mkuu hiyo ni taarifa ya jikoni magogoni. amini usiamini.
Kwenye Press release ya Ikulu leo Kurugenzi ya mawasiliano wanasema hivi:
"....Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Brazil, amerejea jana Aprili 21, 2012 jioni. Hajaonana wala kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Mhe. Pinda. Hivi sasa Mhe. Rais anasubiri kupata taarifa rasmi kutoka Bungeni Dodoma".
Sasa ningeomba kuuliza, rais anasubiri taarifa ya bunge au yuko safarini (tena) huko Malawi? kwa taarifa hiyo ya Ikulu rais hana habari kuhusu nini kinaendelea hapa nchini maana 'hajafanya mazungumzo na waziri mkuu". Yaani amefika nchini na kuondoka bila kujua chochote? Na anasubiri nini kama hajaongea na PM?
Binafsi naona hapa washauri wa rais wamemwangusha. Inakuwaje rais ahairishe safari kutokana na kifo cha mcheza sinema (Kanumba) lakini sio wakati nchi iko kwenye hali tete kama sasa? Kwa nini asimtume Makamu wa rais amwakilishe kwenye hayo mazishi? Priority yake ni ipi? Tanzania first? au foreign leaders first? Kama ni kweli yuko Malawi italeta tafsiri mbaya sana.
Si mnajua Rais wetu mtu wa watu jamani? Hakosi misiba ilimradi tu kuwe na vyombo vya habari aweze kuuza sura
Ikulu kuna popobawa hapakaliki!
Si mnajua Rais wetu mtu wa watu jamani? Hakosi misiba ilimradi tu kuwe na vyombo vya habari aweze kuuza sura
Huyu jamaa JK kwa kula bata anatisha, akiwa Malawi lazima atafanya maombi utokee msiba sehemu nyingine duniani aende. Hapa alishindwa kwenda kumzika mkuu wa jeshi mstaafu akatuma mwakilishi lakini Malawi hataki kutuma mwakilishi