Rais Kikwete ateua makatibu wa Wizara!

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa, Desemba 30, 2011, amefanya uteuzi wa Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Mkuu na pia amefanya uhamisho wa Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu kuanzia jana, Alhamisi, Desemba 29, 2011.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Phillemon Luhanjo, inasema kuwa Bwana Fanuel E. Mbonde, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Ikulu, anahamishiwa Wizara ya Katiba na Sheria, na Bwana Alphayo Kidata, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Ikulu, anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa Bwana Eliakim C. Maswi, ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Maswi alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Kwa sasa anakaimu nafasi ya Katibu Mkuu, Nishati na Madini.

Mheshimiwa Rais Kikwete pia amemteua Bwana Peter Ilomo, Mratibu Mkuu wa Sera na Mipango, Ofisi ya Rais, Ikulu, kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Ikulu.

Naye Bibi Susan Paul Mlawi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Ikulu. Kabla ya uteuzi huu, Bibi Mlawi alikuwa Msaidizi wa Katibu wa Baraza la Mawaziri (Cabinet Under Secretary) Kamati ya Katiba na Bunge ya Baraza la Mawaziri.

Taarifa ya Bwana Luhanjo inamalizia kwa kusema kuwa mabwana Maswi na Ilomo pamoja na Bibi Mlawi wataapishwa Jumatatu, Januari 2, 2012, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

30 Desemba, 2011
 
Huwa anawaulizi kina nani kufanya uteuzi??? it seems kuna upendeleo uliopita kiasi kwenye teuzi zake sasa hivi..
 
Tumeshamzoea huyu acha afanye ajuavyo. Siku zake zinahesabika hapo kwenye madaraka aliyonayo!
 
Huwa anawaulizi kina nani kufanya uteuzi??? it seems kuna upendeleo uliopita kiasi kwenye teuzi zake sasa hivi..

Mkuu acha tuhuma nyepesi nyepesi, hebu tuambie wewe ulitaka amteue kina nani, hebu tupe majina yao na Cv zao hapa.
 
Huwa anawaulizi kina nani kufanya uteuzi??? it seems kuna upendeleo uliopita kiasi kwenye teuzi zake sasa hivi..

Hahahahaha imekuuma eeh! Pole sana msiwe walalamishi sana pigeni shule kwa sana najua umeuliza swali baada ya kuona majina jamani udini huu utawamaliza kwa kweli
 
Interest ya kujua nani kateuliwa na jakaya iliisha muda mrefu uliopita. Actually, ni tangu ngwe ya kwanza ya Dr. Dr. Dr. (heshima - UDOM) JAKAYA KIKWETE.
 
Kuna jambo moja ambalo kila siku analisahau kulifanya JK na ambalo tutaendelea kumkumbusha nalo ni Kumuhamisha Philemon Luhanjo kutoka Ukatibu Mkuu Kiongozi hadi kwenye Payroll ya Pensheni ya Wastaafu! Hili kila siku analisahau. Anyway tutaendelea kumkumbusha!
 
Tusubiri wale wanaohubiri udini waongee kama kweli wanamaanisha udini ni kuchagua upande mmoja, ama udini kwao ni uislamu?
 
Back
Top Bottom