Rais Kikwete awashtukia wanaoomba misamaha ya kodi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,929
287,589
Posted Date::11/20/2007
Kikwete awashtukia wanaoomba misamaha ya kodi
Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

RAIS Jakaya Kikwete ameshtukia baadhi ya asasi zinazoomba misamaha ya kodi na kuitaka Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), kuchunguza kwa kina waombaji ili kuepuka ujanja katika ukwepaji kodi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika maadhimisho ya pili ya siku ya walipa kodi, Rais Kikwete alihoji na kutilia shaka kama watu wanaopata misamaha ya kodi wote wanastahili kufanyiwa hivyo.

"Hivi ni kweli wote wanaopata misamaha ya kodi wanastahili, tuangalie upya, nafikiri ni wakati wa kufanya utafiti wa kina kabla ya kuruhusu misamaha ya kodi," alisema Rais.

Alisema siku hizi kumekuwa na kasi ya kuanzishwa Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs) lakini baadhi zimekuwa zikidai kusaidia jamii na kupata misamaha ya kodi, ambayo baadaye hutumia fursa hiyo kufanya biashara.

Rais Kikwete alitoa mfano wa asasi moja ya Manyoni Mkoani Singida, ambayo iliomba msahama wa kodi kwa madai ya kulea watoto yatima lakini ikaja kubainika inasafirisha sukari ya biashara ambayo ilikamatwa Makambako Iringa.

"Mfano wa NGO ya Manyoni Singida, ilijieleza inalea watoto yatima, lakini ikaja kukamatwa na sukari eneo la Makambako, inakuwaje?" alihoji Rais.

Licha ya kuitaka TRA kuchunguza waombaji wa misamaha ya kodi, lakini pia aliitaka mamlaka hiyo kudhibiti uvujaji wa mapato katika maeneo ya mipakani na bandarini.

Rais Kikwete alisema pamoja na mamlaka hiyo kufanya vizuri lakini bado maeneo ya mipaka na bandari yamekuwa yakiikosesha serikali mapato.

Alisema bado kuna ulegevu katika ukusanyaji mapato mipakani na bandarini na kuitaka TRA, isiruhusu hali hiyo kuendelea.

Rais alimwagiza Waziri wa Fedha Zakia Meghji, kuchukua hatua za haraka katika sehemu zote zenye mapungufu na kama akishindwa afikishe suala hilo kwake achuke maamuzi.

Awali Meghji akimkaribisha Rais, alisema TRA imekuwa ikifanya kazi kwa ufanisi mkubwa hadi kufikia kukusanya zaidi ya sh 320 bilioni katika kipindi cha mwezi Septemba.

Meghji alisema matarajio ni kuona makusanyo yakizidi kuongezeka na kuvuka rekodi katika kipindi cha mwezi ujao na Machi.

Alisema wizara itaendelea kuhakikisha mapato ya serikali yanaongezeka ili yaweze kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa (GDP).

Kwa upande wake Elisante Muro, akizungumza kwa niaba ya walipa kodi alisema ingawa TRA imeweza kuboresha mbinu za ukusanyaji kodi, bado inapaswa kuangalia vyanzo vipya.

Muro alisema tatizo jingine ni ubadilikaji wa viwango vya kodi mara kwa mara na kupendekeza viwango hivyo viwe vinadumu kwa angalau miaka mitano ili kuwezesha walipa kodi kukuza mitaji yao.

Katika siku hiyo jumla ya makampuni 10 walipa kodi yalitangazwa kuwa washindi kitaifa huku Kampuni ya Sigara (TCC) ikiwa ya kwanza baada ya mwaka jana kulipa kodi takriban sh 70 bilioni.

Nyingine ambazo zimo katika tatu bora ni Kiwanda cha Kutengeneza Saruji cha Tanzania Portland na Mamlaka ya Bandari (TPA). Nyingine ambazo zimo katika kumi bora ni Benki ya CRDB, NBC LTD, NMB, Kilombero Sugar, Standard Chartered, Shirika la Umeme (Tanesco) na Kampuni ya Songas.
 

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,189
53
Yaani Huyu Kikwete hadi anachekesha, yaani hapa imebidi nicheke na nimeanza kutoa maelezo kwa nini nimecheka so kwa nguvu wakati wa kazi.

Huyu baba yeye kila siku amegundua au kushtukia watu, baada ya hapo hakuna kitu anachofanya. Nimesoma hili nikajiuliza kama JK ndio kwanza ameingia TZ baada ya kuishi uhamishoni for years or samthin'

Yaani yeye kila siku amegundua:

watendaji wabovu, wauza unga, mafisadi 38, majambazi, utendaji mbovu wa mawaziri wake, wanamtandao wanafilisi nchi, nk

Akishagundua hilo na kutoa vitisho magazetini, kesho anapanda zake ndege kuzunguka dunia na kufanya umatonya!

Kuna watu wanataka this guy afike mwaka 2015, mbona nchi yote itakuwa imebadilishwa jina na kuitwa Aziz au Smith?
 

Dua

JF-Expert Member
Nov 14, 2006
3,233
657
Ataacha kugundua lini na kufanya kile ambacho anatakiwa kukifanya?

BTW hivi ni vidagaa tu vipi kambale wanaojulikana kutoka kila sehemu?
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,929
287,589
Ataacha kugundua lini na kufanya kile ambacho anatakiwa kukifanya?

BTW hivi ni vidagaa tu vipi kambale wanaojulikana kutoka kila sehemu?

Hapo umesema kweli tupu, maana katoa mfano wa NGO! wakati Manji mpaka leo anakwepa kulipa 1.3 billion baada ya kuuza magodown yake. Huyu Manji ni mtu wa karibu naye sana alimsaidia sana kwenye kutafuta mgombea wa CCM 2005. Na kuna matajiri wengine chungu nzima wanaokwepa kulipa kodi kila siku.
 

Koba

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
6,132
1,333
mbona katika hayo makampuni yanayolipa kodi nyingi Barric haimo
 

tauphiq

Member
Sep 5, 2007
14
0
Jamani mwache ashutuke si mnajua tena muda mwingi huwa yuko nje ya nchi na ndio tu katua jana.

Sasa mie namwona ayaangalie makampuni yetu yanayoomba misamaha ya VAT kwa malighafi zinazoagizwa nje ya nchi maana makampuni mengi hasa ya kutengeneza madawa wanaomba misamaha hii lakini wanapata faida kubwa lakini hawatoi taarifa sahihi.
\

Pia je makampuni yaliyouzwa na serikani ambao baadhi bado serikali ina hisa huko yana hali gani??
Kuna viwanda vipo lakini havitengenezi faida miaka zaidi ya 10 tangu kuuzwa kwake na je serikali ya JK inaviona?? na je hawa ana mpango gani nao maana viwanda hivi havina manufaa kwa serikali pamoja na ukweli kwamba viliuzwa kwa upendeleo kwani waliouziwa hawawezi kuviendesha na mfano mzuri ni kiwanda cha madawa cha KEKO.

Jamani mbona kina kufa wakati serikali ina 40% share????? Au ile 40% haipo tena??
Naomba JK avitembelee viwanda vyote vilivyouzwa na serikali zilizopita ili kuona manufaa yake kwa watanzania. Kama wameshindwa serikali ivichukue kwani ni hazina inayo zidi kuharibika kwa taifa letu.
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
37,537
65,077
Hii miaka miwili mimi nimechoka kabisa na vioja vya muungwana,sijui hali itakuwaje hadi hiyo 2010. Naijutia kura yangu.
 

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
4,977
774
JK kama kiongozi wa taifa anatakiwa awe mfano katika kuchangia maendeleo ya taifa. JK akiwa kama rais anapokea mshahara bila kukatwa kodi (PAYE) kama watumishi wengine. Wakati sasa umefika kwa sheria mbovu ambazo ni za kubagua watumishi kwa matabaka ya nafasi zao za utumishi kufutwa. JK anapokemea misamaha ya kodi tunategemea sasa atatoa idhini kwa waziri wa fedha ambao ndio wanaoandaa mshahara na marupurupu yake yaanze kukatwa kodi.
 

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,812
629
Hii miaka miwili mimi nimechoka kabisa na vioja vya muungwana,sijui hali itakuwaje hadi hiyo 2010. Naijutia kura yangu.

Heri mimi sikupiga kura kwi kwi kwi!!!!

Huenda huyo ndiye alikuwa bora katika wote waliokuwepo. Tutaendelea kukataa, lakini tatizo la Tanzania ni kubwa zaidi ya uwezo wa rais. Tungekuwa na rais mwenye uwezo ingesaidia lakini bado matatizo yetu yanaanzia chini kabisa. Yanahitaji mabadiliko katika utamaduni wetu wa kupenda vya bwerere na badala yake kuthamini kazi. Mabadiliko ya kuchukia wizi na dhuluma na kuheshimu haki ya mtu hata kama hana sauti kama sisimizi.

Kadri ninavyopita kwenye maofisi ya serikali, vyombo vingine vya kutoa haki kwa umma, ninazidi kuishiwa nguvu.

Huku kwa wenzetu kilicho imara ni system na ndio maana wanaweza kupata rais bwege kama Bush lakini bado nchi ikaenda. Chini kuna watu wanaoweza kufanya kazi bila kujali rais anasema nini, lakini sisi kila siku tunapiga siasa tu, watu wanakufa sisi ni siasa tu. Ndio maana rais naye anaongea kama msanii na hapati matatizo yoyote.
 

Simabwachi

JF-Expert Member
Mar 31, 2017
306
391
Duuuh hili nalo ni kaburi limefukuliwa, endeleeni kufukua mie nawasubiri kina Shivji, Kabudi, Luoga na wengineo walete mrejesho wa namna tutakavyolipwa dolari zetu na Barrick Gold
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom