Rais Kikwete ateua makatibu wakuu wa wizara

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,876
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa Makatibu Wakuu watano wapya na kuwahamisha wengine wanne kutoka wizara moja kwenda nyingine. Uteuzi na uhamisho huo unaanza mara moja.

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Februari 28, 2011, mjini Dar Es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Ndugu Phillemon L. Luhanjo inasema kuwa mabadiliko hayo yanatokana na Muundo mpya wa Serikali ambako Wizara ya Miundombinu imegawanywa katika wizara mbili, na baadhi ya Makatibu Wakuu kustaafu kazi kwa mujibu wa Sheria.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Kikwete amemteua Bw. Fanuel E. Mbonde kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Ikulu. Kabla ya uteuzi wake Bw. Mbonde alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu.

Wengine walioteuliwa ni B. Hussein A. Kattanga kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa; Bw. John M. Haule kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa; Bw. Herbert E. Mrango kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi; na Bw. Eric K. Shitindi kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi na Ajira.

Kabla ya uteuzi wake Bw. Kattanga alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto; Bw. Haule alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha; Bw. Mrango alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Bw. Shittindi alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Kuhusu uhamisho, Rais Kikwete amemhamisha Bw. Sazi B. Salula kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenda kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais; Bibi Maimuna K. Tarishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwenda Wizara ya Maliasili na Utalii; Injinia Omar A. Chambo kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi akitokea Ukatibu Mkuu wa Wizara ya zamani ya Miundombinu; na Bibi Kijakazi R. Mtengwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.

Taarifa hiyo ya Ndugu Luhanjo imesema vile vile kuwa Dkt. Ladislaus C. Komba, aliyekuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii anapangiwa kazi maalum katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Rais Kikwete amemhamishia Bibi Elizabeth J Nyambibo Wizara ya Fedha na Uchumi ambako anachukua nafasi ya Naibu Katibu Mkuu iliyoachwa wazi na Bwana John H. Haule. Kabla ya uhamisho wake, Bibi Nyambibo alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Taarifa hiyo ya Ndugu Luhanjo imesema kuwa Makatibu Wakuu wapya wataapishwa saa tatu asubuhi kesho, Machi Mosi, 2011.

Mwisho.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
28 Februari, 2011
 
kwa hiyo luhanjo kapokelewa mikoba?

Heshima kwako kwelekwelea.

Mkuu nafasi ya katibu mkuu kiongozi bado inashikiliwa na Luhanjo nadhani unachanganya na nafasi ya katibu mkuu ofisi ya rais amabayo kapewa bwana Mbonde.
 
hapo inaonekana Luhanjo anabakia kuwa katibu mkuu kiongozi na Mbonde ni katibu mkuu so Luhanjo ameretain position yake

Inaelekea Luhanjo atastaafu kwa umri muda si mrefu ujao, huu ukatibu mkuu kiongozi ni namna ya kufanya transition kati ya Luhanjo na Mbonde,
 
Kama kawaida hatutarajii jipya kutokana na uteuzi huo. Sanasana ni kwa ajili ya kuendeleza ufisadi:decision:
 
Inaelekea Luhanjo atastaafu kwa umri muda si mrefu ujao, huu ukatibu mkuu kiongozi ni namna ya kufanya transition kati ya Luhanjo na Mbonde,

ukiwa katibu mkuu ofisi ya Rais ikulu inafahamika ndio katibu mkuu kiongozi au siku hizi imebadilika ni watu wawili tofauti?
 
kama JK hajui mmiliki wa Dowans basi Anna Makinda hajui lilipo jengo la bunge Dodoma.
 
Inaelekea Luhanjo atastaafu kwa umri muda si mrefu ujao, huu ukatibu mkuu kiongozi ni namna ya kufanya transition kati ya Luhanjo na Mbonde,
<br />
<br />
Nafasi ya Luhanjo inakwenda kwa George Yambesi aliyekuwa katibu mkuu Menejiment ya U/umma pia ndiye alikuwa kaimu katibu mkuu kiongozi,ukiangalia kule menejimenti kapelekwa mwingine na hawajasema Yambesi anakwenda wapi,hii ni habari ya jikoni kabisa
 
Hivi hizo nafasi zote zipo au mkwere anaongeza akijisikia nadhani hii ni moja ya weaknes za katiba yetu yani rais anateua viongozi kwa matakwa yake.
Sasa unakuta wizara moja waziri,naibu waziri,katibu mkuu,katibu msaidizi wakurugenzi kibao na hatujui nani anafanya nini ila mishahara na allowance kibao ziko palepale. Nikiona hujuma Ya namna hii nakumbuka madai ya katiba mpya jamani tumeisha
 
dah, mbona mm kanisahau?
usijali kwani hata hao waliochaguliwa hawatakaa mda mrefu sana, maan serikali mpya iinakuja na hapo ndio post zote lazima ziwe wazi na kuajiri watu wenye sifa na elimu husika sio kama sasa wanachaguana tu kwa kujuana
 
Hivi hizo nafasi zote zipo au mkwere anaongeza akijisikia nadhani hii ni moja ya weaknes za katiba yetu yani rais anateua viongozi kwa matakwa yake.
Sasa unakuta wizara moja waziri,naibu waziri,katibu mkuu,katibu msaidizi wakurugenzi kibao na hatujui nani anafanya nini ila mishahara na allowance kibao ziko palepale. Nikiona hujuma Ya namna hii nakumbuka madai ya katiba mpya jamani tumeisha
usishangae sana kwani hizo nafasi tutaziondoa zote, siku zinakunaja wala hatutaendelea kuvumilia
waliyoyafanya yanatosha
 
Back
Top Bottom