ijumaa. Halafu Mkuu wa nchi anaendelea na ziara nje ya nchi? Inamaana ameshindwa kumuomba makamu wake akamuwakilishe huko malawi?. Ngoja tusubiri kwanza taarifa ya MP leo bungeni, tutapata pa kuanzia.
 
Hivi hii taarifa ya Premi Kibanga mbona imechomekewa pia kanusho la Salva Rweyemamu kuhusu JK na mawaziri wake? Kumbe kati ya Premi Kibanga na Salva Rweyemamu nani bosi wa mwenzie? Salva kaandika akiwa Dar, Premi kaandika akiwa Blantyre habari hiyohiyo siku hiyohiyo, hawana mawasiliano? Hawagawani majukumu? Na tunashika la Salva au la Premi?
 
There is something wrong somewhere,nadhani ni wakati wa wananchi kuchukua maamuzi magumu na makini sana!
 
Back
Top Bottom