Rais Kikwete ateua mabalozi wapya. Marmo, Batilda na wengine ndani!

3.jpg
custom_name_congratulations_phd_card-p137422218283970646q6ay_400.jpg

PHD ya Ukweli.
Kumbe ubongo wako Rejao una Gia ya Rivas tu..!!!!!!!!!.
You made my day Litvinienko, are you Russian?
 
Katika watu fyatu huyu Rejao ni mmoja wapo!
We wajua ni fyatu, ila bosi wake alomtuma jamvini anamuona kama lulu.
Anafanya kazi vizuri lakini.
Ila afanye homework kidogo, Angekuwa wa mwisho kabisa kuchallenge PHD (ya ukweli) ya Slaa.
 
Naomba munisaidie,
Dr Batilda Burian ameteuliwa kuwa mjumbe wa bodi ya TRA.Je atakuwa anawajibika vipi akiwa Kenya? au ndio atakuwa analambishwa posho zisizo na tija kuja kwenye vikao?Je hakuna watu/vijana wengine ili mgawanyo wa kazi ugawanywe sawasawa?:lol::lol::lol:
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Hapa ndipo magamba huwa wananiacha hoi. Mtu anakataliwa kuwakilisha jimbo yaani anashindwa kwenye uchaguzi kisha anateuliwa kuwakilisha nchi. Shame on magamba
 
Hata Slaa alikuwa makapi ya CCM..just to remind you
Nyie si washikilia mapembe tu wakati wengine wakikamua kwa mnavyokenulia wengine nilitegemea kusikia Rejao, ritz, FF au mzee angalau mmoja wenu yumo kwenye list.
 
hongera kwa watu walioteuliwa ...ujue wabongo kwa kulalamika tumezidi ....balozi ni mwakilishi binafsi wa rais katika nchi nyingine , na mbunge ni mwakilishi wa wananchi ...sasa kwa kuwa walishindwa ubunge ndio wasiwe mabalozi wapi na wapi ?
 
JK kanisahau dah,si angenipeleka hata Syria au Yemen jamani.Mlioteuliwa mkaiwakilishe Tanzania vyema.
 
wametupwa jalalani na wananchi, jk kaenda kuwaokota kwenye dampo! Kweli jk ni rais.
jk is neither a politician nor a civilian leader he is an army officer who was given political posts and wants to be loved. He is lost
 
Uteuzi leo na kuapishwa tarehe 19/12/11. Lakini ajira yao inaanzia tarehe 12/10/11; hivyo watalipwa malipo ya nyuma kama Mabalozi,kuanzia 12/10/11; huu nao ni wizi wa mchana. Pia wengine kuwataja kuwa walikuwa mawaziri wakati uwaziri wao ulikoma tangu tangu mwaka jana!! Ingefaa kama wangetumia neno aliyewahi kuwa waziri wa------.
Lakini kitendo cha kuwalipa tangu October ni UFISADI wa mali ya umma.
 
mkuu si ufisadi ...ukiangalia hapo kama kdr komba aliondolewa ukatibu mkuu muda sasa ..wakasema tu amepelekwa wizara ya mambo ya nje akingojea kupangiwa kazi ...lakini majina yao lazima yapelekwe nchi husika alafu wamkubali ...watu wa TISS nao wacheki ..kwa hiyo mara nyingi wao wanakuwa wanajua miezi 2/3 kabla wamekuwa mabalozi ...ila ndo hivyo vitu vinakuwa pending sasa si haki yao kuwalipa......ila nakubaliana na wewe kwenye ishu ya uwaziri ...
 
Rais JK Nyerere alimuamini Salim Ahmed Salim kumteuwa kuwa balozi wetu Egypt akiwa na umri mdogo sana, sasa ninchojiuliza hivi kuna umuhimu wowote wa kuwalipia shool fees vijana wetu pale chuo cha Diplomasia wakati nafasi zao kumbe hazihitaji uwe mwanadiplomasia zaidi ya kuwa mpika majungu mzuri wa CCM tu?
Jamani hivi ubalozi ni uteuzi wa kisiasa au unaangalia wana Diplomasia?
 
Ama kweli JK ni bonge la kilaza! Yaani watu ambao wameshindwa kukubalika na watu wao je nje watakubalika? Je watejenga mahusiano bora au watajenga mianya ya rushwa kwenye balozi zetu?
 
uteuzi uhu ni moja ya zile ahadi alizozitoa kwa wana CCM waliokosa nafasi za kuchaguliwa na wanachi katika mbio za chaguzi mkuu.......
 
Back
Top Bottom