Rais Kikwete awasili mjini Blantyre, Malawi kushiriki mazishi ya Mutharika

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
Tanzania nchi yangu nakupenda kwa moyo wote. Nitafia hapahapa Tanzania.

Rais...amewasili...Malawi leo jioni kuhushuria Mazishi...anatarajia kurejea nchini kesho tarehe 23 April mara baada ya maziko - P. Kibanga





TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI




Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Blantyre ,Malawi leo jioni kuhushuria Mazishi ya Profesa Bingu wa Mutharika, aliyekuwa Rais wa Malawi., aliyefariki tarehe 5 April, 2012 Kufuatia matatizo ya Moyo

Rais Kikwete ni miongoni mwa Viongozi wakuu Saba kutoka nchi jirani na Malawi.

Nchi hizo ni Afrika Kusini, Benin, Kenya, Msumbiji, Zimbabwe na Zambia.


Wakati huohuo Ikulu inapenda kukanusha taarifa zilizonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari kudai kuwa Rais ametofautiana na Waziri Mkuu kuhusu aina ya hatua za kuwachukulia Mawaziri wanaotuhumiwa na ubadhirifu katika Wizara zao.

Napenda kueleza Umma kuwa taarifa hizo si za kweli.

Pia nitumie nafasi hii kuwatahadharisha waandishi wa habari kuwa makini, waangalifu na wachambuzi wakati wa kupokea, kusikiliza na kuandika au kutangaza taarifa wanazopata.

Rais kikwete aliwasili kutoka Brazil alipokuwa amekwenda Kwa Ziara ya kikazi ya siku tano tarehe 21 April, 2012.

Kwa hivyo basi Rais hajapata taarifa yeyote rasmi kutoka kwa Waziri Mkuu, na bado anasubiri kupewa taarifa hyo rasmi Kwa vile suala la tuhuma hizo limetokea Bungeni.

Na kama kuna Waziri ambaye ameandika barua ya kujiuzulu, basi atakua amemuandikia Rais na kama zipo Rais ndiye atakaye zipokea na kuamua hatua inayofuatia.


Kwa hivyo sio busara hata kidogo kwa vyombo vya habari kueneza uongo na fitna zenye lengo la kuchonganisha si viongozi tu, bali hata viongozi na wananchi kwa ujumla.


Rais Kikwete anatarajia kurejea nchini kesho tarehe 23 April mara baada ya maziko.


Imetolewa na Premi Kibanga,


Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi

Blantyre -Malawi.

22 April, 2012
 
I see huyu jamaa nafkiri mgonjwa tumsifuni kwa roho Yake ngumu kama chuma..ewe mwenyezi mungu tuokoe na hili janga.
 
Kasign resignation zao mwache akale raha. Mwalimu angechelewa kufa asingeupata
 
ila kikwete anadharau mbaya..huyu inabidi siku moja akirudi akute ikulu imetekwa.
 
Jamani mbona anatia aibu alimteua makamu wa raisi wa nini si anaweza kufanya kazi zote bila msaidizi.BIG UP VASCO DA GAMA
 
hamna mapumziko wala kutuma mwakilishi, akiondoka madarakani atakuwa na picha za dunia nzima
 
Kwenye Press release ya Ikulu leo Kurugenzi ya mawasiliano wanasema hivi:

"....Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Brazil, amerejea jana Aprili 21, 2012 jioni. Hajaonana wala kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Mhe. Pinda.
Hivi sasa Mhe. Rais anasubiri kupata taarifa rasmi kutoka Bungeni Dodoma".


Sasa ningeomba kuuliza, rais anasubiri taarifa ya bunge au yuko safarini (tena) huko Malawi? kwa taarifa hiyo ya Ikulu rais hana habari kuhusu nini kinaendelea hapa nchini maana 'hajafanya mazungumzo na waziri mkuu". Yaani amefika nchini na kuondoka bila kujua chochote? Na anasubiri nini kama hajaongea na PM?

Binafsi naona hapa washauri wa rais wamemwangusha. Inakuwaje rais ahairishe safari kutokana na kifo cha mcheza sinema (Kanumba) lakini sio wakati nchi iko kwenye hali tete kama sasa? Kwa nini asimtume Makamu wa rais amwakilishe kwenye hayo mazishi? Priority yake ni ipi? Tanzania first? au foreign leaders first? Kama ni kweli yuko Malawi italeta tafsiri mbaya sana.
 
Si mnajua Rais wetu mtu wa watu jamani? Hakosi misiba ilimradi tu kuwe na vyombo vya habari aweze kuuza sura
 
teh teh huku nyumbani kunaungua. sasa si mchomo nyumba moto tu ili akiudi akose pa kufikia. upuuzi huu! kuna mambo ya msingi ya kufanya kuliko huo msiba kipindi hiki. anyway kama tanzania daima walivyosema kilichopo TZ ni upepo wa muda tu. so why should he care kama utatulia? kalakabahoo wa tz tumeliwa
 
we mwache tu sasa utaamini kwamba serikali ya nchi hii sio sikivu makamu wa raisi yupo wapi kwani hawezi kwenda dr shein kuiwakilisha muunganano? naamni sasa kwamba hakuna waziri atakae jiuzulu hata mmoja Mungu itazame tanzania kweli mungu anakazi "wabariki viongozi wake" ni moja ya maneno katika wimbo wa taifa
 
Jamani mbona anatia aibu alimtaka makamu wa raisi wa nini si anaweza kufanya kazi zote bila msaidizi.BIG UP VASCO DA GAMA

ujuwe nilipopata ile taarifa ya ikulu vs tanzania daima na kusikia hii mpya ya kwamba kawasili malawi nikajuwa katua blantaya akitokea kwa maximo. kumbe kalala magogoni, na leo anaenda kula ubwabwa wa hitma kwa bingu.
 
Back
Top Bottom