Rais Kikwete ateua Katibu wa Ikulu

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2006
Messages
4,155
Points
1,250

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2006
4,155 1,250
Rais Kikwete ateua Katibu wa Ikulu

Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete amemteuwa Michael Mwanda kuwa Katibu Mkuu wa Ikulu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana katika vyombo vya habari na Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo, uteuzi huo unafuatia nafasi iliyoachwa wazi Rose Lugembe ambaye amestaafu kazi kwa mujibu wa sheria.

"Rais Jakaya Kikwete amemteuwa Michael Mwanda kuwa Katibu Mkuu wa Ikulu," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba kabla ya uteuzi huo, Mwanda alikuwa Naibu Katibu Ofisi ya Waziri Mkuu na uteuzi huo unaanza rasmi leo.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 

Gembe

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2007
Messages
2,505
Points
1,225

Gembe

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2007
2,505 1,225
bado kuna uteuzi mmoja haujatajwa,changa la macho hilo.hata yule aliyesaini mkataba wa RDC kwa niaba ya serikali kapewa shavu serikalini,uteuzi wote now unafanywa na EL,so anawatanguliza watu wake IKulu ili wawe wanampa habari za ndani
 

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2006
Messages
4,155
Points
1,250

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2006
4,155 1,250
hee hee mmmh sio JK eeh? haya ndio tuseme EL ndio akiachiwa ikulu huteuwa bila ya kupewa idhini na muungwana?


mmmh hatukosi la kusema, sasa tunataka kujua jee uteuzi vipi ? alieteuliwa na nafasi aliyoteuliwa inamfaa?
 

Forum statistics

Threads 1,364,029
Members 520,629
Posts 33,304,309
Top