Rais Kikwete awapandisha vyeo makanali

Obama,umekosea sana.Vyeo jeshini vina sifazake ili upande na sio kumju Cdf au kuwa karibu na Amiri jeshi karibu. Mwombe
 
Hata kwenye majeshi hawamo,inatisha,inabidi wazingatie mawaidha ya Mufti kuwa wasiitupe elimu dunia na kuangalia upande mmoja,watabaki kulalamika kila siku.

sasa wewe unaangalia watu kwa dini zao wakati humjui hata mmoja wao na uwezo wao kikazi. angechagua waislamu wengi ungesema ana udini. wakati mwingine tusikashifu watu tu kwasababu tunahaja ya kuponda kila kitu.

mtazamo wako wa kuangalia majina na dini na kabila za watu umenikera, tubadilike; kweli sijapenda
 
Hivi mnadharau ADC kwa kuwa Ana Beba bag ...huyoo Ana kazi kubwa Sana ....anamwandalia Rais mambo mengi ..na ni Mkuu wa motorcade popote Rais alipo...na mengine mengi....anatumika pia kuangalia Usalama wake akishirikiana na maafisa wa Usalama .....kuacha hayo anatakiwa kuwa na Elimu ya field na utambuzi ...yaani uwezo wa kusoma mazingira haraka...na kuamua...hayo yote hayapatikani..bila mafunzo STAHIKI ......kimsingi cheo chake Huwa kanali...na pale ni Kama anatongoza kikosi Kizima...kwa kazi zake......
huwezi kupewa cheo bila kufanya mafunzo jeshini.....KIMSINGI KAMA UTARATIBU UTAFUATWA ..ATAKOMA KUWA ADC....Kwani kwa cheo cha Brigedia Sasa AdC ni jukumu dogo kwake atahitaji kupewa more roles jeshini....NI WAZI KARIBUNI RAIS ATAANZA KUONEKANA NA ADC MPYA.....HUYO ATARUDISHWA KAMBINI......
ADC WA RAIS MKAPA ( brig gen simuli )ALIPANDISHWA CHEO BAADA YA RAIS MKAPA KUMALIZA TU ...NAYE AMERUDI KAMBINI...
Huyu ni msaidizi wa karibu wa Rais. Mkuu wa msafara wa Rais ni Mkuu wa Protokali.ADC ni 'ceremonial' zaidi..
 
Nikitumia slogan ya book 7, mbona wengi wao ni wa Kaskazini, ina maana Mkuu wa Majeshi naye ni CDM?
Tiba

Ukitumika 'u-kaskazini' mbona wataenda mbali.Majaji wa Mahakama Kuu wamejaa,Majaji wa Mahakama ya Rufaa wamo, Polisi usiseme,Jeshi la Magereza ndiyo majanga..
Swali la kizushi - mbona wakina Ibra wako watatu tu..??
 
Hongereni makanda. lakini mbona makamanda kama kina Sukambi Mahela, au kina Msindai, Mfikirwa, Msingiri, Mwaya, Masalamado n.k- walioshughulika kule Comoro hawamo? Amiri Jeshi tafadhali wakumbuke!!
<br>
<em>
Kama kweli uloandika ni mwenye jina hilo hapo juu basi bado tuna safari ndefu.Kifupi vyeo vya kijeshi ni zaidi ya unavyojua. Kuwataja majina marafiki zako, sana sana ni kuwaharibia tu. Ni sawa na mimi nianze kuhoji kwa nini rafiki yangu mwandishi mwenye cerrtificate&nbsp; asiwe mhariri wa gazeti lako au kwa nini hajawa mwenyekiti au katibu wa mct. Labda ndo tafsiri ya uhuru wa vyombo vya habari mnaouzungumzia-ga.
 
Ukitumika 'u-kaskazini' mbona wataenda mbali.Majaji wa Mahakama Kuu wamejaa,Majaji wa Mahakama ya Rufaa wamo, Polisi usiseme,Jeshi la Magereza ndiyo majanga..
Swali la kizushi - mbona wakina Ibra wako watatu tu..??

Mungo Park, huko unakokwenda mimi simo!!!!!!

Tiba
 
Vipi Kuhusu ndugu zetu wa Zanzibar, sijawaona akina Makame Kabisa hapa aisee, kulikoni jaman, na pia Majina ya wale walalamishi naona yako kama matatu tu, Elimu Dunia ni muhimu jaman pia as well.
 
Hata wewe umesema “kama ana sifa”, sasa wewe unadhani huyo Kimario ana sifa gani ya ziada zaidi ya huo upambe wake kwa M.k.w.e.r.e? Hebu zitaje basi kama wewe unazijua!

.........kwani 'upambe' peke yake hauwezi kuwa ni sifa !?.......kuna mwanajeshi mmoja alikerwa na mbunge mmoja hivi, yule Major Gen, alimuambia yule mbunge kuwa yeye wakati wowote anaweza kuwa 'mbunge', lakini yeye hawezi kuwa Major Gen.
Na huo ni ukweli !
 
Vipi Kuhusu ndugu zetu wa Zanzibar, sijawaona akina Makame Kabisa hapa aisee, kulikoni jaman, na pia Majina ya wale walalamishi naona yako kama matatu tu, Elimu Dunia ni muhimu jaman pia as well.

Nyie ndio wenye nchi !..........tengenezeni tu 'gap' na majibu mtayapata !:A S 27:
 
Hongereni makamanda weredi na nidhamu mbele daima !
Yaonekana wastaafu wamekuwa wengi sana mwaka huu one General star 28 kwa mpigo? Duuu nao ukute hawana zaidi miaka. 5 wanastaafu
 
Dar es Salaam.Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, amewapandisha vyeo maofisa 28 kutoka Kanali na kuwa Brigedia.

Huku Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Samweli Ndomba akiwataka maafisa hao kuchapa kazi kwa bidii ili kuongeza ufanisi wa Jeshi.

Hatua ya Rais Kikwete kuwapandisha vyeo maofisa hao imefanywa kwa mujibu wa kanuni za Majeshi ya Ulinzi inayompa mamlaka kufanya hivyo.

Wakati Rais Kikwete akiwapandisha vyeo maofisa hao, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Samweli Ndomba kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, amewataka kuendelea kuchapa kazi kwa bidii ili kuleta tija na maendeleo jeshi.

Pia mnadhimu huyo amewasisitizia maafisa hao kusimamia nidhamu na uwajibikaji kwa sababu ndiyo msingi wa mafanikio katika utendaji wa jeshi.

“Napenda kuwakumbusha suala na nidhamu ni jambo muhimu kwani ndiyo kioo chetu katika jeshi hivyo nasisitiza kuendelea kuzingatia jambo hilo. Lingine ambalo ningependa tuendelea kulizingatia ni kufanya kazi kwa weledi,” alisema.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na JWTZ, maofisa waliopandishwa vyeo ni pamoja na Kanali Denis Raphael Janga, Kanali Jason Nestor Musikula, Kanali Jackson King Mrema, Kanali Martin Amos Kemwaga, Kanali Joseph Cosmas Chengelela, Kanali Martin Nikubuka Mwankanye, Kanali Harold Kidundi Mziray, Kanali Emmanuel Peter Kapesa na Kanali Mwita Wambura Isamulyo.

Wengine ni Kanali Francis Asilia Njau, Kanali Pendo Uledi Kamungwele, Kanali Moses Adolph Shinyambala, Kanali Ibrahim Abdarahamani Kimario, Kanali Michael Garo Luwongo, Kanali Nelson Hosea Msanja,Kanali Blasius Kalima Masanja, Kanali Aloyce Damian Mwanjile, Kanali Rajabu Goma Hanti na Kanali Ignas Beatus Mubofu.

Pia wamo Kanali Dominic Basil Mrope, Kanali Hamis Issa Majumba, Kanali Salehe Omari Semtaua, Kanali Henry Sweko Kamundo, Kanali Sylivester Msafiri Minja, Kanali John Bangantagoka Bishoge, Kanali Anselm Shigongo Bahati, Kanali Robinson Mboli Mwanjela na Kanali Kaisy Philip Njelekela.

Source Mwananchi 22/01/2014
 
All the best new Generals. Inaelekea jeshi limepanuka sana kiasi kwamba lina mahitaji mengi ya magenerali kwa kipindi chetu...hope so...
 
All the best new Generals. Inaelekea jeshi limepanuka sana kiasi kwamba lina mahitaji mengi ya magenerali kwa kipindi chetu...hope so...

Kuwa Kanali ina maana unakuwa ni incharge wa Regiment na kwa kwa kupewa commission ya kuwaa Brigadier ina maana watakuwa wakuu wa brigade zenye battalion tatu (approx Troops 3000)
 
Kikwete kafanya hivyo bila kuzingatia mahitaji halisi ya jeshi na uwezo wa nchi kuwahudumua magenerals wengi.Ukipiga hesabu za haraka haraka unaweza kuta nchi itatumia 5 bilioni kuwahudumia watu 28 huku huduma za maji,umeme na miundo mbinu ikizidi kudorora.

Mwaka jana alipandisha vyeo mabrigadia wengi pamoja na major general kibao mwaka huu tena karudia mchezo ule ule.
 
... maofisa waliopandishwa vyeo ni pamoja na Kanali Denis Raphael Janga, Kanali Jason Nestor Musikula, Kanali Jackson King Mrema, Kanali Martin Amos Kemwaga, Kanali Joseph Cosmas Chengelela, Kanali Martin Nikubuka Mwankanye, Kanali Harold Kidundi Mziray, Kanali Emmanuel Peter Kapesa na Kanali Mwita Wambura Isamulyo.

Wengine ni Kanali Francis Asilia Njau, Kanali Pendo Uledi Kamungwele, Kanali Moses Adolph Shinyambala, Kanali Ibrahim Abdarahamani Kimario, Kanali Michael Garo Luwongo, Kanali Nelson Hosea Msanja,Kanali Blasius Kalima Masanja, Kanali Aloyce Damian Mwanjile, Kanali Rajabu Goma Hanti na Kanali Ignas Beatus Mubofu.

Pia wamo Kanali Dominic Basil Mrope, Kanali Hamis Issa Majumba, Kanali Salehe Omari Semtaua, Kanali Henry Sweko Kamundo, Kanali Sylivester Msafiri Minja, Kanali John Bangantagoka Bishoge, Kanali Anselm Shigongo Bahati, Kanali Robinson Mboli Mwanjela na Kanali Kaisy Philip Njelekela.
Hapa katupendelea akina sisi
Sio kwamba alipenda kutupendelea akina sisi, ila alilazimika kuwapandisha kutokana na taaluma zao na utumishi wao jeshini. Ingekuwa ni zile teuzi zisizozingatia taaluma, angewajaza jamaa. Sasa subiri teuzi zile zije kwenye kumi na nane yake, atapiga vyeo majamaa hadi mnabaki kujiuliza vigezo! Bahati nzuri baadhi ya positions analazimika kwa kuwa anapelekewa list na wataalam, yeye anakuwa pale just for his ceremonial position
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom