Rais Kikwete awaagiza TAWIRI kufanya uchunguzi wa upotevu wa wanyama waitwao palahala!

Hakikwanza

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
4,034
1,003
Katika hali ya kustaajabisha nimesikia leo kutoka magazetini Mh Jk amewaagiza TAWIRI kufanya uchunguzi kuhusu utowekaji huo; wakati nijuavyo mimi yeye Rais ni mhusika mkuu. Ukiangalia juzijuzi tu ndege ya Jeshi la Quatar ilitua KIA na kupakia wanyama kibao wa aina mbalimbali na kutoweka.Rais kama mkuu wa nchi hajatolea tamko hili. Je anapata wapi nguvu za kutoa maagizo haya wakati yeye ndio msababishaji mkubwa? hii ni kufuru kubwa na kutuona sisi watanzania ni mabwege. Sasa nchi mbalimbali zimeanzisha zoo zenye miundombinu yote ktk nchi zao kwa wanyama wanao watoa huku kwetu kwa bei ya kutupwa toka kwa vigogo wetu, hivyo watalii wengi tunawakosa. Wakati ilitakiwa tuwalinde wanyama wetu wao wajekuwa angalia hapahapa na uwe urithi wetu na vizazi vijavyo. Kweli rais tunaye.
 
Back
Top Bottom