BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,011
Posted Date::11/20/2007
Kikwete awashtukia wanaoomba misamaha ya kodi
Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi
RAIS Jakaya Kikwete ameshtukia baadhi ya asasi zinazoomba misamaha ya kodi na kuitaka Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), kuchunguza kwa kina waombaji ili kuepuka ujanja katika ukwepaji kodi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika maadhimisho ya pili ya siku ya walipa kodi, Rais Kikwete alihoji na kutilia shaka kama watu wanaopata misamaha ya kodi wote wanastahili kufanyiwa hivyo.
"Hivi ni kweli wote wanaopata misamaha ya kodi wanastahili, tuangalie upya, nafikiri ni wakati wa kufanya utafiti wa kina kabla ya kuruhusu misamaha ya kodi," alisema Rais.
Alisema siku hizi kumekuwa na kasi ya kuanzishwa Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs) lakini baadhi zimekuwa zikidai kusaidia jamii na kupata misamaha ya kodi, ambayo baadaye hutumia fursa hiyo kufanya biashara.
Rais Kikwete alitoa mfano wa asasi moja ya Manyoni Mkoani Singida, ambayo iliomba msahama wa kodi kwa madai ya kulea watoto yatima lakini ikaja kubainika inasafirisha sukari ya biashara ambayo ilikamatwa Makambako Iringa.
"Mfano wa NGO ya Manyoni Singida, ilijieleza inalea watoto yatima, lakini ikaja kukamatwa na sukari eneo la Makambako, inakuwaje?" alihoji Rais.
Licha ya kuitaka TRA kuchunguza waombaji wa misamaha ya kodi, lakini pia aliitaka mamlaka hiyo kudhibiti uvujaji wa mapato katika maeneo ya mipakani na bandarini.
Rais Kikwete alisema pamoja na mamlaka hiyo kufanya vizuri lakini bado maeneo ya mipaka na bandari yamekuwa yakiikosesha serikali mapato.
Alisema bado kuna ulegevu katika ukusanyaji mapato mipakani na bandarini na kuitaka TRA, isiruhusu hali hiyo kuendelea.
Rais alimwagiza Waziri wa Fedha Zakia Meghji, kuchukua hatua za haraka katika sehemu zote zenye mapungufu na kama akishindwa afikishe suala hilo kwake achuke maamuzi.
Awali Meghji akimkaribisha Rais, alisema TRA imekuwa ikifanya kazi kwa ufanisi mkubwa hadi kufikia kukusanya zaidi ya sh 320 bilioni katika kipindi cha mwezi Septemba.
Meghji alisema matarajio ni kuona makusanyo yakizidi kuongezeka na kuvuka rekodi katika kipindi cha mwezi ujao na Machi.
Alisema wizara itaendelea kuhakikisha mapato ya serikali yanaongezeka ili yaweze kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa (GDP).
Kwa upande wake Elisante Muro, akizungumza kwa niaba ya walipa kodi alisema ingawa TRA imeweza kuboresha mbinu za ukusanyaji kodi, bado inapaswa kuangalia vyanzo vipya.
Muro alisema tatizo jingine ni ubadilikaji wa viwango vya kodi mara kwa mara na kupendekeza viwango hivyo viwe vinadumu kwa angalau miaka mitano ili kuwezesha walipa kodi kukuza mitaji yao.
Katika siku hiyo jumla ya makampuni 10 walipa kodi yalitangazwa kuwa washindi kitaifa huku Kampuni ya Sigara (TCC) ikiwa ya kwanza baada ya mwaka jana kulipa kodi takriban sh 70 bilioni.
Nyingine ambazo zimo katika tatu bora ni Kiwanda cha Kutengeneza Saruji cha Tanzania Portland na Mamlaka ya Bandari (TPA). Nyingine ambazo zimo katika kumi bora ni Benki ya CRDB, NBC LTD, NMB, Kilombero Sugar, Standard Chartered, Shirika la Umeme (Tanesco) na Kampuni ya Songas.