Rais Kikwete awasili jijini Kampala kuhudhuria mkutano wa EAC

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,571
[h=2]Rais Kikwete awasili jijini Kampala kuhudhuria mkutano wa EAC....Maada kuu watakazoongelea ni pamoja na Sarafu moja ya jumuiya ya Afrika Mashariki[/h]




1.png
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama wa Uganda muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki.
*****************

Wakuu wa nchi zinazounda jumuiya ya Africa Mashariki wanakutana leo tarehe 30 Novemba huko Kampala, Uganda.

Wakuu hao ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, Yoweri Mseveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Pierre Nkuruzinza wa Burundi na Uhuru Kenyatta wa Kenya.


Masuala watakayozungumzia leo ni pamoja na soko la pamoja, umoja wa forodha, shirikisho la kisiasa na umoja wa sarafu ambapo leo watatia saini mkataba wa kuwa na sarafu moja.
 
mkuu R.B leo umenichanganya kidogo au hii post ya zamani?
mbona tulitengwa au Tz tumejialikisha?
 
Last edited by a moderator:
Kweli hatutoki EAC na kama kutoka tutakuwa wa mwisho tena kwa hiyari yetu...sisi ni wanachama waaminifu wa jumuia hiyo tangu enzi na enzi hata kama wanatubagua....
 
Naomba aonane na wanajeshi waliotimuka wa m23 kwenye kambi za jeshi la uganda
 
mbona simuoni mwenyeji wake M7? siku akija M7 dar,tumpe kova akampokee.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom